Care Giver
Member
- Apr 2, 2024
- 69
- 204
Kuna jambo nimelifanya leo...
Leo nilikua naelekea hospitali na mgonjwa wangu... Sasa kufika maeneo flani nikasimamishwa Traffic, basi kwa kutii sheria nkasimama kwa mbele. Alikuja Traffic wakike kukagua kama gari inadaiwa na kufanya ukaguzi wao.
Baada ya ukaguzi wake akaja dirishani kuomba leseni yangu. Hapa ndio balaa lilipoanzia, nkamwambia hapa nipo na mgonjwa namuwahisha hospitali hivyo nimeisahau. Ila ki ukweli nlikuwa nayo lakini kwa kuwa inadaiwa sikutaka kuitoa. Alinkomalia sana hakuna kutoa gari mpaka ntoe leseni.
Basi nkamuuliza vipi kama nkikutajia namba maana naijua... akasema sawa ntajie.
Nkaitaja nzima nzima,"bilioni nne milioni mbili elfu tano mia tatu na nane."
Baada ya kujaribu kuandika mara kadhaa akasema hauna deni nenda, wakati mi najua nina deni kabisa.
Sasa ebu tumsaidie kuiandika kwa namba..