Nangu Nyau
JF-Expert Member
- Jul 1, 2022
- 4,790
- 13,664
Kiongozi/ mtumishi yeyote wa umma akiugua na kwenda nje kutibiwa iwe Kwa gharama zake au za Serikali. Wananchi tuandamane aje atibiwe hapa kwenye hospitali zetu hizi kama Amana nk.
Aliyekujulisha yupo sahihi, na makondoo pia, siyo"mapaka" tu.Nasikia unafuga mapaka?
Hawa wengi wao elimu zao za magumashi sema tu wanabebwa na ma Godfather wao wengi wao wamesoma hapo IFM, diploma za Banking wakawa chawa wa maMD waliokuwepo enzi hizo na kukabidhiwa vijiti vya u CEO, utaona mtoa CV hajaandika shule na vyuo alivyosoma, wapo wengi kwenye taasisi za kifedha hasa benki.Nyingi nafasi za kubebwa na Mzee wa Msoga tu. Kipimo halisi n̈I alipokuwa CEO wa NBC na namna alivyofeli vibaya kiuongozi hadi kutolewa na makaburu
Kwani kuugua UKIMWI ni dhambi sijui kwanini watu mnaogopa kusema marehemu kafa kwa UKIMWI? Raisi Kaunda na Mandela waliwahi kutangaza kuwa watoto wao wamekufa kwa UKIMWI, kusema mtu kafa kwa UKIMWI si dhambi na kifo kipo tu hata ukisema au usiseme kuhusu Ukimwi siku ikifika utaondoka tu. Kuogopa UKIMWi ni kujidanganya ,UKIMWI upo na unampata mtu yeyote.HIi ni post ya taarifa ya kifo, unaposema ukimwi unaua unamaanisha nini? Unless huelewi hata maana ya kitu unachoandika eti? Au wewe hutokufa?
Mm nimechelewa nipo ya 39 mpk watoto walalae naahidi siruki hata mojaUko video ya ngapi hadi sasa? Wengine wapo ya 276 hawana haraka kuruka clip
Rip dudeView attachment 3147717
Lawrence Nyasebwa Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango amefariki Dunia leo Novemba 9, 2024 katika hospitali ya Apollo nchini India.
Rais Samia Suluhu Hassan ameandika katika Mitandao yake ya Kijamii kuhusu Kifo cha Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango,
View attachment 3147755
"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru, Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango kilichotokea leo tarehe 09 Novemba, 2024 katika hospitali ya Apollo nchini India.
Ninatoa pole kwa familia, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji) Mheshimiwa Prof. Kitila Alexander Mkumbo, watumishi wa Tume ya Mipango, ndugu jamaa na marafiki kufuatia msiba huu.
Bw. Mafuru atakumbukwa kwa utumishi wake uliotukuka, bidii na ubunifu alipotumikia nafasi mbalimbali ndani ya Serikali.
Mwenyezi Mungu aijalie familia yake subra na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu na ailaze roho yake mahali pema."
Wasifu wa Mafuru
Lawrence Mafuru ni mtaalamu mashuhuri wa masuala ya fedha mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika benki, uwekezaji, na sera za serikali. Ni Certified Chartered Banker kutoka Taasisi ya Wataalamu wa Benki ya London na pia ni Certified Financial Markets Dealer aliyeidhinishwa na ACI Financial Markets.
Alianza safari yake mwaka 1998 katika Benki ya Standard Chartered, akijikita katika Ufadhili wa Biashara za Kimataifa. Kwa kipindi cha zaidi ya miongo miwili iliyofuata, alishika nyadhifa mbalimbali za uongozi katika sekta ya fedha nchini Tanzania, ikiwemo kuwa Mkuu wa Hazina katika Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, na Mwenyekiti wa Chama cha Mabenki Tanzania (TBA).
Uzoefu wake unaenda zaidi ya benki za biashara, kwani pia aliwahi kuhudumu kama Msajili wa Hazina katika Wizara ya Fedha. Kama mamlaka inayotambulika katika masuala ya benki na fedha, Bw.
Mafuru huombwa mara kwa mara kuwa mzungumzaji kwenye mijadala ya sekta hiyo. Ana shauku ya kutumia utaalamu wake ili kuleta manufaa kwa wateja na wadau wake.
Kabla ya nafasi yake ya sasa, Bw. Mafuru alichangia pakubwa katika kuunda sera za uchumi za Tanzania. Alihudumu katika Wizara ya Fedha kama Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera na baadaye kama Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Sera za Usimamizi wa Uchumi.
Hadi kifo kinamkuta, Bw. Lawrence Nyasebwa Mafuru alikuwa akihudumu kama Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango.
Muogope Mungu unamuonea kwa hilo binafsi namfahamu Mafuru na makandokando yake ila hilo mtake radhi hata kama hatakusikia ishu yake ni (EKIA) majasusi wamenielewa.Alikuwa jizi,tu, wala simungunyi maneno,huyu na mkapa, ndio waliuza NBC benk kwa bei ya kutupa, Maghu alimtumbua alipokuwa hazina,kizimkazi, akamrudisha,
TZ is better off without him, he used is expertise to plunder and steal!
Yeye ndio wa kwanza kufa na ukimwi?UKIMWI unaua. Rest in peace bro.
Imeandikwa kwenye Sehemu ya Tatu ya Katiba. Ibara ya 51 Ibara ndogo ya (2)Imeandikwa wapi katika Katiba ya Tanzania nionyeshe tafadhali.
Agree that was how simple he was.R.I.P pengo lako litazibwa kesho tu.
kwenye nini alimgomea?RIP mwamba uliyemgomea jiwe
Wow! Nikidhani ni mimi pekee niliona ili...nikasema labda ana high testosteroneUnaanza kujisahau mwandiko unabadilika na kuwa wa jinsia nyingine.
Jamaa yupi? 🤣Inna li Llahi wa inna Ilayhi rajiun.
Kafanana sana na yule jamaa, tofauti ni rangi zao tu, yule mweupe, huyu mweusi.
Utajaza mwenyewe.Jamaa yupi? 🤣
Mafuru ni majina common kwa wajita ni sawa na jina Chacha,Marwa au Mwita kwa WakuryaPole kwa familia nzima,naomba kuuliza Kuna huyu mwingine nae huitwa Ephraim Mafuru,Hawa ni ndugu