Kwanini nchi husimama Raisi Magufuli ategemewapo?

Tunafurahia kuskia maneno yake ya busara na pia nani atatumbuliwa leo? Na pia ataibuka na ubadhirifu au ukwepaji kodi eneo gani miaka nyuma. Ndyo maana huwa tuna hamu sana kumsikia.
 
Imerejea wapi Magufuli kavaa viatu vikubwa kumshinda.
Naona anatumia mbinu za Lowassa kujijenga kisiasa. Kweli nimeamini maneno ya Lowassa kuwa Mzee Pombe hana vission amebaki kucopy na kupaste.
Tumesha mstukia na tume huru ya uchaguzi ikipatika 2020 tunampiga chini.

Kama anatumia mbinu ya Lowassa iko wapi Richmond yake? Na mvua kutoka Malaysia kaitamka lini? Na mafuriko ya kugushi kuwapa watu mapesa na kuwaambia waje waseme wewe ndiye kiongozi unayefaa kafanya lini? Na kuwapa watu pesa wazimie eti watu ni wengi mno kafanya lini???
 
Mwogope Mungu. Tafuta kiki kwa njia nyingine.
 
Watu kuwa na shauku ya kukusikiliza, kuna uwezekano wa watu wanajua kuwa kila wakati utakuja na jipya. Na jipya lenyewe linaweza kuwa na mantiki au la kipuuzi. Kama lina mantiki, watataka kujua jema lipi linakuja. Kama ni la hovyo, watu watataka kujua utaropoka nini!

Wakati Amin akiwa Rais wa Uganda, ikitolewa taarifa kuwa atahutubia, wahindi walikuwa wanafunga mpaka maduka ili wasikie safari hii atasema nini. Rais wa Maisha Dr. Ngwazi Kamuzu Banda wa Muyayaya, ndege yake ilipokuwa kwenye anga la Malawi, hakuna ndege iliyokuwa ikiruhusiwa kiruka au kutua mpaka ndege ya Rais maisha itue. Wananchi wengi walikuwa hawaendi hata kazini ili wasikie atakapotua ataongea nini.

Watu huwa wana shauku kubwa ya kumsikia kiongozi wao mkuu pale ambapo hawajui kesho au keshokutwa kutatokea nini. Ni dalili ya kutukuwepo mfumo wa kiuongozi unaoweza kuwapa watu uhakika wa maisha yao.

Mkuu umemaliza kila kitu.......eid mubarak
 
Ni kwa sababu wati wanataka kujua katoa kipi kipya maana haachi kutoa yasiyodhaniwa
 
Mimi kitaani kwetu huwa hapatoshi, bar zote na mtoto huwa hatumwi dukani siku wakisia Raisi Magufuli anatemewa kuongea!

Kitaa gani unaishi nitambue uzushi wako . Pengine mimi ni jirani yako nione jinsi unavyo ongopea umma
 
Kama anatumia mbinu ya Lowassa iko wapi Richmond yake? Na mvua kutoka Malaysia kaitamka lini? Na mafuriko ya kugushi kuwapa watu mapesa na kuwaambia waje waseme wewe ndiye kiongozi unayefaa kafanya lini? Na kuwapa watu pesa wazimie eti watu ni wengi mno kafanya lini???

Hahaaaaa ! Ukweli unauma siku zote .
Wala sibishani na wewe kwa kuwa unaonekana hufuatilii matukio ya kisiasa .
 
Tuseme lbada uko sawa, lakini kwa nini nchi husimama pindi ategemewapo kuhutubia mahali? Nimeshashudia watu wakiwahi nyumbani na wengine bar kila wakisikia Raisi Magufuli anategemewa kuongea hata kama amealikwa tu kwenye Mkutano wa Bodi fulani, sasa ni kwa nini?
Umetembea nchi nzima ukaona unayoandika au unasukumwa na hisia zako? Acha kujibaraguza kama muuza mchicha supermarket we jamaa!
 
*ategemewapo?

Hivi ni kwa nini kama ikijulikana tu Raisi Magufuli atakwenda mahali na kuongea kitu basi nchi nzima huwa karibia wiki nzima hujawa na shauku kubwa ya kutaka kusikia Raisi atasema nini, hii sijawahi ishuhudia tena katika maisha yangu hapa Tanzania, hata wale wasiompenda raisi Magufuli lakini siku wakisikia kaalikwa mahali na atahutubia basi wote hujawa na shauku katika kusikia atasema nini, hivi ni kwa nini?
mkuu inayo tafsiri pana na mchanganyiko wa athari nzuri na mbaya, shauku lazimz iwepo kwani anayo mamlaka ya kusimamisha taratibu zilizo zoeleka/andikwa na kuelekeza vinginevyo. maelekezo hayo yana athari katika maisha ya kila siku. mfano tamko la kuzuia sukari kutoka nje na kilicho tokea baada ya tamko hilo, kufuta maadhimisho ya shere zilizo zoeleka na kiasi cha pesa iliyo okolewa na kuelekezwa kwenye more burning issues za kimaendeleo, kutumbua watendaji wa selekali live live kwenye mikutano kila mtu ana shauku ya kujua nani atatumbuliwa live leo,..................................mf. ni mingi.
na shauku ya kusikilizwa haipo tu pale napo hutubia, bali kila siku kwenye taarifa za habari watu wana shauku ya kujua mwongozo wa siku itakayo fuata!!!!!!!...........
 
Wanakusikiliza endapo wanakwamini. Ni wapi watu wakaanza kimsikiliza mwokota makopo?
 
Tuseme lbada uko sawa, lakini kwa nini nchi husimama pindi ategemewapo kuhutubia mahali? Nimeshashudia watu wakiwahi nyumbani na wengine bar kila wakisikia Raisi Magufuli anategemewa kuongea hata kama amealikwa tu kwenye Mkutano wa Bodi fulani, sasa ni kwa nini?
Sijawahi kuona nchi imesimama. Wapo watu ambao wewe ndio umewaona wanaosubiri ujio wa mtukufu kama mlinzi angojeavyo asubuhi...lakini nakuhakikishia wapo wengi tu ambao hata jana hawakujua kama anakwenda 'kula Eid' na kugawa fedha, nikimaanisha kwamba walikuwa busy na mambo yao.
 
Back
Top Bottom