miss chagga
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 57,815
- 49,031
ndoa si harusi na harusi si ndoa.. wakiweza kudadavua haya maisha yatakuwa mepesi sana
Ushaitoa au wasubiri kutolewa?Sawia kabisa, wengine tunaolewa ili kutoa nuksi tu.
Hatujajiandaa na maisha ya kindoa
NshatolewaUshaitoa au wasubiri kutolewa?
Hongera sana ...umetolewa zote?Nshatolewa
Zote kabisaHongera sana ...umetolewa zote?
Wengi huwa hatujiulizi maswali hayo.NDOA KWANINI HAZIDUMU SIKU HIZI
Ndoa hazidumu kwa sababu kabla ya kufunga ndoa watu wanakuwa obssesed na wedding ceremony imaginations, bila kujua ndoa inaenda mbali zaidi!
Kuna ndoa na kuna harusi...
Wengi mnapenda zaidi harusi, na mnapowaza ndoa picha inayowajia ni suti kali, boonge la shela kutoka Uturuki, make up ya ukweli ya bibi harusi kutoka Maznat Mikocheni, mashosti kuingia ukumbini na wimbo wa selfie,wanafiki kukomeshwa kwa jinsi pati yako itakavyokuwa kali pale Karimjee Hall.
Je, Umewahi kuwaza?
1. Mmeo au mkeo akiumwa miaka 5 mfululizo utaweza kumvumilia?
2. Watoto watakapozaliwa na ulemavu utawa-care namna gani?
3. Mtakapokosa watoto miaka 6 ya ndoa utahimili maneno ya mama mkwe na mawifi kwamba unawajazia choo cha kaka yao na huna kizazi?
Ndoa ni zaidi ya sherehe ya harusi. Baada ya yale matarumbeta kuzimika usiku kifuatacho ni majukumu mazito na kiapo kisichovunjika.
Achana na fantasy za kwaito,waza mbali kidoogo.
Je, Uko tayari kuwa mme au mke wa mtu mmoja tu au Ma-Ex watarejea kidogo kidogo kama hupati satisfaction ya kutosha kama ya Ex wako?
Huwa mnawaza hayo au mnawaza zawadi ya kamati itatoa Verossa ya kuanzia maisha?
Sidhani kabla ya kuoa na kuolewa jiulize,unatamani ndoa au ni tamaa ya sherehe ya harusi?
Teh! Teh!Kila nikiwazaga kuoa naona bdo kichwa changu akijatulia kukaa na mtu 1 ndani" Ndoa si kitu cha mchezo
Kweli tupu.Kimsingi ndoa ni jambo jema na lenye kuleta faraja kubwa sana maishani kwa wana ndoa. Mambo sio mabaya kama hivyo yanavyotiwa chumvi, kuna ndoa nyingi zimedumu kwa upendo, furaha na amani. Asiliamia kubwa ya wana ndoa wana maisha bora zaidi kuliko waliyokuwa nayo kabla kuoa au kuolewa. Ndoa zimewafanya wamekua kiakili na kutambua majukumu kimaisha katika jamii. Kuoa au kuolewa kunatimiza misingi mikuu ya maisha ya mwanadamu. Ndio kuna changamoto za hapa na pale hazikosekani lakini hiyo ni kawaida ya maisha, bila changamoto hakuna maisha, changamoto zinatufundisha kukomaa na kujenga ukaribu wa wanandoa, hata ukiishi na wazazi, ndugu lazima mikwaruzano ya hapa na pale ijitokezee, huwezi kuacha kuishi kwsabababu kuna matatizo katika ndoa. Ndoa moja ya ndugu au rafiki kuwa mbaya au kuvunjika haina maana kwamba 'Ndoa Hazidumu Siku Hizi' na kupelekea kuchochea mawazo mabaya kuhusu ndoa. Inasikitisha kuona vijana wengi wakiwa na mawazo hasi kuhusu ndoa wakati wala hawajaingia katika ndoa. Ni faraja ilioje unaporudi nyumbani kwako jioni baada ya siku ndefu na ngumu kazini unakuta angalau kuna mwenzako wa kumshirikisha jinsi siku yako ilivyoenda leo. Tuitazame ndoa kwa mapana na marefu na sio kirahisi rahisi tu na kejeli. Wanaokejeli ndoa hebu wajiulize wao wangekuwa wapi leo kama taasisi hii ya ndoa isingekuwepo.
Nakubali kabisa.duuh iko wap furaha yangu na tabasamu langu nilipokuwa single.daaah limepoteaHill halinihusu. kuoa haimo katika mipango yangu ya maisha. ukitaka kupoteza furaha ya maisha yako, oa/olewa.
NDOA KWANINI HAZIDUMU SIKU HIZI
Ndoa hazidumu kwa sababu kabla ya kufunga ndoa watu wanakuwa obssesed na wedding ceremony imaginations, bila kujua ndoa inaenda mbali zaidi!
Kuna ndoa na kuna harusi...
Wengi mnapenda zaidi harusi, na mnapowaza ndoa picha inayowajia ni suti kali, boonge la shela kutoka Uturuki, make up ya ukweli ya bibi harusi kutoka Maznat Mikocheni, mashosti kuingia ukumbini na wimbo wa selfie,wanafiki kukomeshwa kwa jinsi pati yako itakavyokuwa kali pale Karimjee Hall.
Je, Umewahi kuwaza?
1. Mmeo au mkeo akiumwa miaka 5 mfululizo utaweza kumvumilia?
2. Watoto watakapozaliwa na ulemavu utawa-care namna gani?
3. Mtakapokosa watoto miaka 6 ya ndoa utahimili maneno ya mama mkwe na mawifi kwamba unawajazia choo cha kaka yao na huna kizazi?
Ndoa ni zaidi ya sherehe ya harusi. Baada ya yale matarumbeta kuzimika usiku kifuatacho ni majukumu mazito na kiapo kisichovunjika.
Achana na fantasy za kwaito,waza mbali kidoogo.
Je, Uko tayari kuwa mme au mke wa mtu mmoja tu au Ma-Ex watarejea kidogo kidogo kama hupati satisfaction ya kutosha kama ya Ex wako?
Huwa mnawaza hayo au mnawaza zawadi ya kamati itatoa Verossa ya kuanzia maisha?
Sidhani kabla ya kuoa na kuolewa jiulize,unatamani ndoa au ni tamaa ya sherehe ya harusi?
Duh!kuna style mnaita kwenda kuangalia mkato wa chumba.Sawia kabisa, wengine tunaolewa ili kutoa nuksi tu.
Hatujajiandaa na maisha ya kindoa
Ha haa mie mgeni wa hiyo banaDuh!kuna style mnaita kwenda kuangalia mkato wa chumba.
Ndo hivyo wenzio wakitaka kuolewa na bwana hawamtaki ndugu wanambembeleza wacheze sebene ndo wanamwambia nenda kaangalie mkato wa chumba baada ya mwezi ndoa inaota mbawa.Ha haa mie mgeni wa hiyo bana
hahaaaaaaaaaNakubaliana na wewe mkuu kwa asilimia zote,watu wanafikiria Ndoa ni lele mama,mie ningejua mwanzo Ndoa ikoje mbona ningesema basi staki tena,kama hukujikaza wallah hukai hata miezi 6,manake baada ya ndoa tuu ndio ma buzi ndio yatakua mengi mpaka unajiuliza jamani mlikua wapi mwanzo,kwa upande wa mume nae Totoz wanajileta mpaka unasikia kichefuchefu,upande wa pili kuna ma wifi na na mashemeji wana midomo na maneno makali utadhani wao hawana watoto au hawana mume/mke, lakini chamsingi bora hizo hela za mchango ukalipie japo kodi ya nyumba na usitake harusi kubwa
kwanza hapo kwenye harusi unaweza ukapa mtu akakutonya "yule alovaa nguo ya red anaecheza sana ndio mwanamke wake
na yeye ndio kamualika aje akuone tena kaja na wapambe wake wakuthamini kama unamfikia uzuri" hapo bi harusi picha lazima zitoke kama analia...