kumbe unagari!!!Ha ha ha niliwatoa baru huko moro mpk meneja akaja na kushangaa hivi kuna nini jameni, ilikuwa mwaka 2009 tangu hapo nikiona utepe wa lile benki najisikiaa kinyaa sna na ole wako nifahamu we ni mteja wao hata gari yangu usipande sitaki kabisa
Wakati unaondoka uliongea na meneja au dada wa pale counter???
Kama uliongea na mdada wa counter, umetwanga maji kwenye kinu mkuu.
Wewe una mawazo kama hao wahudumu wa benki. Mawazo yao ndio hayo hayo 'aende tu na vilaki vyake .Inategemea ulikuwa na mzigo kiasi Gani mkuu, unaweza kukuta hawakushtuka wala 'kukomoka' sana.
Ukitaka kuwachanganya nbc waambie habari za INTERNET BANKING&PAY PAL,utawakubali kwa sound hapo
Sitakagi ujinga Mimi!Kuna bank moja ya nbc ipo huku kwetu na sitaitaja mahali ilipo ili kama zipo bank zenye tabia kama hii bank hizo zijirekebishe haraka sana na bila kufanya hivyo hizo bank zitakuja kubaki ni sehemu za historia. kwamba hapa kulikuwa na bank ilikuwa inaitwa nbc na haitakiwi msubili ije itokee hivyo wakati wa kujilekebisha ni sasa.
Hiyo bank ninayoisema inafanya kazi kimazoea sana na wanafanya kazi kama ni mwaka 1947 ambapo kukaa masaa 2 kwenye foleni ni kitu cha kawaida na wakati huo saizi ushindani wa kibiashara umekuwa mkubwa. watu wanataka kupata vitu kwa haraka na kwa urahisi zaidi.
mm ni mvumilivu sana lakini hii bank imenishinda. na mara nyingi ninapo ona makosa huwa sipendi kuzungunza najua hiyo ni bahati mbaya huenda ipo siku watajilekebisha. lakini naona ndio wanazidi kuwa sugu. na unakuta siku zingine naenda kutoa pesa kwenye mida ya saa 5 asubuhi na ninakuta pesa hamna hadi nikapange foleni hadi saa saa 7 mchana. na wakati huo nikipiga hesabu saizi mtu ukienda kutoa hela m pesa dakika mbili nyingi.
na nikajiuliza kwanini kila siku niwe ninahangaika na bank moja na wakati huo mm ndio ninawafaidisha na nikiwa bank mara wameandika zima simu. yani mm kazi zangu zilale wakati nipo kwenye foleni.
na huo bank ni nyingi zinatafuta wateja na wanawafungulia watu acount bure na unachagua unafungua acount gani kama ni acount ya akiba hawakukati hata sh. 10.
na nikawaza hawa wanafanya hivi kwasababu huwa hawajawahi kuonyeshwa action wamezoea kunyenyekewa.
na nilicho fanya leo nimeenda kutoa pesa zangu zote na kuwaludishi kikadi chao na nikawaambia leo nimehama bank yenu rasmi kwasabu sijaridhika na huduma zenu. na nikawa naondoka na sikutaka kuwapa maelekezo zaidi.
malengo ya kufanya hivyo ili bank ya nbc wajitathimini upya vile wanavyo fanya kazi. na kuondoka kwangu huenda hao walio baki kutawafanya wapate huduma bora. sio bora huduma.