Nkobe
JF-Expert Member
- Feb 17, 2013
- 2,208
- 3,289
Lowasa anatokea mkoa wa Arusha wilaya ya Monduli. General tire ni kampuni la tairi ambalo lilikuwa mti wa mgongo katika uchumi wa Arusha, hata nchi kwa Ujumla. Pamoja kwamba kiwanda hiki Muhimu cha Tairi kimekufa katika hali ya sintofahamu, sijawahi kumsikia Lowasa akilalamika, au kuhudhunishwa na ufilisikaji wa kiwanda hiki. Nimewahi kumsikia Lema akilalamika na kutaka kiwanda hiki kifufuliwe, lakini jambo la ajabu Lowasa hakuwahi kusikika akiongelea kuhusu kiwanda hiki, pamoja kwamba kiwanda hiki kilikuwa muhimu sana kwa uchumi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.