Kwanini riba za mabenki ni kubwa sana?

Attachments

  • Screenshot_20240903-183606~2.png
    Screenshot_20240903-183606~2.png
    139.4 KB · Views: 4
Kwa mfanyakazi mpya ndio risk ni kubwa kwa sababu bado mafao yake hayawezi kulipa mkopo just in case akafa ama akafutwa kazi mapema ila kwa mtu ana miaka 15 na kuendelea kazini hata akikopa akafa ama akaacha kazi bado mafao yake yanaweza kulipa mkopo lakini pia mkopo huo mfanyakazi ameulipia bima.

Banks walipaswa wawe wana profile wafanyakazi independently kuliko kuwaweka kundi moja, alieajiriwa leo na alieajiriwa 20years ago kwani risk profile zao ziko tofauti kama inavyofanyika kwenye business ama individual borrowers
Watanzania kwenye mambo ya mikopo uaminifu ni mdogo, mtu akihama kazi tu kapata sehemu nzuri hatoi taarifa na marejesho haleti, na anaweza fanya mpango akakopa tena sehemu nyingine. Au akaamua tu halipi. Acha hao wanaopunguzwa na kufukuzwa kazi
 
Kwanini Riba ya mikopo ya mabenki ni kubwa kuliko anachopata mtumishi mfano unaeza kopa mil 6, take home mil 5.31 alafu marejesho inakua mil 9 hii imekaaje wakuu? Tuwasaidie Gen Zee
Serikali inakopa kwenye mabenk ya ndani kwa riba nzuri, ya asilimia 13 mpaka 20,na mabenk yanaona serikali ni mteja mzuri,mwenye uhakika, hawezi kufirisika, kwa hiyo pesa wanapereka huko kwenye bond, nk, sasa ukija wewe unataka mkopo, kwanza, ya minikin, pili mtu binafsi na kampuni ndogo, ni risk Sana, unapigwa asilimia 23 kwenda juu, hapo wananchi hawawezi kukopesheka, biashara hazikuhi, uchumi unadoda, lakini serikali ikiacha kukopa ndani, mabenk yatakosa pa kupeleka pesa zao, watazileta kwa wananchi kwa riba ndogo,
 
Afadhali ya hiyo ya benk ndugu, huku mtaani kausha damu wala hawafuati hiyo %. Yaani ukikopa 100,000 asubuhi ikifika jioni jamaa anataka 150,000.

Hutaki anaomdoka na TV ama fridge. Ukienda kwa m/kiti wa mtaa kushtaki anakwambia mlielewana malizaneni kwa amani.
 
Serikali inakopa kwenye mabenk ya ndani kwa riba nzuri, ya asilimia 13 mpaka 20,na mabenk yanaona serikali ni mteja mzuri,mwenye uhakika, hawezi kufirisika, kwa hiyo pesa wanapereka huko kwenye bond, nk, sasa ukija wewe unataka mkopo, kwanza, ya minikin, pili mtu binafsi na kampuni ndogo, ni risk Sana, unapigwa asilimia 23 kwenda juu, hapo wananchi hawawezi kukopesheka, biashara hazikuhi, uchumi unadoda, lakini serikali ikiacha kukopa ndani, mabenk yatakosa pa kupeleka pesa zao, watazileta kwa wananchi kwa riba ndogo,
Acha uongo, crdb watumishi wanakopa kwa riba ya hadi 13%, wafanyabiashara ni 17-21%
 
Ukiingia Exim mkopo unaenda mpaka miezi 120.Usitegemee aliyechukua miezi 48 riba yake ilingane na wewe.
Afu hua tunajaza tuu hatusomi Terms and Conditions
 
Back
Top Bottom