Kwanini Manji anaandamwa na huu utawala?

Manji amepatwa misukosuko mingi tangia hawa vibosile wakamate ulaji kwa sababu kubwa moja tu wakati Wa mchakato Wa uraisi ndani ya CCM alimpigia debe la nguvu Membe.

Yale maburunkutu yalidakwa baadaye yakatakatishwa na polisi kuwa hayakuwa na dhamira ya kuhonga wajumbe wa mkutano mkuu wa CCM bali yalikuwa ya kuendesha shughuli za mfanyabiashara huyo.

Membe alipodondoka na Manji khali yake kisiasa ikaingia matatani.

Iwe Koko Beach, iwe ni Yanga na sasa madawa ya kulevya Manji anasomeshwa namba na chama chake.

Visasi ndiyo mkakati uliopo lakini pia kumdhoofisha kiuchumi na kisiasa asiweze kufurukuta na kuwa na ushawishi wowote chaguzi zijazo.

Unapoona kibosile anakerwa gari la Manji kuoshwa Central Police na kama yeye angelikuwa ni IGP angeona cha mtema kuni ujue huo ni uhasama mtupu na visasi.

Kwani kuosha gari polisi ni kuvunja sheria ipi hadi kibosile autamani u-IGP?

Manji ikumbukwe alianza kutajirika wakati wa Mwinyi, Mkapa na JK wakamneemesha vilivyo kwa madili kebekebe sasa ni wakati wake Wa kusoma namba.

Akina Professa Kapuya waliomnyoshea njia wako kwenye mawe na ndiyo maana anasoma namba ila hajaielewa......ukiona hata maamuzi ya mahakama vibosile hawa wanayapuuza ujue hii ni vita ya "survival of the fittest."
msomi wa kitanzania '' kamaliza kupresent
eee mungu baba ' watu wako wanaangamia kwa kukosa maarifa
 
Na ndio lengo hilo ndo maana mengi kawa mpole na mdogo ka piriton. Wakati USA waki create mabilionea wengi huku wanafilisiwa badala ya kuwezeshwa ili kutoa ajira kupitia hata viwanda
Kinacho nishangaza katika awamu hii ndio hiko, atajiri wanaoenakana kama watenda dhambi.
Wakati kama ukikaa nao vzuri, uka punguza kodi uka punguza regulations ngumu hao ndio huwa wana saidi uchumi kukua, na ma midleclass kuongezeka
 
Walishakosea tangu mwanzo hawako smart enough na kutaka Ku deal na watu aina hyo sasa had jamii ishtukie.
Mwanzo walianza hivo kwa kigezo cha kunyoosha nchi, sijui uzalendo hadi hawakufata sheria na kuingilia mamlaka nyingine, baada ya mwanzo kuchekewa na RAIA.
Hata kujenga nchi ya viwanda wameweka kando baada ya kutembeza kombe la misaada wajengewe viwanda kugonga ukuta sasa wamerukia vita vya kiroho baada ya vya kimwili kuwagalagaza
 
Kinacho nishangaza katika awamu hii ndio hiko, atajiri wanaoenakana kama watenda dhambi.
Wakati kama ukikaa nao vzuri, uka punguza kodi uka punguza regulations ngumu hao ndio huwa wana saidi uchumi kukua, na ma midleclass kuongezeka
Wanawaogopa matajiri kama Trump iko siku watawamaliza kisiasa. Watagombea na kuwafuta Kazi. Siasa zetu ni kuutukuza umasikini. Ukiinuka tu wewe utabebeshwa mengi
 
Back
Top Bottom