SI KWELI LHRC wametoa barua inasema Tanzania imeonesha hatua kubwa katika kuimarisha demokrasia kutokana na uchaguzi wa serikali za mitaa

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu nimekutana na barua mtandaoni inasambaa inaonekana kuwa ya LHRC ina kichwa cha habari, uimarishwaji wa demokrasia uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, barua hiyo inaeleza kuwa Tanzania imeonesha hatua kubwa katika kuimarisha demokrasia kutokana na uchaguzi wa serikali za mitaa. wakuu hapa uhalisia ni upi imetolewa na LHRC kweli?

 
Tunachokijua
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) ni shirika la utetezi wa haki za binadamu nchini Tanzania. LHRC ilianzishwa mwaka 1995 kama shirika lisilo la kiserikali, la hiari, lisiloegemea upande wowote na lisilo la faida, likiwa na madhumuni ya kufanya kazi ya kuwawezesha na kuhamasisha uelewa wa kijamii, wananchi wa Tanzania kuhusu haki za kisheria na za binadamu.

LHRC imekuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha utawala wa kisheria wenye misingi ya kidemokrasia na unaozingatia haki za binadamu. Katika kulitekeleza hilo kupitia uchaguzi wa serikali za mitaa 2024 imekuwa ni moja kati ya waangalizi tangu kuanza kwa mchakato wa uchaguzi huo mpaka kukamilika, ikishiriki kwa kutoa elimu pamoja na matamko dhidi ya maovu yanayovunja demokrasia na haki za binadamu.

Kumekuwapo na barua ya taarifa kwa umma inadaiwa kutolewa na LHRC ambayo inasema Tanzania imeonesha hatua kubwa katika kuimarisha demokrasia kupitia uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024.


Je ni upi uhalisia wa barua hiyo?

Ufualitiaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck umebaini kuwa barua hiyo si ya kweli kwani haijachapishwa wala kutolewa na LHRC kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii. Hata hivyo JamiiCheck imebaini mapungufu kadha kutoka kwenye barua hiyo yanayoitofautisha dhidi ya barua rasmi ambazo hutolewa na LHRC.

Sehemu ya mapungufu hayo ni pamoja na kutofautiana kwa mstari mnene unaotenganisha sehemu ya anwani na maneno ya juu kabisa ya LHRC, Kutofautiana kwa mwandiko uliotumika kuandika kichwa cha barua ambao umekuwa na mng’ao zaidi tofauti na inavyotumika katika barua rasmi, pamoja na hayo ubora mdogo wa muonekano wa nembo (logo) ya LHRC, maandishi ya anwani, pamoja na majina ya wajumbe wa bodi yaliyopo sehemu ya chini, unaonesha sehemu hizo zilitolewa kutoka barua za awali za LHRC na kutumiwa katika barua hiyo isiyo ya kweli na kusababisha sehemu hizo kuwa na muonekano hafifu tofauti na sehemu zingine.

Aidha katika kutaka kupata uhalisia zaidi JamiiCheck iliwasiliana na LHRC ambao waliikana barua hiyo na kwamba si ya kweli, LHRC wakaenda mbali zaidi ambapo kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii iliikanusha barua hiyo hivyo kuthibitisha kuwa si ya kweli.​
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…