Kwanini Tanzania tunaamini viongozi lazima wawe masikini au watokane na familia masikini?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
1,042
4,765
Mtu kuwa maskini Tanzania ni kigezo iikoja wapo cha uongozi kwenye jamii. Kigezo cha umaskini kimefungamanishwa na kilimo hivyo kila kiongozi anaamini ni mtoto wa mkulima na kwamba ni maskini anayekwenda kuwatetea maskini.

Matokeo yake masikini amekuwa kila akipata maungo yanalia mbwata means anapoteza maono dhidi ya maskini wenzake anajipanga kuwa tajiri. Na kwakuwa watu tunachukia matajiri basi automatically inabidi masikini anapopata ajitenge na maskini ajiunge na matajiri. Kwa mantiki hiyo maskini anaendelea kukosa mtetezi bali anaendelea kutumika kama daraja la kutengeneza wasaliti na wezi wanaojiita watoto wa maskini.

Nchi ikitaka kuendelea kwa maskini kutaka kujikomboa kupitia maskini ni kazi sana. Nchi inapaswa kulazimisha matajiri wengi wawe viongozi ili watumie muda mwingi kujadili utajiri wao na kuwekeza mawazo ya utajiri ambayo yatatoa ajira na maskini wengi watajikwamua.

Unachagua masikini anawaza kujenga na hivyo sera zake na fikra zinabaki kuwaza posho za vikao na rushwa huku malengo yake makubwa yakiwa amiliki gari na ghorofa kabla uchaguzi mpya haujafanyika.

Matajiri wanawazi namna ya kutunga sera na sheria za kulinda utajiri wao. Masikini anawaza kutunga sera zakupambana na matajiri na misingi ya utajiri.

Tukiamua kutochagua masikini tukaamua kuchagua matajiri kila mtu atakaye tamani kuongoza watu atafanya kazi awe tajiri kwanza. Tutaondoa watu ambao wanataka uongozi wakaibe wawe matajiri. Piga vita umaskini chagua tajiri.
 
labda kwa sababu tanzagiza > 95% ni masikini au wamelelewa na wazazi masikini, hakuna mtanzagiza asiye na umaskini …
 
Mtu kuwa maskini Tanzania ni kigezo iikoja wapo cha uongozi kwenye jamii. Kigezo cha umaskini kimefungamanishwa na kilimo hivyo kila kiongozi anaamini ni mtoto wa mkulima na kwamba ni maskini anayekwenda kuwatetea maskini...
Na Hao Hao ndo wanatulizaaa
 
Mtu kuwa maskini Tanzania ni kigezo iikoja wapo cha uongozi kwenye jamii. Kigezo cha umaskini kimefungamanishwa na kilimo hivyo kila kiongozi anaamini ni mtoto wa mkulima na kwamba ni maskini anayekwenda kuwatetea maskini.

Matokeo yake masikini amekuwa kila akipata maungo yanalia mbwata means anapoteza maono dhidi ya maskini wenzake anajipanga kuwa tajiri. Na kwakuwa watu tunachukia matajiri basi automatically inabidi masikini anapopata ajitenge na maskini ajiunge na matajiri. Kwa mantiki hiyo maskini anaendelea kukosa mtetezi bali anaendelea kutumika kama daraja la kutengeneza wasaliti na wezi wanaojiita watoto wa maskini.

Nchi ikitaka kuendelea kwa maskini kutaka kujikomboa kupitia maskini ni kazi sana. Nchi inapaswa kulazimisha matajiri wengi wawe viongozi ili watumie muda mwingi kujadili utajiri wao na kuwekeza mawazo ya utajiri ambayo yatatoa ajira na maskini wengi watajikwamua.

Unachagua masikini anawaza kujenga na hivyo sera zake na fikra zinabaki kuwaza posho za vikao na rushwa huku malengo yake makubwa yakiwa amiliki gari na ghorofa kabla uchaguzi mpya haujafanyika.

Matajiri wanawazi namna ya kutunga sera na sheria za kulinda utajiri wao. Masikini anawaza kutunga sera zakupambana na matajiri na misingi ya utajiri.

Tukiamua kutochagua masikini tukaamua kuchagua matajiri kila mtu atakaye tamani kuongoza watu atafanya kazi awe tajiri kwanza. Tutaondoa watu ambao wanataka uongozi wakaibe wawe matajiri. Piga vita umaskini chagua tajiri.
Mawazo mufilisi kabisa. Mawazo ambayo hayajafanyiwa utafiti. Mawazo ya kusikia tu(hear say). Mawazo yasiyokuwa na namba.
Haya sasa twende kwa mifano:
1. Rais wa kwanza wa Tanzania alikuwa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Huyu anatokea katika familia ya kichifu. Familia za kichifu ndio zilikuwa familia tajiri wakati wa ukoloni na hata kabla. Cabinet yake ilikuwa na watu waliotokea katika familia zilizofanikiwa kusoma wakati wa ukoloni kupitia kanisa katoliki au uchifu wa familia na koo zao.
Kulikuwa na maskini hapo ukiangalia hali ya watu wakati ule?
2. Rais wa pili alikuwa Ally Hassan Mwinyi. Aliweza kusoma hadi nje ya nchi hata kabla ya ukoloni. Wakati anaingia kuwa Rais alishakuwepo kwenye cabinet, ubalozi na Rais wa Zanzibar. Alikuwa na umaskini gani?
3. Rais wa 3 alikuwa Benjamen William Mkapa. Mseminary. Wakati anaingia kuwa Rais alishakuwa mtumishi wa ngazi ya juu ndani ya serikali, Balozi na Waziri. Alikuwa na umaskini gani?
4. Rais wa 4 alikuwa Jakaya Mrisho Kikwete, huyu anatokea familia ya Kichifu na Baba yake alishakuwa DC na RC, yeye JK alishakuwa ngazi ya Kanali jeshini, aliahakuwa katika ngazi mbali mbali ndani ya CCM, alikuwa Waziri tangu muda mrefu. Alikuwa maskini? Maskini ni nani kwako?
 
Back
Top Bottom