Yusuph Salehe
Member
- Nov 12, 2010
- 58
- 1
Kwa wataalam wa lugha naombeni msaada wenu. Katika sentensi kama hii HA-KU-CHEZ-A Je nini kazi ya "KU" zaidi ya kuonesha wakati uliopita?
Ku- inaweza kuwa na dhima kadhaa katika maneno lkn inategemea muktadha,
kutokana na mfano ulioutoa,kimofimu, dhima yake ni hiyo uloitaja tu.Ikitokea
katika muktadha tofauti ndo huweza kubeba dhima nyingine,
Hainoyeshi wakati uliopita pekee maana pamoja na "HA" inaonyesha pia ya kwamba kazi haikutendeka maana ni kinyume cha "LI" inayoonesha pia wakati uliopita ("alicheza").Kwa wataalam wa lugha naombeni msaada wenu. Katika sentensi kama hii HA-KU-CHEZ-A Je nini kazi ya "KU" zaidi ya kuonesha wakati uliopita?
KU- HUWEZA KUWA NA DHIMA ZIFUATAZO:
1. Kudokeza wakati uliopita katika tendo linapokuwa katika ukanushi
mf: Hakucheza
2. Kudokeza mtendwa jambo (nafsi ya pili - wewe)
mf: amekupiga wewe
3. Kudokeza idadi (umoja)
mf: amekuona (umoja) wingi : wamuwaona
4. Huweza kuwa ni sehemu ya mzizi wa neno.
mf: kumbuka, kumbatia, kung'uta nk
5. Husaidia shina la kitenzi cha silabi moja
mf: i)kula, shina -kul-, mzizi -l- ; amekula,tutakula,amenilia,mlaji,sili,mlo,nk
ii)kufa, shina -kuf-, mzizi -f- ; amekufa,tutakufa,amenifia,hafi,kifo,nk
*vitenzi vingine vyenye mfumo huo ni kuja,kunya,kunywa,nk
*ktk mifano i na ii hapo juu tumeona -ku- imeweza kuonadoka kadiri
tulivyokuwa tunanyambua kwa vile husaidia shina -kul- na -kuf- na wala sio
sehemu ya mzizi wa maneno km ilivyo ktk 4 hapo juu.
6. Hudokeza upatanisho wa kisarufi.
mf i) Kuchakachua kumezidi
ii) Kule kuna kiza.
7. Huunda kitenzi jina
mf kusoma, kuimba, kulima
HA na KU ni neno moja HAKU, na linasimama kama kielezi cha kitendo ambacho kwenye sentensi hiyo ni CHEZA...!Kwa wataalam wa lugha naombeni msaada wenu. Katika sentensi kama hii HA-KU-CHEZ-A Je nini kazi ya "KU" zaidi ya kuonesha wakati uliopita?
HA na KU ni neno moja HAKU, na linasimama kama kielezi cha kitendo ambacho kwenye sentensi hiyo ni CHEZA...!
Mf: Haku-Kimbia, Haku-imba, Haku-Kataza/zwa, Haku-muita, vile vile linaweza kutumika peke yake, kama vile umetoa shutuma fulani kwa mtoto naye akakujibu "Haku mimi sikuwepo"
Tunapoandika kwa kuanzia na Siku-*** na kumalizikia na kitendo, hapo inaonyesha umimi, yaani nafsi ya kwanza katika kupinga au kukataa jambo au kitendo...! Mf: Siku- iba, Siku- mkamata, Siku-mpiga, Siku-mdhurumu, Siku-muona, Siku-mtarajia n.k.Una hakika? "Siku - Kimbia" - kwa maana ile ile - ni silabi 2 pamoja lakini si neno?
HA na KU ni neno moja HAKU, na linasimama kama kielezi cha kitendo ambacho kwenye sentensi hiyo ni CHEZA...!
Mf: Haku-Kimbia, Haku-imba, Haku-Kataza/zwa, Haku-muita, vile vile linaweza kutumika peke yake, kama vile umetoa shutuma fulani kwa mtoto naye akakujibu "Haku mimi sikuwepo"
Hi yote sawa kabisa.Tunapoandika kwa kuanzia na Siku-*** na kumalizikia na kitendo, hapo inaonyesha umimi, yaani nafsi ya kwanza katika kupinga au kukataa jambo au kitendo...! Mf: Siku- iba, Siku- mkamata, Siku-mpiga, Siku-mdhurumu, Siku-muona, Siku-mtarajia n.k.
Nashukuru kwa ujumbe huu lakini najitahidi sana kukumbuka kama nimemsikia mtu kusema vile. Sikumbuki.HAKU linakuwa ni neno lenye kujitegemea pale mtu anapo tuumiwa kufanya jambo fulani na yeye hakakanusha kwa kutamka neno "HAKU sikuwa mimi"
Huwa linatumika sana hasa na wasichana!Nashukuru kwa ujumbe huu lakini najitahidi sana kukumbuka kama nimemsikia mtu kusema vile. Sikumbuki.
Je kuna uwezekano ya kwamba ni neno lililo kawaida kieneo tu? Labda athira ya lugha jirani ya kikabila?
Maana yake ni nini?
Kuna uwezekano ni lahaja kwa "hakika"? Au ni kuongeza ukanusho?
Karibu tena na tena!Nashukuruni sana jamani kwa majibu yenu mmenipa mwanga mzuri na nimeridhika na majibu yenu mliyoyatoa ahsanteni sanaaa