Kwanini Wanajeshi wengi wakipewa Mkopo hukimbilia kununua tu Magari na si kujiendeleza Kimaisha?

Wengi ulituhesabu ukajua idadi yetu na kutambua ni wangapi wana magari ya mikopo?

Maisha ya mtu ni yake acha kuyachunguza, hiyo mikopo haikuhusu na wala hakuna mwanajeshi hata mmoja anakuhusu kaa kimya.

Maisha ni mafanikio ya kupata kile anachotaka sio kila mtu anataka kujiendeleza kimaisha
 
I wanajeshi tu, ni wafanyakazi wa Siri Kali wote wanaigana. Hili ni baada ya kunyanyasana kwa maneno.

Pia hili liko Vyuo vikuu kwa wakufunzi kuigana kwa kubadilisha magari
 
Hizi mada mziache huko huko fb... Kwan wewe mwanajeshi kununua gari inakuhusu nin?? Katika maisha umeambiwa kila mtu mpk ajenge? Unaweza jenga lkn nyumba yako na banda la mbuzi visiwe na tofaut... Mbna hamwasem wahind wanaomilik magar ya mamilion lkn wanakaa kwenye nyumba za NHC?? Ukiona maisha magumu kwako kaa kimya angalia wenzako wanavosukuma kete za mchezo..
 
Mkuu wewe unaielewaje hii sentensi "kujiendeleza Kimaisha?"

Kwa uwezo wa ufikiri wangu, hata kununua gari ni sehemu ya kujiendeleza kimaisha.

Unless otherwise proven wrong.

Kama unanunua Gari halafu unaliendesha kwa siku 3 mpaka 5 tu za mwanzo wa mwezi na siku 2 hadi 4 za katikati ya mwezi kisha unalipaki na kuanza kuwasumbua Watu wakupe mtonyo wa kujaza mafuta ili upite nalo tena Kitaani kuoshea nyota kisha mwisho wa mwezi ukifika Mshahara wako wote unaishia kulipia madeni yako ya mizinga ndiyo maendeleo yako ya kimaisha unayosema basi ni sawa Mkuu.

Hata hivyo nafurahi tu kuwa wapo Wanajeshi wengine wajanja na wana akili ambapo wao wakipewa tu Mkopo haraka sana huwa kununua Uwanja na kuanza Ujenzi wa Nyumba zao na cha kuchekesha kama siyo kusikitisha utakuta kuna mwingine alichukua Mkopo akaenda kununua Gari lakini akiishiwa anaenda kuishi kwa muda kwa mwenzake yule yule ambaye Mkopo wake aliutumia Kujengea mjengo wake.
 
Labda wanajeshi wa huko kwenu ndiyo hawajamka, ila wa huku kwetu wanamijumba huwezi amini. mfano: eneo Kibaha ukianzia maili moja mpaka miembe Saba, wanajeshi wengi wanaishi kwenye nyumba zao, kuna sehemu wanaita kwa Banduka, nyumba nyingi eneo hilo ni wanajeshi, mpaka wanapaita Darfuu. wapo wazembe wa maisha ila ukweli kizazi hiki wengi wana nyumba zao. wataalamu husema, kama umeweza kununua gari ina maana una kipato pia cha kukuwezesha kujenga, hivyo basi tunachotofautiana ni kipaumbele tu uanze na nini.
Hata mimi namshangaa huyu mburura, sijui kaitoa wapi hii nayo? Hao walikuwa wanajeshi wa zamani, mbona madogo wanaporomosha majumba ya hatareeee? Nina wadogo zangu wawili wako jeshini kila mmoja ameshajenga nyumba nzuri tu, mwingine keshajenga nyumba mbili za maana. Sasa hao wanaoishia kununua magari ni wa wapi hao?
 
Hivi kweli nyie hii mitandao inwaharibu mtu kama wewe hujawahi hata kukesha hata siku moja leo unaita Askari wa Jeshi washamba...njoo basi uwafundishe waache ushamba njoo hapa Mgulan
 
Mimi cna jibu lolote mkuu wangu tusubirie majbu toka kwa wajuvi

Huyo Komando ambaye sasa ni Marehemu uliyemweka katika Avatar yako hapo Lieutenant ( Luteni ) Rajab Mlima kuna Mtu ananiambia kuwa baada ya kupigwa risasi na Sniper kule DR Congo alichowafanyia wale Waasi wa M23 japo alikufa katika battle kamwe hawatakuja kukisahau maishani mwao.

Baba yake Mlezi Balozi Mzee Tambwe wa pale Makonde Mbezi Beach kila mara humkumbuka huku akimsifu kuwa Jamaa alikuwa ni Shujaa wa uhakika na kwa jinsi shughuli yake nilivyoisikia huku nyingine nikipewa na Washikaji zake ama hakika Tanzania imepoteza moja ya Komandoo wake mahiri, mweledi, makini na wa kutukuka.
 
Nature ya kazi ya jeshi hasa la ulinzi Tanzania si wafanyabiashara, hivyo hawana ndoto kama zako za kuwa big businessman.
Jambo lingine ni kwamba wanajeshi si watu wenye tamaa ya mali/pesa kama walivyo wafanyakazi wa kada zingine, maadamu analipiwa pango(kama amepanga) umeme, posho ya chakula anapewa, akivuta taswira atakapostaafu ana pesa isiyopungua mil.100 wakati huo tayari alishajenga nyumba ya kumtosha na familia yake why asinunue gari?.
Do you know the meaning of BAKABAKA?
 
Tungefanya unayotaka Nooo wangefanya unayotaka ungepata wapivcha kuandika by the way uhakika WA maisha ya baadae upo ndo maana hakuna haraka hiyo
 
Kujenga kukariri tu! labda wewe kujenga ndo unaona ishu kubwa, mfano nyumba nzima ya kawaida kwa mwaka tuchukulie mil 5 kupanga, mfano unaishi miaka 70 sasa hapo si itakuwa 5'000'000?*70yrs sawa na milioni 350, sasa mili 350 si hela ya kawaida tu kuipata.
 
Hata mapolisi,

Unakuta amepark magari matatu hapo nje ya chumba alafu anagongana makalio na vitoto kordo kwenye choo cha kotaz za polisi zaidi ya miaka 15.

Mkuu umenifanya nicheke hadi Njemba zinanishangaa hapa. Kuna Kaka yangu mmoja ni Ndata ( Police ) aliishi sana pale Kota zao za Stesheni mkabala na Makao Makuu ya Trafiki na haya uliyoyaandika ndiyo uhalisia / ukweli wenyewe na hata Mimi nilikuwa namshangaa mno ila namshukuru Mungu alipata akili za kujiongeza na Alhamdullilahi kajitahidi kujenga na kuwekeza na pale kawaacha akina nanihii waendelee kutanua huku wakiwa hawana hata Banda la Kufugia Kuku.

Mkuu umejuaje life style yao hii? au na Wewe ulishawahi kuwa mwana Kota za Police kwani umepatia mno kuwaelezea.
 
Yaani huku mtaani imekuwa fashion.
Kila mwanajeshi ninayemjua anamiliki gari sasa hivi.
Akipita lazima mjue kapita mana huo mziki anaoufungulia mpaka unajiuliza kama wewe uliyeko nje unaona kelele je huyo wandani ya gari hali ipoje.
Hiyo speed sasa.
Ila hii nimeiona kwa vijana wenye late 20s na early 30.
Watu wazima sijaona kwakweli.
Hongera kwao pia.

Kuna eneo moja hivi waliweza kulikabili kikamilifu kabisa hilo tatizo lao la kupenda kupita na Magari yao huku wakiwa wameweka sauti ya juu kwa kuwategeshea Misumari kila mara na wengi wao walikoma na sasa hivi hata kama wakiwa wanatoka huko watokako wakifika tu hilo eneo limepewa jina la danger zone hupunguza kabisa sauti ya Magari yao na huwa ni wapole na sometimes huwaamkia hata Watu wa pale kwa adabu zao zote.

Nakubalina na Wewe kwa 100% kuwa wenye huu u hovyo hovyo ni wale wenye 20's na 30's ila kwa Wale aged ones wana busara na hekima ya ajabu na ni nadra mno kuwaona au kusikia kuwa wamefanya upuuzi fulani japo na Wao siku ukiingia anga zao ndiyo utajua kwanini Nyoka hana Ugoko kwa shughuli yao utakayopewa.
 
Nimepitia comment zote za wadau mbalimbali nimejifunza kuwa wengi wenu hamjui chochote kuhusu jeshi mmekalia wivu tu kwa makamanda waacheni wale matunda ya nchi yao!

Nadhani kwa hii Kauli yako ni kama vile unawatukana Watu humu. Mkuu kumbuka JF ni darasa huru na humu kuna wengine tunapapenda kwasababu kumetusaidia kujua kujenga hoja, kuburudika na hasa hasa kuelimika hivyo ulichokisema Wewe ni tofauti kabisa hata na JF Motto isemaye " Where We Dare To Talk Openly ".

Hawa siyo Watu wa Kwanza kuzungumziwa humu JF kwani hata Taasisi zingine NYETI kama JWTZ nazo huwa tunazijadili humu na nia siyo kuwadhihaki Watu bali ni Kujengana. Huwezi jua pengine uzi huu unaweza kuwa msaada mkubwa kwa Watu fulani au ukasaidia jambo fulani.

Kuna Watu nchi hii wameifanyia makubwa kuliko hata hao unawasifu na Taifa lako au Nchi yako pamoja na Serikali nzima mpaka leo bado inawatambua na kuwaenzi. Kufanikiwa au kuwa Shujaa wa nchi siyo lazima uwe Mwanajeshi Mkuu bali hata Raia tu anaweza kuwa na mchango mkubwa sana katika Maendeleo ya nchi yake. Siku nyingine jikite katika kujenga hoja na siyo kuja humu na kutokwa na mapovu utadhani umekunywa juice ya OMO Detergent au TOSS.
 
Back
Top Bottom