Kwanini mbuga ya Serengeti haiunufaishi mkoa wa Mara badala yake inainufaisha Arusha

Mkoa wa Mara uliharibiwa na Mwl Nyerere mwenyewe. Enzi zake hakutaka kufanya jambo lolote kwenye mkoa huo, kwa kigezo cha kuonekana anapendelea kwao. Yaani hata barabara za lami tu hazikuwepo.

Hadi leo mkoa ule ni wa mwisho kwa kila kitu. Jambo litaanzia sehemu zote na Mara ndio itakuwa ya mwisho.
 
Mkoa wa mara uliharibiwa na Mwl Nyerere mwenyewe. Enzi zake hakutaka kufanya jambo lolote kwenye mkoa huo, kwa kigezo cha kuonekana anapendelea kwao. Yaani hata barabara za lami tu hazikuwepo.

Hadi leo mkoa ule ni wa mwisho kwa kila kitu. Jambo litaanzia sehem zote na mara ndio itakuwa ya mwisho
Je viongozi wote waliofatia baada ya mwl Nyerere hawajaona umuhimu wa kuunganisha miundombinu iliyokuwa bora na rafiki zaidi kwa utalii ndani ya mkoa wa Mara?
 
Mtu akiwa Arusha ni rahisi kupata access ya Tarangire, Ngorongoro, Serengeti kuliko akiwa Musoma, Bunda, Mwanza

Sent from my M2006C3LG using JamiiForums mobile app
Katika hizo mbuga ulizotaja inayotembelewa na watalii wengi ni Serengeti iliyopo mkoa wa Mara na ukiangalia distance kutoka Arusha mpaka Serengeti ni kubwa kuliko kutoka Musoma mjini to Serengeti.
 
Mkoa wa mara uliharibiwa na Mwl Nyerere mwenyewe. Enzi zake hakutaka kufanya jambo lolote kwenye mkoa huo, kwa kigezo cha kuonekana anapendelea kwao. Yaani hata barabara za lami tu hazikuwepo.

Hadi leo mkoa ule ni wa mwisho kwa kila kitu. Jambo litaanzia sehem zote na mara ndio itakuwa ya mwisho
Hapana Lindi ndio wa mwisho tena mwisho kushoto kabisa wakifuatiwa na Mtwara kule puuuh!
 
kwasababu kanda ya ziwa hakuna international airport, kama ilivyo KIA kwa kilimanjaro ndio maana Arusha inanufaika

pambaneni mwanza kuwe na international airport ndio hiyo Mara itafaidika; tofauti na hapo ni ndoto
JNIA tu haiko busy kwa kifupi the whole of Tanzania haipokei flights nyingi bado ujenge liuwanja likubwa lingine la nini brother?
 
Bora huko walau wanalima mahindi na korosho. Ule mkoa wa mara hata kilimo ni shida tu, labda tarime kiasi
Mzee mkoa wa Mara sehemu yake kubwa ni water bodies na nyingine ndo hyo Serengeti. Sasa unategemea sehemu kama za Musoma vijijin watapata wapi ardhi kubwa kihivyo ya kilimo wakati kila sehemu ni maji tu.
 
Wasaalam ! kwa fikra pana sana na hofu ya Mungu iliotikuka ningepend kulileta suala hili mbele yenu tulijadili kwa mapana zaidi bila ya chuki za ukanda wala ukabila ..
Mna madini ya dhahabu. Tangu yaanze kuchimbwa yamewasaidia nini?

Pia Serengeti National Park haipo entirely mkoa wa Mara peke yake. Part ipo Simiyu na Arusha pia so hiyo mikoa nayo ina madai sawa na Mara.
 
Mna madini ya dhahabu. Tangu yaanze kuchimbwa yamewasaidia nini?

Pia Serengeti National Park haipo entirely mkoa wa Mara peke yake. Part ipo Simiyu na Arusha pia so hiyo miko nayo ina madai sawa na Mara.
Simiyu ni pori la akiba Kijereshi na Arusha hakuna sehemu ndani ya mkoa wa Arusha hifadhi ya Serengeti inafanya coverage na hifadhi ya Serengeti kwa mapana zaidi ipo ndani ya mkoa wa Mara. I stand to be corrected.
 
mzee mkoa wa mara sehemu yake kubwa ni water bodies na nyingine ndo hyo serengeti .sasa unategemea sehemu kama za musoma vijijin watapata wapi ardhi kubwa kiivo ya kilimo wakati kila sehemu ni maji tu
Hizo water bodies ndizo fursa za umwagiliaji. Haya niambie huko Musoma vijijini kwa hao wenye ardhi ndogo, nani anaweza hata kununua generator ya kumwagilia mahindi hata robo ekari tu akavuna junia zake 10 kwa msimu.

Hao wenye ardhi ndogo hawawezi hata kutumia fursa ya ziwa kumwagilia mazao, yet unalaumu eti sehemu kubwa ni ziwa?

Ambao wako sehemu za jangwa watasemaje kama sisi tunalalamikia maji, tena maji baridi yasiyo na chumvi.

Huo mkoa nakwambia Nyerere ndo aliumaliza kabisa kwa sera za ujamaa
 
Back
Top Bottom