Kwanini Tundu Lissu hafai kuwa Mwenyekiti wa TLS?

Habari wadau,

Kwa takribani wiki sasa kumekuwa na mjadala mkali juu ya Mgombea wa Uenyekiti wa TLS Mhe. /Mwanaharakati /Wakili Mahiri Tundu Antipas Lissu.

Nimaamini Kamati ya Uchaguzi ya TLS, kwa kuwa inaundwa na mawakili wote, Na katiba yao wanaifahamu kwa undani zaidi wamezingatia vigezo vyote vya kisiasa, kisheria na kimaadili kupitisha jina la Tundu Lissu, Na kwamba Lissu anakidhi sifa na Vigezo vya kuwa Mwenyekiti wao, wao Mawakili.

Hivyo basi ni jukumu Lao wenye chama kuamua matakwa yao bila ushawishi wa taasisi yeyote ya Nje.

Mjadala ulioanzishwa juu ya kumkataa Lissu umejengwa katika dhana ya Hofu, Uchama na Ukandamizaji wa taasisi zenye weledi katika kuhakikisha sheria za Nchi zinalindwa.

Hoja ya Mwakyembe kwamba Wajumbe wawe makini na kumchagua Lissu, Na kwamba anaweza kuifuta taasisi, sio tu ni kinyume cha sheria bali ni maelekezo mahsusi kwa Wagombea tofauti na Lissu, kwamba Serikali inawapigia kampeni Wagombea wengine kwa kigezo cha kukifuta chama.

Kwa kifupi Lissu anafaa, Na mawakili wanaoona nyakati, Na matakwa ya Nchi kwa sasa wanajua nini cha kufanya. Niwatakie Uchaguzi mwema. It's time to draw a bold line.

To go for Mwakyembe au To go for National Interest.
unajiit Dr. wakati hujui hata TLS inaongozwa na nani .... Mwenyekiti ni huko kwenye mavyama yenu yasiyojali utawala wa sheria .... TLS President to be is Tundu Lissu
 
Lissu ana uwezo mkubwa sana kuliko hata wewe mleta nyuzi hii unawezaje kumkosoa mtu aliekuzidi wa kufikiri na kute na kutetea jambo nimepima uwezo wako kwa hoja yako dhaifu isiyo na mashiko...
mkuu hebu rudia kisoma maelezo yake utamuelewa vizuri!
Mbona jamaa ameelezea vizuri kabisa! sasa unachopinga nini?
 
unajiit Dr. wakati hujui hata TLS inaongozwa na nani .... Mwenyekiti ni huko kwenye mavyama yenu yasiyijali utawala wa sheria .... TLS President to be is Tundu Lissu
Siamini kama umesoma heading tu ukakimbilia kucomment!
Hebu rudi usome maelezo yake ya ndani utamuelewa vizuri
 
Habari wadau,

Kwa takribani wiki sasa kumekuwa na mjadala mkali juu ya Mgombea wa Uenyekiti wa TLS Mhe. /Mwanaharakati /Wakili Mahiri Tundu Antipas Lissu.

Nimaamini Kamati ya Uchaguzi ya TLS, kwa kuwa inaundwa na mawakili wote, Na katiba yao wanaifahamu kwa undani zaidi wamezingatia vigezo vyote vya kisiasa, kisheria na kimaadili kupitisha jina la Tundu Lissu, Na kwamba Lissu anakidhi sifa na Vigezo vya kuwa Mwenyekiti wao, wao Mawakili.

Hivyo basi ni jukumu Lao wenye chama kuamua matakwa yao bila ushawishi wa taasisi yeyote ya Nje.

Mjadala ulioanzishwa juu ya kumkataa Lissu umejengwa katika dhana ya Hofu, Uchama na Ukandamizaji wa taasisi zenye weledi katika kuhakikisha sheria za Nchi zinalindwa.

Hoja ya Mwakyembe kwamba Wajumbe wawe makini na kumchagua Lissu, Na kwamba anaweza kuifuta taasisi, sio tu ni kinyume cha sheria bali ni maelekezo mahsusi kwa Wagombea tofauti na Lissu, kwamba Serikali inawapigia kampeni Wagombea wengine kwa kigezo cha kukifuta chama.

Kwa kifupi Lissu anafaa, Na mawakili wanaoona nyakati, Na matakwa ya Nchi kwa sasa wanajua nini cha kufanya. Niwatakie Uchaguzi mwema. It's time to draw a bold line.

To go for Mwakyembe au To go for National Interest.
Hafai kabisa!! Ataleta UCHADEMA kwenye mambo ya msingi!!
 
Nitawadharau na kuwashangaa hao mawakili/wanasheria ambao siku zote wanaitwa wasomi kama hawatamchagua msomi Tundu Lissu halafu eti wafuate ushauri wa 'mwakiembe', sijui 'mwakipapai"!
Hii nchi ni ajabu,watu washapigwa biti kitambo,hukuona juzi mkuu wa Sheria alichosema ?
 
Lissu ana uwezo mkubwa sana kuliko hata wewe mleta nyuzi hii unawezaje kumkosoa mtu aliekuzidi wa kufikiri na kute na kutetea jambo nimepima uwezo wako kwa hoja yako dhaifu isiyo na mashiko...
mkuu msome tena mleta uzi baada ya hapo some comment yako
 
Habari wadau,

Kwa takribani wiki sasa kumekuwa na mjadala mkali juu ya Mgombea wa Uenyekiti wa TLS Mhe. /Mwanaharakati /Wakili Mahiri Tundu Antipas Lissu.

Nimaamini Kamati ya Uchaguzi ya TLS, kwa kuwa inaundwa na mawakili wote, Na katiba yao wanaifahamu kwa undani zaidi wamezingatia vigezo vyote vya kisiasa, kisheria na kimaadili kupitisha jina la Tundu Lissu, Na kwamba Lissu anakidhi sifa na Vigezo vya kuwa Mwenyekiti wao, wao Mawakili.

Hivyo basi ni jukumu Lao wenye chama kuamua matakwa yao bila ushawishi wa taasisi yeyote ya Nje.

Mjadala ulioanzishwa juu ya kumkataa Lissu umejengwa katika dhana ya Hofu, Uchama na Ukandamizaji wa taasisi zenye weledi katika kuhakikisha sheria za Nchi zinalindwa.

Hoja ya Mwakyembe kwamba Wajumbe wawe makini na kumchagua Lissu, Na kwamba anaweza kuifuta taasisi, sio tu ni kinyume cha sheria bali ni maelekezo mahsusi kwa Wagombea tofauti na Lissu, kwamba Serikali inawapigia kampeni Wagombea wengine kwa kigezo cha kukifuta chama.

Kwa kifupi Lissu anafaa, Na mawakili wanaoona nyakati, Na matakwa ya Nchi kwa sasa wanajua nini cha kufanya. Niwatakie Uchaguzi mwema. It's time to draw a bold line.

To go for Mwakyembe au To go for National Interest.
Kuanzia mwanzo umekosea. TLS si chama cha mawakili kama unavyotaka watu waamini. Hata huyo Dr Mwakyembe ni mwanachama wa TLS. Tulia, Chenge, AG, Jaji Mkuu na wanasheria wote ni wanachama wa TLS.

TLS kama vilivyo vyama vingine vya kitaaluma hususani MAT (Kwa madaktari) na CWT (kwa waalimu) kwa mjibu wa sheria ya kuanzishwa kwake havipaswi kujihusisha na masuala ya kisiasa.

Ni hatari sana kwa mstakabali wa nchi vyama hivi vikiruhusiwa ama vikiingiliwa na wanasiasa. Ni mwaka juzi tu tuliona madhara haya pale chama cha MAT kilipoingiliwa na wanasiasa wa upinzani. Hivi sasa tunashuhudia yale yanaowapata Wakenya kuelekea uchaguzi mkuu kupitia chama cha madaktari wanaodai nyongeza ya mshahara ya mara 300.

Tusitake kuleta mzaha kwa vyama hivi. Nguvu ya vyama hivi ni kubwa vikiingiliwa na siasa. Nguvu ya Chama cha Waalimu Tanzania ni balaa kuliko vyote kama kitajihusisha na siasa. Ni ukweli usiopingika kuwa Tundu Lissu ni mania wa siasa (political mania), hivyo ni dhahiri akipewa urais wa TLS chama hicho hakitabaki salama. Kitageuka kuwa mkono wa chadema na hivyo kukiuka sheria ya uanzishwaji wake na kulazimisha mamlaka zilizokianzisha kukifuta.
 
duuu kwahiyo akiwa wa upinzani ni nongwa ila akiwa ccm haina kosa
 
Hata kama angekuwa ni wakutoka chama cha ccm. Tena angekuwa ccm ndiyo hatari zaidi. Just imagine Dr Tulia awe rais wa TLS!!! Ama Dr Kingwangala awe rais wa MAT ama Prof. Ndalichako awe rais wa CWT?

Hawa wanataaluma walioamua kuingia kwenye siasa ni vyema wakaachana au wakalazimishwa kuachana na masuala ya vyama vyao vya kitaaluma. Kutakuwa na conflict of interest.
 
Wewe ni Mwakiembe kabisa yaani..tunawasema wenzetu Nyumbu kumbe wewe ni kondoo hasa..tusiishi kwa kulishwa maneno. Tusiishi kwa hofu kuu na ya juu..tuishi maisha yetu tutabarikiwa. Pamoja na uanachama wangu hai wa CCM nasema LISU akachangamshe TLS imelala mnoo..
 
Kwa hiyo na Dr Mashinji akachangamushe MAT imelala mno?
 
Mods tafadhali nawaomba mfikirie kuanzisha sheria/kanuni ya kuwafungia wanachama watakaokuwa wanachangia bila kusoma uzi husika na kuuelewa,maana hii sasa ni matumizi mabovu ya rasilimali. Mpaka sasa kuna wachangiaji wanne ambao ama uelewa wao ni hafifu sana au wamesoma kichwa cha habari tu kikilaza kilaza na kukimbilia kuchangia.
 
Hata kama angekuwa ni wakutoka chama cha ccm. Tena angekuwa ccm ndiyo hatari zaidi. Just imagine Dr Tulia awe rais wa TLS!!! Ama Dr Kingwangala awe rais wa MAT ama Prof. Ndalichako awe rais wa CWT?

Hawa wanataaluma walioamua kuingia kwenye siasa ni vyema wakaachana au wakalazimishwa kuachana na masuala ya vyama vyao vya kitaaluma. Kutakuwa na conflict of interest.
Hivi kwaakili ya kawaida unaweza kuwapata watu wasio na vyama tanzania hii!
Nafikiri mawakili sio wendawazimu mpaka wakampitisha TL
 
Shida si kuwa mwanachama wa chama fulani cha siasa. Shida ni kuwa ni mfanyakazi wa chama cha siasa, yaani kipato chako cha kuendesha maisha kinatokana kwa kiasi kikubwa na shughuli za chama chako cha siasa. Kwa mfano mbunge, waziri, spika, rais wa nchi, diwani na kadhalika. Tundu Lissu si mwanachama tu wa chadema, yeye ni mwanasiasa tena mwanaharakati wa siasa za chadema. Ni kiongozi ndani ya chadema na ni mbunge kupitia chadema. Anapokea kipato kikubwa kutokana na shughuli zake hizo za kisiasa ambazo zinalipa kuliko huo uwakili wake.
 
Habari wadau,

Kwa takribani wiki sasa kumekuwa na mjadala mkali juu ya Mgombea wa Uenyekiti wa TLS Mhe. /Mwanaharakati /Wakili Mahiri Tundu Antipas Lissu.

Nimaamini Kamati ya Uchaguzi ya TLS, kwa kuwa inaundwa na mawakili wote, Na katiba yao wanaifahamu kwa undani zaidi wamezingatia vigezo vyote vya kisiasa, kisheria na kimaadili kupitisha jina la Tundu Lissu, Na kwamba Lissu anakidhi sifa na Vigezo vya kuwa Mwenyekiti wao, wao Mawakili.

Hivyo basi ni jukumu Lao wenye chama kuamua matakwa yao bila ushawishi wa taasisi yeyote ya Nje.

Mjadala ulioanzishwa juu ya kumkataa Lissu umejengwa katika dhana ya Hofu, Uchama na Ukandamizaji wa taasisi zenye weledi katika kuhakikisha sheria za Nchi zinalindwa.

Hoja ya Mwakyembe kwamba Wajumbe wawe makini na kumchagua Lissu, Na kwamba anaweza kuifuta taasisi, sio tu ni kinyume cha sheria bali ni maelekezo mahsusi kwa Wagombea tofauti na Lissu, kwamba Serikali inawapigia kampeni Wagombea wengine kwa kigezo cha kukifuta chama.

Kwa kifupi Lissu anafaa, Na mawakili wanaoona nyakati, Na matakwa ya Nchi kwa sasa wanajua nini cha kufanya. Niwatakie Uchaguzi mwema. It's time to draw a bold line.

To go for Mwakyembe au To go for National Interest.
Kwa sababu unamtaka huyo mwingine awe mwenyekiti wa TLS kwa matakwa yako.
 
Back
Top Bottom