Etwege
JF-Expert Member
- Jul 4, 2018
- 7,095
- 17,471
Combination ya Makonda na Sabaya kwenye serikali ya awamu wa tano ilikuwa ya kuotea mbali na shida za wananchi zilitatuliwa papo kwa papo field. Sasa baada ya Makonda kurudi kama katibu mwenezi ameendelea kupiga kazi ya field bila msaidizi hivyo ndiyo maana wananchi wameanza kummis kijana mchapakazi Lengai Ole Sabaya.
Kwenye mizani Sabaya na Mbowe wote walikuwa wafungwa wa kisiasa na tuhuma za Mbowe zilikuwa ni nzito sana na ushahidi wake umetolewa na watu wakubwa ambao ni viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama lakini tuhuma za Sabaya ni nyepesi sana na ushahidi unatolewa na watu ambao tangu mwanzo wanajulikana wana chuki na Sabaya, Wengine wametamba waziwazi kwenye mabaa kuwa lazima wamkomeshe huyo kijana.
Mh rais haiwezekani ukubali kuingilia uhuru wa mahakama na kumsamehe mwana Chadema Mbowe alafu ukamuacha kijana na mtoto wako na mwana CCM mwenzako Sabaya akiteseka kwa tuhuma za uongo na uzushi alizotungiwa na wakwepa kodi na wauza madawa ya kulevya wa wilaya ya Hai.
Ni kweli chadema na wapinzani wengi wameshangilia sana kifungo cha Lengai Ole Sabaya cha miaka 30 jela lakini ukweli ambao hausemwi ni kwamba wana ccm wengi wamehuzunishwa na kuchukizwa mno na kifungo cha Sabaya.
Kwenye macho ya wazalendo wa nchi hii, Sabaya ni mzalendo wa kweli aliyejitoa kuleta mabadiliko kwa vitendo na siyo maneno kama wanavyofanya wengi.
Bila Lengai Ole Sabaya kuwa mkuu wa wilaya ya Hai haya yangeweza kutokea kwenye wilaya hii.
1. Wilaya ya Hai kupanda kwa ukusanyaji mapato kutoka ya mwisho hadi kuwa ya nne kitaifa. Kabla ya Sabaya wilaya hii ilikuwa imekithiri kwa rushwa na ukwepaji kodi.
2. Mbunge na madiwani wa ccm kushinda na kuongoza Halmashauri.
Wilaya hii ilikuwa ngome ya Chadema kwa miaka mingi na kila aliyejaribu alikiona cha mtema kuni kutoka kwa Mbowe na genge lake.
Lakini kupitia Sabaya sasa jimbo la Hai ni ngome ya CCM na itawachukua miaka mingi Chadema kulirudisha tena hasa baada ya Mbowe kuwa gaidi na kupoteza imani kwa wananchi wengi.
Lakini pia Mbowe ametangaza kuachana na siasa za majukwaani.
Kwa kifupi mbunge ,madiwani na wenyeviti mbalimbali wa wilaya ya Hai wanakula kupitia jasho la Sabaya.
3. Kurejeshwa kwa aridhi ya waislamu iliyoporwa kwa miaka mingi.
Wilaya ya Hai wamepita wakuu wa wilaya wengi lakini hakuna aliyefanikiwa kumaliza mgogoro huo mpaka Lengai Ole Sabaya alipofika na kumaliza kadhia hiyo.