Bila sadaka mchungaji na familia yake watakula nini? Watavaa nini? Wataishi wapi? Maana hiyo ndio ajira yake na kila ajira inastahili ujira; Na ujira wa mchungaji ni kupitia sadaka zenu.
"Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihame-hame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii. Na mji wo wote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu;" - Luka 10:7-8
"Ni askari gani aendaye vitani wakati wo wote kwa gharama zake mwenyewe? Ni nani apandaye mizabibu asiyekula katika matunda yake? Au ni nani achungaye kundi, asiyekunywa katika maziwa ya kundi? Ikiwa sisi tuliwapandia ninyi vitu vya rohoni, je! Ni neno kubwa tukivuna vitu vyenu vya mwilini? Hamjui ya kuwa wale wazifanyao kazi za hekaluni hula katika vitu vya hekalu, na wale waihudumiao madhabahu huwa na fungu lao katika vitu vya madhabahu? Na Bwana vivyo hivyo ameamuru kwamba wale waihubirio Injili wapate riziki kwa hiyo Injili." - 1 Wakorintho 9:7, 11, 13, 14
Vyote ni hiari yako kusali na kutoa sadaka au kusali bila kutoa sadaka au kusali na kutoa sadaka. Makanisa yote hayana magereza kwa kutofanya mojawapo hufungwi hata mara moja. Lakini kama imani yako inakutuma kuwa ni bora kuliendeleza kanisa lako kwa kuwapa mahitaji muhimu wahubiri wako, na kuwasaidia kuwafikia wasiona uwezo wa kuwapa mafuta na kwenda kwao...kwa kufanya hivyo unasaidia kuinjilisha pia.
biashara hiii jmn hata sijui itaisha lini, bwana tuokoe
Siku hizi kuna matangazo radioni na kwenye tv ( wanalipia) ya wapi kanisa la mchungaji fulani lilipo au matangazo ya barabarani linakuelekeza wapi kanisa lilipo,unadhani wanafanya hivo hili iweje ??????
"..Siku hizi za karibuni inaonekana sadaka ni pesa tu, na kwenye makanisa kuna vikapu zaidi ya vi tano kwa ajili ya sadaka. lakini sadaka ya kweli ni kumpa chochote mtu aliyena na uhitaji.."
Aliye nacho ataongezewa na asiye nacho hata kile kidogo alichonacho atanyang'anywa....Umeshaambiwa hapo juu usiende kanisani kama huna michango...ila ile ya kanisani sio sadaka ni michango....kama ilivyo michango ya harusi.
mimi hapo napita sijataja kanisa yapo mengi hapa darMlima wa moto
TAG
Sasa hilo la kuwekwa kimakundi sijawahi kuliona live, nasikia tu; Kwa sababu inategemea dhehebu na dhehebu. Kama waumini wameridhia iwe hivyo sioni tatizo, otherwise kama hawajaridhia wanapaswa kuwasilisha mapendekezi yao kwenye baraza lao, nafikiri huu ni utaribu mzuri na rasmi.asante kwa huu uchambuzi mzuri na kuvitoa vifungu kabisa kutoka biblia JE UNAONA NI HAKI KUPANGIWA KIASI CHA KUTOA kama sadaka? na je kuwekwa kimakundi kisa umetoa kiasi kikubwa ni sahihi NI LAZIMA TUMLISHE MCHUNGAJI LAKINI NDO TUWEKWE KWENYE MAKUNDI KISA UMETOA KIASI FULANI? sadaka ni siri lakini siku hizi sio siri wa elfu kumi mbele na mia tano nyuma sahihi ivo?
"..Mungu akuongezee thawabu kama umelitambua hilo.."kabisa na huyo ndie anaebarikiwa UMEMPITA KILEMA BILA KUMSAIDIA eti sadaka yako itapokelewa na MAKANISA YA SASA HIVI WALIVO ROHO NGUMU mwenye uhitaji akijitokeza hawamsaidii wakati sadaka inafaa itumike kote
vyema umenena mkuu swali kwako umeamua kuliendeleza kanisa kama maelezo yako mara unaambiwa kama una sadaka ndogo wewe nyuma waanze wa kuanzia elfu kumi kwanza ndipo nyinyi wenye ndogo mtafuata hiyo kauli unaichukuliaje sio unyanyapaa vipi yule mjane angenyanyapaliwa kisa alitoa kiasi kidogo lakini huyo akaonekana katoa kingi kuliko wote[/QUOTE
Richards, naamini kauli hiyo ni moja kati ya chache za makanisa mengi na waumini wanaofurika katika makanisa hayo. Ikitokea kwangu nitaichukulia kama ni udhaifu wa mchungaji wangu ambaye kwa vyovyote najua si malaika. Yeyote anayeanzisha kisichokuwa cha Mungu tunajua hakitadumu ila tukipinga cha Mungu hata tufanyeje kitadumu (Matedo ya Mitume 5:38-39). Hivyo kama mchungaji huyo ni wa mambo ya dunia uwe na uhakika ataishia na mambo yake.
Sasa hilo la kuwekwa kimakundi sijawahi kuliona live, nasikia tu; Kwa sababu inategemea dhehebu na dhehebu. Kama waumini wameridhia iwe hivyo sioni tatizo, otherwise kama hawajaridhia wanapaswa kuwasilisha mapendekezi yao kwenye baraza lao, nafikiri huu ni utaribu mzuri na rasmi.
Serikali ni lazma iingilie kati hawa watu cwema tena, kuanzia makanisa makubwa hata madogo wote mafisadi tu,ndio maana Mimi huwa nawakubali waislam hawanaga ujingaujinga kama wetu