Kwanini nchi zilizotawaliwa na Wazungu ni masikini sana?

The suspicion is that as far as the 3rd world is concerned you'll always have a conflict between development and human rights... where u have development you may not have human rights and vice versa

Wapi hiyo Kanuni yako haikutumika? Nijuavyo mimi hakuna, wkt USA inajengwa kulikuwa hakuna human rights, hata Uingereza na nchi za Ulaya wamaenza mambo ya human rights karne ya 20 baada ya kuwa wameshaendelea, hivyo hakuna nchi ambayo ilikuwa na inafwata human rights tangu mwanzo na isitoshe inategemea kwako human rights maana yake nini kwa maana imekuwa ikibadilika kulingana na wakati!
 
Uganda ilikuwa nchi huru, wamissionary wa ki-Belgiji na ki-Faransa walieneza u-Katoliki na pia u-Islam uliingia kutoka South Sudan. Wafuasi wa dini hizi mbili yalianza kupigana vita kila moja likitaka kwa na wafuasi wengi Zaidi, na wale waliamua kubaki na dini za asili. Wakati huo Mwingereza alichukuwa Kenya kama koloni lake na alishuhudia vita vya wa-Ganda mara nyingi. Aliamua kutumia njia za ki-diplomasia kumaliza mgogoro na waliwekwa makabila yote chini, Kabaka aliwekwa mtawala na makubaliano yalikuwa Mwingereza atakauwa protectorate. Lakini alijichukulia madaraka ya ukoloni kinyume cha makubaliano.
 
Kwa nini unasema hivyo?
Sababu kubwa waafrica wengi hawatumii akili zao ipasavyo, ni wanafiki, watumwa wa akili, wanapenda kujishushia heshima zao hasa kwa kujipendekeza kwa wenye mamlaka,hawajitumi, sio wadadisi na mengine mengi tu ingawa mengine yanakuhusu na wewe pia.
 
Vp kuhusu wengine niliowataja ambao siyo Waafrika? Kwa nini na bado masikini?
 
Leo ndio nasikia INDIA kuwa ni Masikini... Maajabu haya...

Maendeleo yameletwa na Viwanda na sio Tawala mfano Tanzania ilishakuwa na muelekeo mzur wa Utajili ila uzembe na wizi na kujuana kwingi tukashindwa kushurutishana so hapo Muingereza hausiki kwa lolote.

Nchi Nyingi ni Tajiri labda uzungumzie kipato cha mtu na mtu maana hata Uningereza Masikini wapo kibao tu. United Kingdom haikuzivamia nchi tatu tu Duniani.

Mleta mada una kaupungufu kiasi cha akili za kuwaza maana huendi deep. Israel yenyewe ilikuwa chini ya Uingereza Akili za kuwa na viwanda na kujituma zimeipeleka juu katika nyanja nyingi hadi Muingereza nyanja nyingi kapitwa na Israel
 
Kwa sasa India ina uchumi mzuri kuzipita baadhi ya nchi za ulaya magharibi. Na sasa imeweza kurusha satellite anga za mbali.
 
India ni masikini kama unabisha hilo basi jielimishe upya, India ina masikini wengi klk Afrika!
 
Kwa sasa India ina uchumi mzuri kuzipita baadhi ya nchi za ulaya magharibi. Na sasa imeweza kurusha satellite anga za mbali.

Siyo kweli! India inapata bado foreign aid ktk nchi tajiri na India ina masikini wengi klk Afrika!
 
Ukiondoa nchi ambazo Wazungu walitawala na wakaamua kubakia kama Kanada, USA, AK, Australia n.k. ukiondoa Singapore hakuna nchi nyingine yoyote ile iliyotawaliwa na Mzungu ambayo imeendelea, sasa ni kwa nini?

Afrika yote Masikini wa kutupwa, India, Pakistani, Sri Lanka, Bangladesh, Nepal, Haiti, Jamaika, Iraki, Syria, Lebanon, Papua New Guinea, Nauru, Ufilipino n.k. wote hawa ni masikini na wametawaliwa na Wazungu wkt nchi ambazo hazikutawaliwa na Mzungu leo hii zina first world economy kama Korea Kusini, Taiwani, hata Uchina inakaribia huko, sasa sababu ni ipi?
kwa tanzania umasikini umesababishwa na ccm sijii hizo nchi zingine
 
Ukiondoa nchi ambazo Wazungu walitawala na wakaamua kubakia kama Kanada, USA, AK, Australia n.k. ukiondoa Singapore hakuna nchi nyingine yoyote ile iliyotawaliwa na Mzungu ambayo imeendelea, sasa ni kwa nini?

Afrika yote Masikini wa kutupwa, India, Pakistani, Sri Lanka, Bangladesh, Nepal, Haiti, Jamaika, Iraki, Syria, Lebanon, Papua New Guinea, Nauru, Ufilipino n.k. wote hawa ni masikini na wametawaliwa na Wazungu wkt nchi ambazo hazikutawaliwa na Mzungu leo hii zina first world economy kama Korea Kusini, Taiwani, hata Uchina inakaribia huko, sasa sababu ni ipi?
Kwasababu waliharibu mfumo mzima wa kufikiri
 
ujue kwamba wenyewe wakikunyonya bas wananyonya sawa sawa mpaka ukauke na still hawakuachi until now bado wana colonize most contries kupitia neo colonialism
 
Utaendeleaje kwa teknolojia tegemezi na uchumi wa kilimo cha mazao ya chakula kama mahindi, maharage, mihogo na mazao ya biashara kwa kiasi kifogo sana na vyote hivyo vinategemea mvua na isiponyesha kilio chai mbwa mwizi mdomo juu?! Hata hivyo walitufumbua macho walivyotutawala. Tatizo letu ni uongozi mbovu, teknolojia duni na elimu.
 
India ni masikini kama unabisha hilo basi jielimishe upya, India ina masikini wengi klk Afrika!
Usikimbie kivuli chako Umesema Nchi Masikini 1st Kuhusu India Na Tanzania India Imeipita Tanzania kwa Kila Kitu Iwe Utajili,Umasikini,Ukubwa wa Nchi,Idadi ya Watu ambapo kama sie Watanzania tukigeuzwa kitoweo na Wahindi waache kula chakula kingine basi sisi Watanzania tutaliwa kwa siku moja tu kwa idadi wa watu walio india 1.3 billion sensa ya kitambo.
Kiuchumi India ipo juu zaidi ya England, Kiuwezo wa Jeshi na Ukubwa wake India ina Silaha Nyingi zaidi huwezi fananisha India ina Mabilionea wengi zaidi ya Waingereza.

Wewe Mama siku nyingine unapota Mada zako zitengenishe kwenye nyanja na sio kusema kwa ujumla. Kama Ulimaanisha hali ya umasikini baina ya mtu na mtu ungeweka wazi na sio kusema Nchi Masikini.
 
Korea kusini na taiwan ni first world economy ila india ni maskini? India ni kati ya nchi zenye uchumi mkubwa duniani. Kuwa na watu maskini sio tatizo kumbuka india ina raia zaidi ya billion 1 lazima maskini wawepo ila huwezi kusema nchi yote ni maskini. Hata marekani kuna watu maskini. Pia nchi kama Pakistan, Syria, iraq huwezi kusema ni maskini hizi nchi zina uchumi wa kati na zinawezi kujitegemea.
 
Mbona kuna nchi kama Ethiopia na Liberia hazikutawaliwa lakini hali zao za kiuchumi siyo nzuri?

Unaizungumziaje South Africa ambayo imetawaliwa kwa miaka mingi lakini uchumi wake unakua kwa kasi?
Muondoe kaburu leo hii uone S.A itakavyoanguka kiuchumi. Au unadhani uchumi wa S.A umeshikiliwa na mtu mweusi??
 
Hata hivyo, bado tunasaidiwa na uwepo wa Indians and Arabs. Hawa jamaa wasingekuwepo nadhani tungekufwa kabisa. Hata huo uchumi mdogo tulionao, asilimia kubwa upo chini ya mhindi na mwarabu.
 
Back
Top Bottom