Kwanini kuna muda wa kuisha matumizi kwenye vitambulisho vya Taifa?

Nijuavyo Mimi ni kuwa hususan sisi vijaana sura hubadilika badilika sasa NAHISI hapo ndo ilipo mantiki ya kubadilisha hizo ID na pasipoti, na hata huko walikoendelea hali ni hio hio tu mkuu. Lazima iwe na mda wa kuisha hicho kitambulisho, sio kiroja bali ni hali halisi.
 
Kitambulisho cha utaifa wa mtu hakuna tofauti na Tax Identificatio Number haipaswi kuisha muda huo ni uhuni, ni sawa na birth certificate hakipaswi kuwa na expire date
 
Ni almost ID cards zote zina-expire kuanzia passports (10 yrs); driving licenses (3 yrs); bank cards (10 yrs); n.k. n.k. n.k. Nadhani wana malengo kadhaa ya kufanya hivyo; mosi kuendelea kuwa na monitoring ya ownership - sasa wewe mzee wakupe ID card halafu upotee mazima itakuwaje? Bora hata "ukipotea" lakini wana uhakika ndani ya muda huo hakitakuwa kitambulisho tena na hakiwezi kutumika kwa namna yoyote au hakina effects zozote zile. Pili, id cards ni vyanzo vya mapato - hili sihitaji kulifafanua.
 
Nijuavyo Mimi ni kuwa hususan sisi vijaana sura hubadilika badilika sasa NAHISI hapo ndo ilipo mantiki ya kubadilisha hizo ID na pasipoti, na hata huko walikoendelea hali ni hio hio tu mkuu. Lazima iwe na mda wa kuisha hicho kitambulisho, sio kiroja bali ni hali halisi.

sawa kabisa, ihu ni sura kila baada ya miaka 10 inabadilika
 
Kitambulisho cha utaifa wa mtu hakuna tofauti na Tax Identificatio Number haipaswi kuisha muda huo ni uhuni, ni sawa na birth certificate hakipaswi kuwa na expire date
Hahahaaaaa.....

Mkuu mbona unafananisha certificates na Identification cards....

Think twice mkuu.....
 
Walifuata mfumo wa passport. Kweli tukifanya hivyo itakuwa gharama, kwa vile ni watanzania wachache wanahitaji pasi, na huwa kuna malipo fulani, tofauti na vitambulisho hivyo.
 
Ni control mechanism...kuna kufa au hata kuwa ushabadili uraia....
 
Jamaa yangu mmoja alinieleza kuwa baadhi ya nchi huko majuu driving licence zilikuwa hazina kikomo. Lakini waarabu alipoanza kufanya vitu vyao nao wakaamua kubadilisha gea angani ni kuweka kikomo, kama miaka mitano. Yawezekana hata NIDA walipatwa na hofu kama hiyo. Tusiwashutumu walikuwa au wana nia nzuri tu
 
Kitambulisho cha utaifa wa mtu hakuna tofauti na Tax Identificatio Number haipaswi kuisha muda huo ni uhuni, ni sawa na birth certificate hakipaswi kuwa na expire date
Birth certificate inakuwa na information ambazo azibadiliki katakana muda na kama photo, marital status, death na kadhalika.

Mfano, mtu anayetumia kitambulisho cha wizi ikifika muda wa ku-renew ndio mwisho kuendelea kukitumia.
 
Kitambulisho cha utaifa wa mtu hakuna tofauti na Tax Identificatio Number haipaswi kuisha muda huo ni uhuni, ni sawa na birth certificate hakipaswi kuwa na expire date
kwanini wasiweke utaratibu utakaokuwa wa kuchek na kurekebisha taarifa kwenye mfumo kuliko gharama ya kutengeneza kitambulisho kipya. Inaweza ikatumika ata mfumo wa kuweka sticker maalumu kuonyesha kilishahakikiwa kuliko gharama ya kutengeneza kipya.
 
Na pia nafikiri kuwe na mfumo wa kitambulisho kimoja kuliko kutengeneza vitambulisho vingi, hapa namaanisha kuwe na kitambulisho cha taifa kinachoonyesha taarifa zako muhimu kama uraia,kazi,kura,eneo,pension,kama ni mwanafunzi. yaani vitambulisho vyote kiwe katika kitambulisho kimoja hapo itasaidia kupunguz matumizi makubwa na gharama.
 
kwanini wasiweke utaratibu utakaokuwa wa kuchek na kurekebisha taarifa kwenye mfumo kuliko gharama ya kutengeneza kitambulisho kipya. Inaweza ikatumika ata mfumo wa kuweka sticker maalumu kuonyesha kilishahakikiwa kuliko gharama ya kutengeneza kipya.
ni uhuni na kujitengenezea fursa, hakuna umuhimu wala sababu za msingi kufanya hivyo.
 
Tatizo letu sisi watanzania wengi wetu hatutaki kueleweshwa,unamkuta mtu anaongea kitu ambacho hana uwakika nacho na analazimisha kiwe hivyo anavotaka yeye.
Suala la msingi kuhusu expiring date ya kitambulisho cha taifa ni ku update taarifa zako bi nafsi wewe raia.
 
Nimejiuliza hili nalo sikupata jibu.

Najua kuna wadau wanaweza wakatoa majibu kadhaa kuhusiana na swali hili. Tumeona mchakato mzima wa kuandaa vitambulisho vya taifa ulivyokuwa umegubikwa na giza giza jingi pamoja na ukakasi wa kutosha tu. Ni wengi tulianza kujiuliza kuwa kuna nini nyuma ya jambo hili ambalo kama lingefanyika kwa ulaini lilikuwa jema kabisa machoni pa watanzania

Lakini wenye ufaham wengi walianza kuona kuwa hii hali ya ukakasi, magugu, mabonde mabonde ni ishara mbaya huko mwishoni. nasi tumekuja kuona kuwa pesa nying sana zimetumika kwenye kile kinachoonekana kuwa ni uaandaji wa vitambulisho hivi.

SWALI NINALOJIULIZA PAMOJA NA UKAKASI WOTE HUO KWA NINI KUNA EXPIRY DATE kwenye Kitambulisho cha Taifa? kwa nini ili kuokoa pesa kisingetengenezwa kuwa kina expiery mhusika anapofariki? ku expiry huku je kuna maanisha kuwa ifikapo tarehe 2023 naacha kuwa mtanzania inabidi niombe upya uraia? ni nini kinanifanya niombe tena kitambulisho cha uraia ikiwa sikuukana uraia wangu?

Inasemekena zimetuka zaidi ya elfu 70 ka kitambulisho kimoja hivyo baada ya miaka kadhaa ijayo pesa hizi zitatumika tena? na bila shaka zitakuwa zimeongezeka sana kwa sababu ya wingi wa watu kuongezeka na gharama za maisha pia. kwa nini mnainajisi tanzania kwa kiasi hiki?
SMART LIFE(cards) lazima ziwe na muda ili Uweze Kudhibitiwa....Tumeingizwa kwenye SMART LIFE ili tudhibitiwe....funguka...
 
Back
Top Bottom