Legend wa hiphop Jos Mtambo wa tongwe record rafiki wa Roma aomba msaada hali yake inasikitisha

Dr am 4 real PhD

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
12,353
25,437
Nayajua Maisha yangu mpaka TONGWE kama muvii..oooh kaa tayar...oooh... action...oohh.... Naanza mwisho kwenda mwanzo.... NGOMA Ina goooo...goooo.. nayajua Maisha yangu mpaka tongwe Kama muviiii oooh..kaa tayarii...NGOMA Ina goooo...

Hiki ni moja ya kionjo kwenye wimbo wa Roma akishirikiana na Jos mtambo na darasa....huu wimbo unaitwa KAA TAYARI...

Nimeangalia video ya Jos mtambo akiwa kwenye Hali ya ALOSTO na ulevi ULIO pindukia anatia huruma anaitaji kusaidiwa.

Nacho amini akili ya mwanadamu yeyote akiwa ana boost vilevi hufanya akili kuwa na uwezo mkubwa na upeo usio wa kawaida.

Tatizo huibuka pale wanapo kua waraibu nasikitika na Maisha ya Jos mtambo pia ninae mtu anae nihusu na yeye ana ELIMU NZURII KABISA Ila amekuja kua mlevi wa kutupwa inauma na kusikitisha Sanaa

POMBEKALI, UGOLO, BANGI VILEVI VYOTE KWA UJUMLA WAKE HAVIJAWAI KUA VIBAYA / MBAYA TATIZO NI MTU MWENYEWE HUWEZI KUSHINDANA NA POMBE, BANGI VILEVI UKABAKIA NA UTIMAMU WAKO WA AKILI.

JOS MTAMBO ATAKUA ALIKUA ANATUMIA MUDA MREFU ILA KWA SASA KUTOKANA NA OVERDOSE NA MISUSE IMEMLETEA SHIDA UKIJUMLISHA STRESS ZA MAISHA NDIO VIMEMMALIZA KABISA..

LEO Dr am 4 real PhD Napandaga daladala nashikaga bomba hakuna anae nijua 😔😊☺️ usupastaa ni zigo la miiba ukilibeba lazima utaumia.

NAONA JOS MTAMBO KAJIKATIA TAMAA ANAITAJI MSAADA.

View: https://youtu.be/Ex94EQQL8Ro?si=lN-kvrcCMs41P1RY
 
ni sehem ya maisha asinge kuwa yeye ningekuwa mm au wewe mshukuru Mungu kwa nafasi yako.
True brother.. binafsi Mimi tangia mtoto mdogo....kwetuu 80's kulikua na kioo kikubwa.. dressing table sisi watoto wa kotaa.. kwenye kile kioo kikubwa nikiwa najiangalia nikiwa mtoto nilikataa kua MTU WA OVYO OVYO.

Brother tujifunze na tukatae kua watu wa OVYO OVYO..
 
Ukweli ni kwamba Jose Mtambo ana hali mbaya ya Kiafya kwa namna mahojiano yalivyokuwa anahitaji msaada kutoka kwa Jamii.

Roma na Madee wanaposema wanyimwe Mahojiano na Media tafasiri yake ni kwamba wanataka jamii isijua maisha wanayoishi wasanii wao na je watasaidika vipi??
 
Pole yake. Maisha haya bwana. Ndio maana kuna time mtu inabid uingilie maisha yake hata kama ni uhuru wake kuish atakavyo, kwasababu unajua tu mwisho wa siku atakuja kuwa cost tu japo watu watakuona kama mchawi ila mwisho wa siku uhuru uliopitiliza bila mipaka matokeo yake ndio haya sasa. Sisi ni binadamu lazima tu tutamuonea huruma ila wakat wa starehe zake walikua wanaona watu kama wanga kuingilia maisha yao wakiwakosoa
 
Moja vichwa matata sana kuanzia tungo, flowz na stylez! Yaani mwamba kabisa..... ila ulevi aliupeda nao ukampenda, wakapendana! Ukisikiza kwa makini ngoma zake alikuwa na kibwagizo kama anatapika hivi, kama huelewi ile ilikuwa ni alama yake ya kuutukuza MCHUPA...! mimi sina cha kumsaidia zaidi ya kuiplay ngoma yake moja ya kuitwa TWENDE SASA na niburudike!
 
Yaani ukipata mtu kwenye familia yenu akawa mlevi wa aina hii ni janga kubwa Sanaa..ukimuangalia kakata tamaa
 
Pole yake. Maisha haya bwana. Ndio maana kuna time mtu inabid uingilie maisha yake hata kama ni uhuru wake kuish atakavyo, kwasababu unajua tu mwisho wa siku atakuja kuwa cost tu japo watu watakuona kama mchawi ila mwisho wa siku uhuru uliopitiliza bila mipaka matokeo yake ndio haya sasa. Sisi ni binadamu lazima tu tutamuonea huruma ila wakat wa starehe zake walikua wanaona watu kama wanga kuingilia maisha yao wakiwakosoa
Unajua mtu akifikia hiyo level anakua sikio la kufa labda mwenyezi Mungu angilie Kati maana yeye ndie hubadilisha kiumbe chochote kua kipyaa.
 
Anahitaji wataalamu wa kushape akili yake azaliwe mara ya pili.
Yaani wanaformat upya brain yako na kuiprogram upya.
Brain ikishaingia virus ni lazima uwe teja wa pombe au madawa
 
Back
Top Bottom