Ngamanya Kitangalala
JF-Expert Member
- Sep 24, 2012
- 501
- 1,214
Kwa miaka mingi kumekuwepo na baadhi ya Wakenya wamekuwa wakisema na kutangaza huko duniani kuwa Mlima Kilimanjaro unapatikana ndani ya nchi yao.
Ni jambo ambalo limekuwa likiendelea kwa muda mrefu sana,mpaka kufikia kwa baadhi ya wageni( watalii) kutoka nchi mbalimbali duniani, kuamini kuwa mlima huo mrefu kabisa barani Africa kweli unapatikana nchini Kenya.
Ukipata muda tafuta kitabu kinaitwa "Why Tanzania is where it is: Tanzania's Colonial Boundaries from the Berlin Conference, 1884-1885 until its independence" kitabu hiki kimeandikwa na mjerumani Profesa Heinz Schneppen.
Kwenye kitabu hicho, kinaeleza kuwa kabla ya mwaka 1890 mlima Kilimanjaro na bandari ya Mombasa, zote zilikuwa Kenya,
kwenye himaya ya Waingereza.
Lakini baadaye kukawa na mabishano makubwa sana, kati ya waingereza na wajerumani kwenye kugombea umiliki wa ziwa Victoria
Sababu kubwa ya mabishano hayo, ilikuwa ni kutafuta chanzo cha mto Nile, ndani ya ziwa Victoria, kwa sababu kwa wakati huo, ilikuwa ukipata chanzo cha mto Nile unakamata Sudan, Misri na bahari ya Mediterranean, ambayo ilikuwa ni muhimu sana kwa wakati kwa sababu ya usafirishaji kwa bara la Ulaya.
Baada ya Uingereza kupata chanzo cha mto Nile, kule Jinja nchini Uganda, ndipo wakakubaliana kuchora mipaka upya kupitia mkataba wa Ango- Germany treaty wa tarehe 01 July 1890, ambapo Ujerumani walipewa 51% ya ziwa Victoria
Ndipo mpaka wa himaya ya wajerumani (Tanganyika) ukahama kutoka kusini ya Musoma na kupanda juu mpaka kaskazini ya Musoma haya yameelezwa kwenye kitabu kinaitwa "International boundaries of East Afrika", kilichoandikwa na A.C McEwen mwaka 1971
Ambapo sasa mlima Kilimanjaro na Mombasa zote zikaangukia ndani ya himaya ya wajerumani ( Tanganyika)
Kwa hiyo sasa, bandari zote katika pwani ya Afrika mashariki, zikawa zimeingia ndani ya himaya ya wajerumani ( Tanganyika)
Ndipo Waingereza wakaomba kupewa Mombasa ili na wao wawe na bandari
Na ndio mstari ule wa mpaka ukapindishwa pale kwenye mlima Kilimanjaro na kunyosha mpaka chini, ili Mombasa iwe ndani ya himaya ya Waingereza
Nadhani ndio sababu mpaka leo Wakenya wengi wanaamini mlima Kilimanjaro ni mali yao, kitu ambacho sio sahihi, Mlima Kilimanjaro uko Tanzania, kutokana na mipaka iliyochorwa na wakoloni