Kwanini nchi tulizozisaidia kwa hali na mali zetu huwa wanatudharau watanzania?

Tumewasaidia wakapata uhuru wakaanza kujenga nchi zao sisi tunapiga porojo tu,wamejenga uchumi wao vizuri kama South Africa na Kenya sisi tunaimba ngonjera tu,sasa kwanini wasituone zaidi ya mabwege? Ata mimi ningekuwa raia wa hizo nchi ningekuwa nawadharau watanzania,marasilimali kibao bado mnalialia tu.Hii ni sawa wewe uwe ndo mwendesha 'discussion' na kusaidia maswali wenzako halafu mtihani wa Taifa ufekafeli kisha washikaji wakipata maisha unaanza kujigamba kwamba uliwasaidia lakini hawakujali,kwanini wewe hukufaulu?.
 
YEHODAYA,

..waliosaidiwa ni wazee na wengi wameshatangulia mbele za haki.

..hao ndiyo walikuwa wanawaenzi wa-Tz kwa msaada waliotoa.

..sasa hivi kuna kizazi kipya na kina changamoto mpya za kiuchumi na kisiasa.

..jambo lingine ni aina ya wa-Tz wanaokwenda ktk nchi hizo za kusini mwa Afrika.

..ukienda nchi yoyote ugenini ukiwa maskini na usiye na ujuzi wowote lazima utanyanyasika na kudhauraulika.

..heshima yako ktk dunia ya leo haitatokana na nchi ulikotoka, bali itatokana na ujuzi ulionao, and what you can offer(ujuzi, mali, au fedha).
 
Tulia dawa iingie, mbona ccm wananchi tumewapa nchi halafu mnatudharau au nyani haoni kundule!?
 
Nimefuatilia nchi nyingi tulizopigania uhuru huwa wanatudharau watanzania.

Mfano nikianza na Afrika KUSINI wao walikuja hapa kwa maelfu kule kwao kulipokuwa na hali ngumu tukawapokea wakala chakula chetu,wakatumia ardhi zetu wakiwa hawana passport wala chochote hadui wakarudi kwao salama.Hali nchini kwao ilipokuwa imkaa vizuri watanzania kuingia na kuishi ni shida.

Msumbiji nako vivyo.

Ukienda Rwanda na Burundi na Uganda hutuona watanzania kama wajinga fulani AMBAO UWEZO WETU NA AKILI ZETU NDOGO wao zao ndio kubwa wakati tumewahofadhi na kuwasaidia kwa mengi.Wakenya ndio kabisa hutuona kama mabwege fulani hivi wakati kulipoibuka mauaji kwenye uchaguzi uliopita Kikwete mtanzania ndio aliwasaidia kumaliza tofauti na nchi kuwa na amani.

Najiuliza hivi tuliwakosea nini hawa wenzetu.Kama wanatuonea kwa wema wetu Mungu awalaani wawe ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania.

Mkuu mbona unakwenda mbali hivyo.
Hapa Tanzania wengi wetu Tumetoka mikoani Na kuja Dareslam.Tumekaribishwa Na Waswahili wa hapa.Baada ya kupata Elimu Au kazi nzuri Na vijisenti.Leo tunathubutu kuwaita wavivu,wavamadera Na kejeli za kila aina.
Sijawahi kusikia "Waswahili " wakilalamika tumewakosea nini? Nyie Watu wamikoani.
Ndio maana wahenga walisema "fanya Wema nenda zako"
Sisi WaTanzania tulitimiza wajibu wetu wa kuwasaidia kupata uhuru waki tushukuru sawa wasipo sawa Vilevile.
 
Mimi mwenyewe nilizaliwa Tanzania ila nawadharau watanzania........Why not kama hawatumii akili.......watanzania bwana vilaaaaaaaaaaaza
 
Xenophobia
  1. intense or irrational dislike or fear of people from other countries.
 
Tatizo kubwa la Watanzania ni ushamba ushamba .............. hatuko exposed.

Kama ulikuwa unafuatilia Big Brother Africa nafikiri utakuwa umeona!!!
 
Hakuna nchi inayozarau nchi nyengine,Nchi hujizarau wenyewe kwanza ndipo nchi nyengine zikakuzarau,mfano hapa Tanzania uchumi wetu haukuwi ijapokuwa nchi ina nyenzo na rasilimali nyingi,wananchi hawana uhuru wa maamuzi yao wenyewe,umasikini unazidi kila kukicha,wananchi wanakimbia wanakwenda nchi jirani kutafuta maisha bora,,,

Juzi tu nimemsikia raisi akisema wanaokamatwa na unga nchi za nje wanyongwae tu,Raisi mwenye hekima na kupenda raia wake angelisema hao waliokamatwa na unga wahukumiwe kihaki,kisheria...

Kosa la kukamatwa na unga hasa airport lina mambo mengi inawezekana mtuhumiwa kapewa begi airport asaidie bila kujua kuna nini katika begi,kwani hayo mambo ya kumsaidia mwenzako begi yanatokea kila siku....,

Kama raisi amewadharau hawathamini raia wake nani atawathamini...
 
Hiyo ni tabia ya binadamu wengi duniani,tenda wema nenda zako usingoje shukrani.
 
Kama baba yako hana msimamo na anaonyesha chuki za wazi wazi hadharani unategemea jirani atakuheshimu?
Viongozi wamekuwa wa kwanza kututukana na kuonyesha chuki zao kwetu yaani tunanyanyasika na kudharaulika nje na ndani
 
Kwanza watu tuliowasaidia katika nchi hizi aidha ni wazee au walishakufa. Wanaowatendea haya ni watoto hawana habari na msaada wenu kwa nchi zao, kwa kuwa pia somo la historia katika nchi zao linafundisha kwamba nchi zao zilikombolewa na baba zao bila kutaja kwa undani msaada wa nchi kama Tanzania.
.

Hapa naanza kuelewa
 
Nimefuatilia nchi nyingi tulizopigania uhuru huwa wanatudharau watanzania.

Mfano nikianza na Afrika KUSINI wao walikuja hapa kwa maelfu kule kwao kulipokuwa na hali ngumu tukawapokea wakala chakula chetu,wakatumia ardhi zetu wakiwa hawana passport wala chochote hadi wakarudi kwao salama.Hali nchini kwao ilipokuwa imekaa vizuri watanzania kuingia na kuishi ni shida.

Msumbiji nako vivyo.

Ukienda Rwanda na Burundi na Uganda hutuona watanzania kama wajinga fulani AMBAO UWEZO WETU NA AKILI ZETU NDOGO wao zao ndio kubwa wakati tumewahofadhi na kuwasaidia kwa mengi.Wakenya ndio kabisa hutuona kama mabwege fulani hivi wakati kulipoibuka mauaji kwenye uchaguzi uliopita Kikwete mtanzania ndio aliwasaidia kumaliza tofauti na nchi kuwa na amani.

Najiuliza hivi tuliwakosea nini hawa wenzetu.Kama wanatuonea kwa wema wetu Mungu awalaani wawe ndani ya Tanzania au nje ya Tanzania.
Wanatuona maboya sana kuongozwa na vilaza huku pakiwepo na wapumbavu wengi kama wewe wanaounga mkono huo ukilaZa
 
Back
Top Bottom