Kwanini wengi hukiogopa kifo /kufa?

We
Wengi huogopa kifo nahisi kwakuwa hatujui tutakufaje, i mean namna tutakavyoondoka.
Kwamagonjwa
Ajali barabarani
Kuchinjwa
Kufa ukiwa umesinzia/kuzirai
Kupigwa na kitu kizito
Kwarisasi n.k

Hebu fikiria unapita mahala fulani unakuta watu wamejazana, unauliza kulikoni wanakwambia nenda ujionee. Unasikia wamama wanaangua vilio vya hofu na uchungu, ghafla unashuhudia mwili wa binadamu ukiwa umeraruliwa kwa kuchanwachanwa kwa kisu au panga. Lazima utafeel hali ya uchungu alioupata kabla ya umauti kumfika. Kuna muda huwa nqwaza mwenyewe, mbona ninapochinja mnyama/ndege sina hofu wala kuhurumia kiumbe kinapotikisa mwili kwa maumivu? Lakini kwa binadamu ni hali tofauti kabisa.

Ngoja nitoe mfano kidogo. Zamani tangu ningali mdogo, sikuwa nikiogopa kabisa kuangalia video za mauaji (maigizo) hasa za kuchomana visu na kupigana mapanga. Ila tangia mwaka 2015 hadi leo, ninapatwa na hofu sana ninapoona mtu anachomwa kisu ama kukatwa panga, kwann? Mwaka huuo ndio nilishuhudia documentary ilihusu vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone. Haikuwa video ya kutengenezwa, ilikuwa halisi kabisa (on the battlefield) ilifika mahali hata mwandishi mwenyewe anajibanza sehemu kukwepa risasi. Ilinitisha mpaka leo. Niliona tofauti ya vita, na maigizo ya vita. Kama kuna watu nawaona maadui kwangu, ni wale wanaoomba VITA ITOKEE ILI KULETA HESHIMA. Vita isikie kwa jirani tu. Jiulize mtaani kwako umelala ukasikia risasi nje, unakuwa na hali gani. Halafu hiyo ndiyo iwe desturi yako ya kila siku asubuhi mchana na usiku. Kifo kisikie tu lakini ukweli unabaki palepale pamoja na kuwa tumeumbiwa kusahau, KIFO HAKIZOELEKI ndio maana mtu akifa sasahv, watu watalia weee ghafla akifa mwingine tena wakati mnaomboleza, hofu itaanza upya na mshituko utatokea sawa nq yule wa kwanza
 
KIFO HAKIZOELEKI ndio maana mtu akifa sasahv, watu watalia weee ghafla akifa mwingine tena wakati mnaomboleza, hofu itaanza upya na mshituko utatokea sawa nq yule wa kwanza
 
Mimi binafsi naogopa kifo kwa sababu sijui nini kitaendelea baada ya kufa kitendo cha kifo kua fumbo lisilofumbuka ndio naamini knawafanya watu wengi wakiogope
 

Misss u
 
Mshana:

Nikupongeze kwa andiko lakini ningependa kuweka mawazo yangu. Kifo kina hatua:

Hatua ya kwanza ukiwa mzima na mwenye afya mtu akikwambia unakufa unakataa na mtabishana hiyo inaitwa "Denial"

Hatua ya pili unapokuwa kwenye hatari na unaona hapa sasa sina nakufa nafsi na roho na mwili unakubali unaona hakuna tena jinsi na ndiyo maana usiku wagonjwa wengi huwa wanafikiria kutubu nakuomba wapumzike kwa amani. Hiyo inaitwa "Acceptance".

Lakini ukiwa mtenda mema kifo ni njia ya ushindi ila ukweli kwa mwanadamu ni kuwa kifo hakizoeleki.
 
nimekupata
 
@Mshana Jr mimi binafsi kifo hakinitishi sana pengine kinachonitisha ni ugonjwa ule au ajali inayoweza kunipelekea kifo na mbele huko adhabu zinazotajwa za JEHANAM na nyinginezo' ndio maana naswali sana naepukana na madhambi na kwaupande mwingine naona mtu akifa hatojiskia sawa na usingizi usiokua na njozi au hatojiskia sawa na mtu bado haja zaliwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…