muuza ubuyu
JF-Expert Member
- Nov 23, 2010
- 3,536
- 3,525
Mkuu vijana wa siku hizi hawayatumii mamlaka na nguvu zao kama wanaume.Watoto wa siku hizi mna jinsia za kiume ila roho na maamuzi yakike
hapo ni kwamba
asha mi nataka kuoa na nitafunga ndoa ya kikristo,
badili dini au niruhusu nitafute wa dini yangu,
umemaliza.
Wakati nataka kuoa baba mkwe alikatalia nimlipe mahari kubwa na mimi muoaji nilikuwa najigharamia kila kitu hivyo nikaona isiwe tabu.
Nilimpigia simu mchumba wangu (by then ulikuwa mwaka wetu wa 9 katika mahusiano) kwamba mimi nahitaji kukuoa wewe kwa sababu tumetoka mbali na tumepitia magumu mengi, wewe wajua uwezo wangu, mwambie baba yako kama atashindwa kupokea hii mahari niliyonayo basi naahirisha kuoa mpaka pindi nitakapopata anazozitaka (lengo langu kumweka katika hali ngumu ili amshawishi baba yake kukubali nilichokuwa nacho). Baada ya hapo nikampigia baba yake ni nikamwambia mzee wangu shukrani ila mahali niliyonayo ndiyo hiyo sina zaidi mzee wangu. Kama utakuwa umenikubalia kumuoa mwanao basi naomba utanitaarifu baada ya wiki moja kama utakuwa umenikubalia au la. Haikufika hata wiki moja akapiga simu kunikubalia na mambo yakasonga mbele.
Mahari nilitoa yote ili asije akanisumbua mbele ya safari. Mpaka leo ananiheshimu na hata akiwa na shida ananipigia simu mimi na siyo mwanaye.
Mwanaume unatakiwa kuwa diplomatic lakini ukiona vitu haviendi use your power!
Sent using Jamii Forums mobile app