Kwanini uthubutu?

Richard mtao

JF-Expert Member
May 13, 2018
217
242
Habari wana JF.
Leo katika tafakari zangu nimejiuliza kwanini vijana wengi au watu wengi wanakwama sana au wanaogopa kuthubutu, nikapata majibu kwamba:-
1. Wengi wetu hatujiamini katika kile tunachodhani tunahitaji
2. Wengi tunaogopa kuchekwa ama kukosolewa na watu wengine
3. Malezi tuliyopewa na wqzazi au walezi wetu yaligubikwa na mambo mengi yaliyotujengea hofu na uoga toka tulipokuwa watoto mpaka utu uzima.
4. Wengine ni kwasababu ya matukio mabaya yaliyowahi kuwatokea maishani mwao.
5. Wengine kukosa fursa ya kufanya jambo hivyo kukosa ile hali ya kujiamini kutokana na kutokuwa na uzoefu fulani.
6. Wengine kuchelewa kujitambua.
7. Wengine tamaduni zao na wengine kutokuwa na ndoto au malengo fulani.


Pamoja na hayo yote nakubaliana na waandishi mbalimbali, viongozi, walimu, viongozi wa vyama vya ushirika, vyama vya siasa, taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali kwamba mafanikio ya mtu yanategemea mambo mengi sana ikiwemo uthubutu wa kufanya jambo fulani, kwakua uthubutu kwanza utakupa fursa ya kujifunza, pili utapata fursa ya kuonesha uwezo wako katika kufanya mambo, tatu itakusaidia kujipata na kujiimarisha zaidi katika kitu unachofanya.


Nnachotaka kukazia hapa ni kwamba mafanikio katika jambo lolote yanategemea mindset yako katika kufanya jambo lakini pia namna unavyopokea mambo au vitu mbalimbali, lakini pamoja na haya ni lazima ufungue ubongo wako na kuwa tayari kwaajili ya kujitoa kufanya jambo fulani ambalo unahisi kwa namna moja au nyingine litakusaidia kufikia ndoto na malengo yako. Sio uthubutu kwa kuanza na jambo kuubwa ambalo kimsingi hata ukithubutu kulianza utashindwa tu, anza na vitu vidogo venye uhusiano wa moja kwa moja na jambo kubwa unalotamani kufanya baadae.

Hii itakuwezesha kuelewa zaidi kila hatua muhimu ya jambo husika na kukufanya kuwa bora zaidi katika kufukuzia ndoto yako kubwa.

Mfano kwa wanafunzi wa shule za sekondari mpaka vyuoni ambao wanahofu kubwa sana ya kuonesha walichonacho au kiufupi tunaita hawajiamini( lack of confidence).

Wanaweza kujijengea ujasiri wa kufanya mambo mbalimbali kwa kuanza kutumia nafasi wanazopata wakiwa darasani mfani, kuuliza maswali, kujibu maswala, kuchangia mijadala lakini pia wanaweza kutumia majukwaa ya siasa na uongozi vyuoni au mashuleni ili kujihimarisha zaidi. Kadri wanavyofanya ivi wanazidi kufungua potentiality zao na uwezo mkubwa wa kuthubutu.

Alikadharika kwa watu wazima ambao hawapo katika taasisi hizi wanaweza kubadili mtizamo wao na kuanza kutumia fursa wanazopata kujijengea ujasiri zaidi na kujiboresha.

Mfano kwa mjasiriamari/ mfanyabiashara anaweza kujijengea hali kubwa ya kuwa uthubutu kwa kupunguza hofu au mawazo hasi juu ya matarajio fulani, pale unapowaza biashara fulani punguza hofu ya kusema ntapata hasara au ntafirisika badalaa yake waza namna ya kung'ang'ana ili ufanikishe.

Kupitia mawazo hayo yatakupa nguvu na utapata ujasiri wa kusongambele la mwisho wa siku utakuwa na uwezo mkubwa wa kufanya uthubutu wa mambo makubwa ikiwemo kufanya uwekezaji mkubwa sana katika biashara yako/zako.

Hii inadhihirisha kila kitu kinaanza na "mtizamo".

Waweza kushea chochote juu ya uzi huu tuendlele kujifunza
 
Ulilosema ni kweli mkuu
Mfano mzuri ni kwenye SoC kila anayefungua uzi ni new member, kwamba expert members hawafungui nyuzi?

Utagundua watu hatujiamini!
 
Ulilosema ni kweli mkuu
Mfano mzuri ni kwenye SoC kila anayefungua uzi ni new member, kwamba expert members hawafungui nyuzi?

Utagundua watu hatujiamini!
Nakubaliana naww kiongozi, ila Soc hapa umejiacha kwakwel?
 
Back
Top Bottom