6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,701
- 5,801
Habari wana jamii forum?
Kuanzia miaka ya elfu mbili kushuka chini, eneo la Mbezi beach lilikuwa ni kati ya maeneo machache ya jiji la Dar es salaam ambayo yalikuwa na umaarufu mkubwa kama vile ilivyokuwa Masaki, Osterbay, Sinza nk.
Hii ilipelekea watu wengi hasa wa mikoani wakisikia neno Mbezi, basi akili au mawazo yao yanaenda moja kwa moja kwenye Mbezi beach. Japo Mbezi ya Kimara ilikuwepo, lakini watu hawakuwa wakiifahamu kivile kama inavyofahamika leo.
Sasa hali imekuwa ni tofauti, Mbezi ya Kimara imetokea kuwa na umaarufu mkubwa hadi kupelekea Mbezi beach kusahaulika. Leo hii mfano ukiwa mikoani ukazungumzia neno Mbezi bila kuweka hilo neno beach mbele basi kila mtu akili na mawazo yake yataenda kwa Mbezi ya Kimara kama vile mbezi luis, mbezi mwisho, mbezi magufuli nk.
Je, ni nini chanzo cha umaarufu wa mbezi kuibuka ghafla tofauti na hapo zamani?
Nawasilisha