Mahamud_2000
JF-Expert Member
- Feb 8, 2014
- 200
- 99
Daah
Kumbe hapa napaka rangi upepo,,yaani kumuondoa kazini mfanyakazi aliefoji cheti cha taaluma wewe unaleta stori za redundancy na kushindwa kuwalipa wezi mafao,,tokea lini mhalifu akapewa tuzo,,shame!! Nafahamu hapa sasa najibizana na mtu wa aina gani.Ukiondoa hao watu wenye kazi sensitive zenye professional boards kama madaktari, serikali haiwapangii watu binafsi waajiri watu wenye viwango gani.
Kwa mfano. Serikali inaweza kuwa na kiwango kwamba dereva wa magari ya serikali ni lazima awe na leseni na cheti cha form four.
Serikali hiipangii sekta binafsi dereva awe na elimu gani, zaidi ya kuwa na leseni.
Sasa mnaposema serikali ihakiki vyeti vya sekta binafsi wakati haipangii sekta binafsi viwango vya elimu kwa kazi hizi ambazo si sensitive, serikali itahakiki cheti gani wakati haipangii sekta binafsi viwango vya elimu?
Unatakiwa kuelewa kwanza kwamba ili kuhakiki inabidi uwe na standards.
Sasa mtu binafsi akisema ninachotaka ni mtu mwenye leseni tu, ujinga wa vyeti vingi kwa kazi ya udereva tu siutaki, utataka serikali impangue huyu muajiri binafsi kwamba kwa kuwa dereva wa serikali ninkazima awe na cheti cha form four basi na wa sekta binafsi naye lazima awe na cheti cha firm four?
Kitu hicho hakiruhusiwi nabkanuni za uchumi wa soko huria tunaoutumia sasa.
Huo ninutawala wa kiimla wa kikomunisti.
Zaidi ya hapo, serikali haiwezi kuingikia sekta binafsi kwa sababu ziezi zima la vyeti feki halijalenga kuondoa watu wenye vyeti feki (lengo lingekuwa hilo kina Bashite wasingeachwa). Lengo lilikuwa kupunguza wafanyakazi wa serikali bila kuwalipa mafao, kwa sababu serikali haina hela.
Sasa huko sekta binafsi serikali haina interest kwa sababu haiwalipi watu mishahara, na kwa kweli kupunguza wafanyakazi sekta binafsi ni kuipunguzia serikali mapato yanayotokana na kodi.
Kwa hiyo zaidi ya watu wanaohakikiwa na professiinal boards kama madaktari, hawa wengine ambao wanafanya kazi zisizo sensitive sekta binafsi sahau uhakiki. Labda muajiri wa sekta binafsi atake mwenyewe tu.