Kwanini imezoeleka kuona mtu alietokea maisha yenye hali nzuri (wa kishua) wazazi wake ni waajiriwa, kwanini sio wazazi wafanyabiashara ?

round kick

JF-Expert Member
Feb 3, 2025
611
2,110
Kwanini imezoeleka kukadiria mu flani kama kwao wana maisha mazuri basi wazazi wameajiriwa, kwanini isiwe imezoeleka kukadiria wazazi ni wafanyabiashara ?

Yusufu kwao wana maisha - mzee ni Engineer, Mama ni Muhasibu

Abdallah kwao wa kishua - Baba mkurugenzi, Mama ni mhadhiri pale IFM

Jacky kakulia maisha safi - Mzee wake ni Judge, mama yupo kitengo cha ugavi

Ukhty kwao wana pesa - Mshua wake ni ocd polisi, mama yake ni afisa masoko wa voda


Conclusion niliyoona wafanyabiashara ni matajiri lakini wengi ni waarabu na wahindi, kwa wabongo tajiri moja mfanyabiashara kazungukwa na wenzake wengi wenye hali za chini lakini kwa upande wa wafanyakazi serikalini sio matajiri lakini angalau kuna uwiano kiuchumi kwa wengi.
 
Si kweli
Hata kwa wasanii kina Master Jay baba alikuwa mkurugenzi Tanesco, Vanessa mdee baba alikuwa balozi, Jux mama alikuwa Bandari, Crazy GK mzazi wake lecturer, n.k. ni wasanii waliosifika kuwa na hadhi ya kishua
 
Watanzania wengi bado wanahusudu zaidi ajira hasa za serikalini.
 
Mkuu, uhalisia ni kuwa biashara kwa Afrika, hususani kwa jamii ya watu weusi, ni ngumu sana.

Narudia.
Biashara akiifanya mtu mweusi ni ngumu sana.

Sio kuwa hiyo biashara haina faida, biashara unakuta ina faida kubwa lakini kuna jambo, kuna kitu, ndio maana utakuta matajiri wengi wako katika mkondo wa kuchota pesa sehemu na kuzifanya ziwe zao, na sio katika biashara.
 
Civil servants: Vyeo vikubwa vya serikali kross nyingi % nazo hazikawii hvyo matumizi husika Huwa n yakufuja pesa

Businessman: Huyu Kila pesa anayotumia n yake hvyo lazima iwe na adabu

Mwangalie huyo mfanyakaz akizeeka au kizazi chake kikianza pata wajukuu uje ufananishe na kizazi Cha mfanyabiara utapata majibu.

Mambo ni Yale Yale "Money is better than Education" we upo upande gani?
 
Back
Top Bottom