young solicitor
JF-Expert Member
- Dec 26, 2015
- 1,123
- 713
ukomo wa kuwa mwenyekiti chadema ulikuwa ni awamu ngapi ???FREEMAN MBOWE ASHINDA NAFASI YA UENYEKITI CHADEMA
Jamii
Posted On Monday, 15 September 2014 04:15 Written by mjengwablog
Rate this item
(0 votes)
![]()
Freeman Mbowe akiwasalimia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema.
Freeman Mbowe ameshinda tena nafasi ya Uenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa baada ya kupata jumla ya kura 789 huku mpinzani wake Ngambaranyela Mongatero akipata kura 20.
![]()
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema wakifuatilia mkutano huo.
Mbowe ameshinda nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu wa chama hicho uliofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara imechukuliwa na Prof. Abdallah Safari aliyepata kura 775 za ndiyo huku kura za hapana zikiwa 34 baada ya kuwa mgombea asiye na mpinzani.
Makamu Mwenyekiti Zanzibar ni Said Issa Mohamed aliyepata jumla ya kura 645 huku mpinzani wake Hamad Mussa Yusuph akiambulia kura 163.GPL(P.T)
na kwanini uliongezeka???
zidumu fikra za mwenyekiti
yani tabia zote za kiccm zimeamia upinzani