Leo nawatukana!

Unajua Mkuu![/QUO

Ahsante mkuu, najaribu tu. Nakumbuka miaka ya 80's nilikuwa napenda sana kipindi cha malenga wetu. Namkumbuka mmoja akijiita Boi Manda na kama sikosei kuna mzee alikuwa akiitwa Kandoro sijui kama tunaye tena. Yeye ndiye alinifanya nipende mashairi baada ya kusikiliza mahojiano yake siku hiyo. Hili litakuwa ni shairi langu la kwanza kuliweka hazarani!
 
tafuta kazi we pumbavu,badala ya kuandika kitabu "how to be rich`"au ujasisiriamali uuze km mwenzio shigongo we unaleta mashairi ya sa nane,huyo ushaambiwa na wenyewe manyumbu yupo mzima wa afya na vijiwe vyake vya kahawa anaonekana,msitupotezee muda nyumbu
andika ww mimi nisome....
 
Faru John kapotea, Serikali kashituka,
Na kaburi kufukua, mkuu alivyotaka,
Na vipimo kuchukua, muuaji kumsaka,
Faru john ni mnyama, kwa nini siyo kwa Ben?
 
Allen ndugu nakiri, tena pasina kificho,
Hao watu ni hatari, hutoa kucha na macho,
Wafanyapo uguberi, moyoni hawana kicho,
Ela sisi kwa hiyari, ndio tumewapa ficho,
ishirini ishirini, tusirudie makosa.

Sawa,

Ishirini ishirini, tusirudie makosa,
je wafikiri nini, Ben tuvavyomkosa,

alikuwa mshikaji, mawazo akichangia,
yenye ukali wa Chaji, vichwani yaliingia,
wenyewe walijihoji, wapi yalipoanzia,
je wafikiri nini, Ben tuvavyomkosa,

Tuamke, tukamsake Ben

[HASHTAG]#bringbackalivebensaanane[/HASHTAG]
 
Faru John kapotea, Serikali kashituka,
Na kaburi kufukua, mkuu alivyotaka,
Na vipimo kuchukua, muuaji kumsaka,
Faru john ni mnyama, kwa nini siyo kwa Ben?
Kwao Joni ni muhimu,
dola kitu adimu,
wazungu wakija humu,
wazijaza kwenye dumu,
wao wanazifuja!
 
View attachment 465875

Sianzi na ashakumu, leo ninawatukana,
Mwaufanya uwazimu, na mambo yaso maana,
Huu si ubinadamu, pia sio uungwana,
Ben wetu yuko wapi?

Ben hakuwa mzimu, vipi asionekane?
Kama karuka sehemu, uhamiaji wanene,
Na kama ni marehemu, mwili wake tuuone,
Ben wetu yuko wapi?

Bavicha machakaramu, Katambi una laana,
Siku saba zishatimu, Desemba mwaka wa jana,
Nyumbu twataka fahamu, komeni kulaliana,
Ben wetu yuko wapi?

UTG zenu salamu, mlipo muitikie
Sina pesa hali ngumu, fulana siniuzie,
Lengo si kuwalaumu, ila nanyi mtwambie,
Ben wetu yuko wapi?

Serikali naheshimu, ila kwa hili hapana,
Mloona kwenye simu, sasa yawekwe bayana,
Tunataka kufahamu, naye walopigiana,
Ben wetu yuko wapi?

Mboe ni mtu muhimu, ana kubwa sana dhima,
Ela naye kala ndimu, hataki hata kusema,
Kiasi ni mtuhumu, ameufanya unyama,
Ben wetu yuko wapi?

Nimtaje Jeyi Pi Emu, tuliyempa dhamana,
Mjuwe namuheshimu, ela namna hakuna,
Nahisi anayo damu, ya huyu wetu kijana,
Ben wetu yuko wapi?

Kalamu naomba koma, miye sina roho mbili,
Siniletee nakama, nikenda fichwa mahali,
Kisha niwe madhuluma, athama ni hili swali,
Ben wetu yuko wapi?

31 January 2017 Jumanne.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Call/whats app 0622845394 Morogoro.

Dotto hivi Zitto Zuberi Kabwe aka Ayatolla Khomeni yupo wapi?
 
Tusi lilipokutoka,
nikajua watashuka,
Roho imenilipuka,
moyo umesikitika,
Hawana imani.

imekuwa mara mbili,
hila zao za tumbili,
wana ndumila kuwili,
baba yao ni jahili,
wamelaaniwa.

idadi wameongeza,
wengine wamewatweza,
wamewageuza chaza,
Kimwili kuwachakaza,
Wanawatesa.

Ben kawa sumaku,
kawavuta na wa huku,
wabebwa mkuku mkuku,
kwenye kiza cha usiku,
Hawarudi.
 
The end of old circle and the beginning of new circle
 
The good shall prevail but evilness will perish forever
 
As it was at the beginning so it shall be at the end
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom