Ramsy Dalai Lama
Senior Member
- Apr 5, 2021
- 154
- 551
Kwanza kwa kuanzia tu, ni kwamba tukija upande wa "kiufundi" ningesema sifa tatu muhimu kwenye mpira ni: intelligence, communication, and discipline. Inafahamika kuwa Xavi ni mchezaji mwenye akili, bila shaka ni mmoja wa wachezaji wenye akili sana ndani ya uwanja. Yeye si mchezaji mwenye kipawa zaidi katika masuala ya ustadi wa kucheza chenga za mwili au dribbling skill au physicality ila hata hivyo alikuwa kwenye kinyanganyilo cha FIFA World Player of the Year/Ballon d’Or na Messi (mwenye dribbling skill) na C. Ronaldo (mwenye physicality/nguvu pamoja chenga za mwili) kwa sababu tu ya akili yake akiwa uwanjani.
Nadhani kila mtu anakubali kwamba creative mindset and insight ni moja ya sifa muhimu zaidi kwa kocha / meneja. Xavi huwa anafikiria hatua za mbele wakati wa mchezo na kuwa na maono mazuri. Kila wakati anapopokea mpira, anajua mazingira (position and movement ya wachezaji), na hupanga hatua zinazofuata ipasavyo. Kwa kuzingatia ni muda mfupi tu hutumika kwa Xavi kwa upangaji huu, hivi mtu anaweza kufikiria jinsi ubongo wake unavyofanya kazi haraka?. Xavi pia ana ustadi mzuri wa mawasiliano na wachezaji na charisma, kwa hivyo Guardiola alimtumia kama msaidizi wake kwa upande wa mchezaji "mzungumzaji" au "mtoa maelekezo" uwanjani. Na mawasiliano ni muhimu kwa kocha/meneja ili kuwapa wachezaji wako ari au motisha (man management) na sifa hii Xavi yupo nayo.
Pia Xavi ana pendwa na mashabiki Barca, na hii itawapa mashabiki imani na kuzidi kum support hata kama mwanzoni mambo hayataenda vizuri kwasabab tu wataamini anatengeneza timu ambayo itawapa mafanikio mbeleni. Lakin pia hata ushirikiano ndani ya management ya Barca utakua mkubwa, watamsikiliza na kumpa ushirikiano wa hali ya juu kwasabab ni mchezaji mwenye historia nzuri na heshima ndani ya club na Spain kwa ujumla.
La mwisho kabisa, ni jambo ambalo watu wengi watakua wanasahau ni kwamba Xavi alikuwa/ana kiwango bora cha kazi pale Barca kama mchezaji. Enzi za Guardiola, tuliona jinsi viungo wa Barca walivyokua wanazuia wachezaji pinzani wasiwe na mpira na kuhakisha Barca inakaa na mpira muda mwingi ili kupunguza mashambulizi kwenye safu ya ulinzi ya Barca. Na kinara wakuhakikisha hili linafanikiwa alikua ni Xavi akishirikiana na Iniesta na kiungo mkabaji Busquet. Kwa hiyo Xavi alikua ni mmoja wa wachezaji wenye bidii zaidi pale Barca, na inasemekana alikimbia kilomita 12 kwa wastani wakati wa enzi za Guardiola. Hii ina maana kwamba Xavi ni mchezaji mwenye nidhamu, na ndiyo kitu unahitaji ili uwe kocha/meneja mzuri. Marehemu R.I.P lengend 🙏 Maradona alikuwa mchezaji mzuri sana, lakini hakuwa na nidhamu ya soka na ndo maana ali failed kwenye ukocha). Kwa hivyo, sifa hizo, kwa maoni yangu, zitamfanya Xavi kuwa kocha/meneja mzuri wa Barcelona.
Ila kwa kuweka akiba ya maneno muda nao utasema lolote laweza tokea, Mimi kama shabiki wa FC Barcelona namuombea tu Mungu afanikiwe, ili tupate burudani mashabiki wa soka. Chao 🤘