Leo 03/06/17 Panya Road 12 waitingisha Rombo ya Ubungo, 3 wauawa

NI MTAZAMO TU

JF-Expert Member
Feb 20, 2014
1,203
999
Vijana watatu kati ya kumi na mbili wauawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kupita duka kwa duka wakiwa na silaha aina ya mapanga na visu kuvamia mtaa wa Kibo Rombo Ubungo.

Watu hawa walikuwa wanatoka mazishini kuzika mwenzao ambaye anasadikika aliuawa usiku wa juzi na wananchi kwa tulio la wizi maeneo ya Msewe Ubungo.

Wakiwa wanatokea kuzika wakatanda mtaa wa Rombo wakiwa na mapanga na visu ila baada ya kupora watu wengi simu na pesa,Wananchi waliwazingira na wakawamudu kwa kutumia mawe,baadhi yao wamefanikiwa kukimbia na watatu wakauawa papo hapo na kuchomwa moto.

Picha ya tukio haijapatikana kutokana na kukuta polisi wamefika na kuchukua miili ya marehemu.

Labda wenye picha na habari kamili watujuze...
 
safi
 
Wangewaua angalau nusu dazeni haki ingetamalaki
Hili tukia la saa hii mchana kulianza kama utani huku mtaani na mama wemepigwa na mabapa ya upanga. Na ilikuwa kama taharuki kwakuwa wanaingia dukani wanachukua zao na kila mpita njia unaacha simu la sivyo unakula panga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…