Ikulu T
JF-Expert Member
- Aug 21, 2023
- 1,600
- 4,692
Miundombinu mibovu ndani ya jiji la Arusha.
- Barabara za lami,ndani ya jiji la Arusha barabara nyingi za lami ni nyembamba na haziendani kabisa na wingi wa magari yaliyopo.
- Barabara za vumbi,jiji la Arusha limezungukwa na barabara za vumbi kila kona,hii ni aibu kubwa sana kwa jiji ambalo ndiyo kitovu cha utalii nchini .
- Stendi za daladala,hapa sio aibu tu bali ni fedhea ya hali ya juu mfano stendi ya hiace ya kilombero,samunge,kisongo,ngaramtoni,mbauda etc stendi zote hizi ni mbovu mno.
- Stendi kuu,hapa ni zaidi ya aibu,stendi hii ni ndogo,chafu etc
- Masoko,hapa pia pana kazi kubwa ya kufanya! Masoko yote yaliopo ndani ya jiji la Arusha yana-miundombinu mibovu kupitiliza.
Wengi mtakubaliana na mimi kwamba ukiondoka Arusha ukarudi hata baada ya miaka mitano utalikuta jiji lipo vilevile hakuna mabadiliko yoyote ya maana!!
Mamlaka husika chukueni hatua tafadhali hili jiji lipo overrated sana,kuna kazi kubwa ya kufanya ili hili jiji liendana na sifa linazopewa.