Kwanini Paul Pogba anasifiwa, mbona hana lolote?

Pogba ni bonge la mchezaji ila kocha anakosea namna ya kuwachezesha maana wachezaji watatu wanaocheza no 10 wote anawaanzisha kwa pamoja hivyo kila mmoja anacheza kwa kushindwa kucheza kwa uhuru! Pogba na Payet wanacheza no moja huku Matuid akikosa uhuru wa midfield

Mtu mmoja aliyewekwa nafasi yake ni Kante na ndo maana anaonekana sana lazima kocha aamue kati ya Payet na Pogba nani aanze
Ilo ni kweli kabisa kama asipofanya maamuzi mechi zijazo hawatofika mbali
 
Nadhani wewe na Paul Pogba ni watani. Ngoja tuwachie utani wenu. Ila kama siyo mtani wako basi utakuwa ulienda kuangalia mechi ukiwa negative tayari . Kwa hiyo ulihisi kila akishika mpira=goli. Pogba alicheza kwa kiwango cha kutosha kabisa! Kutolewa siyo hoja! Wengine nao ni wachezaji. Hata hivyo France ilicheza vizuri tokea mwanzo. Nadhani huijui Romania katika ulimwengu wa soka.
 
Nimeangalia game ya France na Romania mpaka dk hii ya 88 na nusu ambapo France inaongoza 2-1 , kiukweli huyu mchezaji anasifiwa bure tu .

Baada ya yeye kutolewa ndio timu ikapata uhai , kwa ufupi ni kwamba alikuwa mzigo kwa timu .

Sasa zile sifa zake zote za kule juventus ilikuwa za uongo ?

Hapana sikubaliani nawe. Pogba anajua angalia vizuri.
 
Ni mapema mno kusema chochote kuhusu Pogba tumuangalie na mechi ijayo na mfumo atakaotumia kocha.
 
Nadhani wewe na Paul Pogba ni watani. Ngoja tuwachie utani wenu. Ila kama siyo mtani wako basi utakuwa ulienda kuangalia mechi ukiwa negative tayari . Kwa hiyo ulihisi kila akishika mpira=goli. Pogba alicheza kwa kiwango cha kutosha kabisa! Kutolewa siyo hoja! Wengine nao ni wachezaji. Hata hivyo France ilicheza vizuri tokea mwanzo. Nadhani huijui Romania katika ulimwengu wa soka.
Haya kaka tuendelee kufuatilia .
 
Yaani kwa mechi moja umepata majibu yako..
Sifa anazomiminiwa huyu mchezaji unaweza kudhani ni wa kiwango cha messi , sasa namna nilivyomfuatilia ( si jana tu ) nimegundua kwamba ni mchezaji wa kawaida sana na ukiangalia kwa makini huwa anapenda sana kucheza na jukwaa ( tabia mbaya ya kiswahili , kama wachezaji wa Faru dume ya manzese ) , kiukweli si kama anavyoongelewa .

Hana tofauti sana na Mwaikimba ; japo yeye anacheza kati .
 
Nashukuru wadau wengi wameamua kumpuuza pogba na kumshangilia Shujaa mpya Payet .
 
Kante ndo alikuwa hatari kwa leo

Ila pogba bado mzuri hata leo si kwamba alicheza vibaya

Hakufikia tuu kiwango cha sku zote

Pia samatta ifike sehem ajifunze kupiga penalt sasa

Samatta kinachomnyemelea ni kulewa sifa, namhurumia sana...ameshaanza kujiona kuwa amefika...
 
Back
Top Bottom