Jambazi
JF-Expert Member
- Jan 18, 2014
- 16,644
- 18,707
Ukipanda za jeshi au zile za kuchungia tembe mbugani si ndiyo utazimiaUmenikumbusha mbali na hiyo picha.Si nilipanda siku moja Dar -Moro (ndege) vile vya watu kumi! Mnaingia kama mnaingia kwenye toyota mark II nikapewa karibu na siti ya dereva (rubani)! Nilishangaa kweli siku hiyo ila lakini, Wee ! Eheee! Yaani kilikuwa kizungumkuti na ile ndege, ilipokuwa ikipita, pishana na hata kawingu kadogo mnarushwa utadhani dalala inapita barabara ya Kutoka dalaja la Nyerere kuelekea Kigamboni ndani! Yaani kama unaroho ndogo ndege zile usipande. Yaani tena pale mbele unajiona kama upo kwenye 'Ungo' uliorushwa mawinguni. Ni wakati huo nilibahatika kuona kwa karibu namna ndege ndogo iendeshwavyo.
====
Sisi bwana hatukuzimiwa taa, tena tulitua pale Kihonda mida ya saa 12:30 jioni.