Kwanini Unaamini Mungu yupo?

Viumbe wengine!!!kina nani hao? Me najua dunia ndio sayari inayowezesha viumbe kuishi sababu kuna uhai. Hao viumbe wengine mi siwajui zaidi ya kusoma dhana za kufikirika, Hivyo swali lako ni imagination na unaweza kujijibu kwa kuimagine
Hata Mungu ni dhana ya kufikirika na imaginations za watu wa kale zinazorithishwa kila panapokucha.
 
Hata Mungu ni dhana ya kufikirika na imaginations za watu wa kale zinazorithishwa kila panapokucha.
Mungu sio dhana ya kufikirika. Mungu yupo na anajidhihirisha kwetu kwa utukufu wake mkuu. Tazama dunia na vyote vilivyomo, jitazame na wewe unavyoishi ukipumua pumzi,ukinyeeshewa na mvua, ukipata mazao yanayokua na kukupatia chakula.

Kisha piga magoti chini na umuabudu Mungu na kuutukuza utukufu wake. Acha kukaza shingo iyo, itavunjika!
 
Mungu sio dhana ya kufikirika. Mungu yupo na anajidhihirisha kwetu kwa utukufu wake mkuu. Tazama dunia na vyote vilivyomo, jitazame na wewe unavyoishi ukipumua pumzi,ukinyeeshewa na mvua, ukipata mazao yanayokua na kukupatia chakula. Kisha piga magoti chini na umuabudu Mungu na kuutukuza utukufu wake. Acha kukaza shingo iyo, itavunjika!
Una uhakika gani kwamba vitu ulivyovitaja ni Mungu aliyeviumba?
 
Una uhakika gani kwamba vitu ulivyovitaja ni Mungu aliyeviumba?
Uhakika ninao wa uhakika kupitia kitabu kitakatifu cha Biblia mambo hayo yameandikwa. Halafu tujiulize ni nani au kiumbe gani mwenye uwezo wa kufanya mambo hayo makubwa? Yupi anaweza kuumba sayari, binaadamu na nyota za angani? Yupi mwenye uwezo wa kutoa uhai kwa viumbe vyote?

Jibu ni wazi kuwa hakuna mwenye huo uwezo mkuu ila Mungu wa Majeshi. Amini ili ujifunze na kuuona utukufu wa Mungu uliokuzunguka, nje na nda yako
 
Uhakika ninao wa uhakika kupitia kitabu kitakatifu cha Biblia mambo hayo yameandikwa. Halafu tujiulize ni nani au kiumbe gani mwenye uwezo wa kufanya mambo hayo makubwa? Yupi anaweza kuumba sayari, binaadamu na nyota za angani? Yupi mwenye uwezo wa kutoa uhai kwa viumbe vyote? Jibu ni wazi kuwa hakuna mwenye huo uwezo mkuu ila Mungu wa Majeshi. Amini ili ujifunze na kuuona utukufu wa Mungu uliokuzunguka, nje na nda yako
Kitabu cha Bibilia kimejaa kila aina ya uovu unaojulikana.Kinajipinga chenyewe wala hakina mantiki kwenye kuandikwa kwake.Hivyo hakifai kutumika kama ushahidi juu ya uwepo wa Mungu.
Je una ushahidi gani kwamba Bibilia ni kitabu cha Mungu?
 
Ukiangalia jinsi mambo yalivyo kwa undani,kuhusu miti,wadudu,wanyama,ndege,binadamu,bahari,anga,upepo,madini nk...utagundua kua Mungu hayupo kabisa

Kama Mungu yupo inabidi aseme yeye chanzo chake ni nini?

Mana mpaka leo...watu wa dini hawajui Mungu/Allah alitoka wapi,lakini pia wanasayansi nao hawajui chanzo cha sayari na nyota na viumbe vingine.

Kwa ufupi mpaka sasa hakuna taarifa sahihi kuhusu Mungu na Dunia
Mungu ameandika mimi nipo ambae nipo.
Biblia inasema Mungu ni roho.

Wewe unaangalia ndege , wanyama, wadudu unasema Mungu hayupo?

Labda nikuulize ulimwengu huu umetokeaje?
 
Mantiki inakueleza Mungu yupo....

Labda tatizo lipo kwenye kutafakari tu na kufikiri.Mungu na dini ni vitu visivyohusiana moja kwa moja....
 
Kitabu cha Bibilia kimejaa kila aina ya uovu unaojulikana.Kinajipinga chenyewe wala hakina mantiki kwenye kuandikwa kwake.Hivyo hakifai kutumika kama ushahidi juu ya uwepo wa Mungu.
Je una ushahidi gani kwamba Bibilia ni kitabu cha Mungu?
Tukitaka hii mada iwe nzuri tusihusishe dini moja kati ya hizi zote tuziweke katika kundi moja

Kwani zote Kuna baadhi ya maswali hazijibu

Mimi pia nipo upande wa hiyo dini yako
 
Tukitaka hii mada iwe nzuri tusihusishe dini moja kati ya hizi zote tuziweke katika kundi moja

Kwani zote Kuna baadhi ya maswali hazijibu

Mimi pia nipo upande wa hiyo dini yako

Utakuwaje upande wa dini yangu ilihali mimi sina dini?
Nikisema dini ni mchezo wa kitoto unaochezwa na watu wazima namaanisha Uyahudi, Ukristo, Uislamu,[Hizi dini za Abraham ndizo zilizoharibu dunia] pamoja na dini za mashariki kama vile za wahindi, wachina na wajapani.
Hata upagani naupinga kwa maana mpagani ni mtu anayeamini uwepo wa Mungu bila kupitia/kuamini dini yoyote.Mbaya zaidi hana ushahidi wa uwepo wa Mungu.

Mimi napenda watu wawe huru juu ya maisha na akili zao.Simaanishi kwamba tusiwe na morality bali nataka watu wajue kuwa hata pasipo hizi dini za kuletwa pamoja na huyo Mungu wa kufikirika, bado watu watakuwa na maadili mema.
 
Mungu ameandika mimi nipo ambae nipo.
Biblia inasema Mungu ni roho.

Wewe unaangalia ndege , wanyama, wadudu unasema Mungu hayupo?

Labda nikuulize ulimwengu huu umetokeaje?
Labda nikuulize wewe, Mungu alitokeaje?
 
Kitabu cha Bibilia kimejaa kila aina ya uovu unaojulikana.Kinajipinga chenyewe wala hakina mantiki kwenye kuandikwa kwake.Hivyo hakifai kutumika kama ushahidi juu ya uwepo wa Mungu.
Je una ushahidi gani kwamba Bibilia ni kitabu cha Mungu?
Biblia ni kitabu cha Mungu, kwa sababu kilichoandikwa kinamhusu Mungu, dunia na binaadamu kwa ujumla. Biblia inaelezea mwanzo wa binadamu, kupotoka kwake, harakati za kumkomboa na mwisho wake hapa duniani. Kiingine kile ni kitabu kitakatifu inabidi uwe na roho mtakatifu ndo utajifunza na kufunuliwa mengi, bali ukisoma biblia kwa lengo la kutafuta udhaifu na mapungufu,utajikuta unabaki kama ulivyo na kuichukulia jinsi unavyofikiri
 
Toa ushahidi kwamba Bible ni kitabu cha Mungu........acha porojo mkuu.
 
Back
Top Bottom