Kweli mambo ya Tanga yapo hivi au makusudi tu?

torvic

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
3,968
9,822
Aje aje wadau,

Daah! Mapenzi bana kweli ni ubunifu lakini sio kwa ubunifu huu ulionitokea mimi, sitaki kubwabwaja sana kama lara..

Ipo ivi kuna mtoto wa kike nimekuanae kama miezi kadhaa hivi, mtoto mwenywe wa kitanga na kama mnavojua story za Tanga na mapenzi yao ya kuunga maji ya kuoga iliki, mdarasini, karafuu nasikia mpaka nyanya wanaweka sikuizi

Sasa mimi nimefanyiwa hayo mambo na uyo mtoto wa kitanga alafu mimi sipendi sasa habari hizo na nimemwambia sana tu mimi sifagilii mambo hayo

Kilichonisibu sasa juzi ameshinda geto ile narudi namkuta ameaanda maji ya kuoga ya moto lakini sio Yamoto Bend ameweka maviungo yake kibao namaliza kuoga nakaa kidogo yani mwili wote ulikuwa unawaka moto kinoma alafu kulikuwa akuna joto kivile.

Sasa mpaka saivi najiuliza aliweka nini sijui kwenye yale maji na nikimuuliza ananikenulia tu kama daktari wa meno, uamuzi naotaka kuufanya ni kumpiga chini anazingua na maviungo yake lakini wadau mimi kaswali kangu kamoja tu aliweka nini mule?

Imefika.
 
Alichanganya na JIK
 
Unaomba ushauri au unatoa taatifa

Na humo itakuwa alikuwekea sprit
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…