Leo natimiza miaka 5 na mke wangu, siku ya kwanza kutoka date alinipa ujumbe mzuri sana

passion_amo1

JF-Expert Member
Dec 3, 2023
1,828
3,910
wakuu habari za uzima?

Mimi na mke wangu niseme watu tunaopenda sana kusoma vitabu, sasahivi tuna mtoto mmoja handsome boy linanipa faraja sana na kunifanya niendelee kupambana.

Niseme katika watu wenye wanawake smart mimi ni miongoni mwao, mke wangu tulikutana miaka mitano nyuma.
Nadhani wote tunajua mapenzi yakiwa mwanzo, baada ya kutupa sana ndoano mwisho akakubali nikamuomba date.

basi siku ya kwanza natoka nae date jioni, tukaagiza chakula huku stori zikiendelea nyingi akiniuliza umesoma kitabu fulani na masuala ya mziki huwa nikiwa na stress zangu za kazi ananiimbia jamani huyu mwanamke acha tu😍.

Basi stori zikawa zinaendelea.

Mimi; unajua wanawake huwa mnapenda vitu vingi mbali na mziki na kusoma vitabu nini kingine?

Mke; unajua tunapokosea sisi ni kusema vitu vyote kwa mwanaume at once hivyo mwanaume ata fulfill vile vitu haraka ili apate kile ambacho anataka hiyo ni kazi yako kujua napenda nini.

Hili jibu likanifanya nijue naongea na mtu wa aina gani, nikajibu sawa.
Tukawa tunaendelea na stori sasa kipindi hicho nilikuwa nasoma(hapa bado hatujakutana kimwili) nikamwambia unajua nipo nasoma ila unajua nilijaribu kufungua biashara ya huduma za kifedha ila naona kama nikiacha mtu kuna hasara kubwa sana na nashindwa kujigawa kuwepo pale muda wote nafikiria kuacha.

Mke wangu alinipa mfano ambao mwanzoni niliuona wakijinga sana.

Akaniambia kuna stori fulani ya zamani ya kitoto ya Mbwa mmoja ambaye alikuwa akijitapa kwamba yeye ndio ana mbio sana na hakuna mnyama ambaye atashindwa kumkamata, basi siku moja mbwa yule akamuona sungura akaanza kumkimbiza sana lakini bila mafanikio hakumpata!

alivyorudi akakuta wenzake wanamcheka wakisema wewe umekuwa ukijitamba hakuna kiumbe kinachokushinda mbio vipi leo imekuwaje?

Akawajibu wenzake, mnajua mnashindwa kuelewa jambo moja mimi nilikuwa namkimbiza kama moja ya kujifurahisha kwangu, lakini sungura alikuwa anakimbia kuokoa maisha yake hivyo lazima aweke bidii kubwa kuokoa maisha yake maana hajui kama mimi ninajifurahisha au nataka kumdhuru kweli.(hii stori alihadithiwa na baba yake ni mwanasheria)

akaniambia mke wangu nafikiri unabidi uangalie biashara hiyo ina umuhimu gani kwako kwenye kukutimizia mahitaji yako.

kiukweli huyu mwanamke amekuwa chachu ya mimi kupiga hatua kila siku, niwanamke mzuri kuanzia sura mpaka akili.

Niliporudi ile siku nilifikiria sana mfano wake nikasema tu huyu ndiye niliyemtarajia.

NB: ndoa ni miaka mitatu ila mahusiano mwaka huu natimiza miaka mitano.

Kanizawadia katoto kamoja kazuri.

Wanaume share ujumbe mzuri wa mke wako au mpenzi wako?

Nawashauri wanaume wenzangu sio lazima uoe rasmi hata kwenda kujitambulisha kwa wazazi wakakujua ni jambo la Hekima sana.
 
Mkuu mke wako ni wakawaida sana na nikuhakikishi kwamba wa kawaida njoo DM...

Unapagawa na vitu vidogo hivyo kweli wewe zipompwepompwe umeoa satawang'ina hilo halafu unaaminia,njoo inbox tukuoneshe kuwa mwanamke wako wakawaida sana
 
Back
Top Bottom