Kwanini Dar kuna vibanda vya chips kila mtaa?

Habarini wadau?

Mimi ni mkazi wa Mbeya, na nimekuwa nikipita katika majukwaa mbalimbali ya JamiiForums na kusikia watu wakisema watu wa Dar wanakula chips sana.

Sasa nina wiki3 toka nimekuja Dar, na nimeshangaa kuona kibanda cha chips karibia kila mtaa, nimeshangazwa na ulaji chips uliopitiliza hapa Dar hasa inayochanganywa na mayai.

Kwa Dar es Salaam chakula kikuu ni chips, tofauti na sehemu nyingne za nchi ambazo chakula kikuu ni ugali, ndizi au wali.

Chips c chakula kinachoshauria ule kila siku, atleast mara 1 kwa mwezi, vinginevo unahatarisha afya.

Naainisha madhara ya chips mayai ya muda mrefu:
1.Kwa wanawake, kizazi kinalegea, pia uchache wa virutubisho husababisha watoto kuzaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi.

2. Husababisha mafuta mwilini yanayoleta sukari na presure. Matatizo ya ini sababu ya kolestro ilopitiliza.

3. Upungufu wa mbegu za kiume. Na zisizo na ubora.

4. Mimba japo ni indirect/

5. OBESITY NA UNENE ULOPITILIZA

Japo chips ni tamu ila si nzuri kwa afya.

Poleni wana Dar es Salaam, wala chips wakuu katika ulimwengu huu
Ushahidi wa research au ndiyo mastory ya Prof Maji Marefu
 
Badala yakusema dar nimeona fursa kadhaa za biashara!we umeona mabanda ya chips tu?? Ukiishi huu mji ndio utaelewa,watu wapo fasta kuliko mda wenyewe!hakuna mda wakusonga ugali na kupika makande uku!na afya tunazo za kutosha na Mungu anatubariki sana tu
uwongo mtakatifu,mna afya nyie??goli moja mnaomba maji ya kunywa??ndo maana hili nijiji la kwanza kwa wanawake kuchepuka.mf wema,lulu,shilole,sinura ambao ndo wake zenu.karibu mwanjelwa mbeya uone shughuli pevu
 
Poleni wana Dar es Salaam, wala chips wakuu katika ulimwengu huu
Nimeishi Mbeya na Dar. Licha ya kwamba viazi mviringo vinalimwa kwa wingi Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (ikiwemo Mbeya), watu wa huko Mbeya hawajui kuifanya chipsi (french fries) iwe na ladha ya kuvutia, na sishangai huyu jamaa anavyoshangaa vibanda vingi vya chips Dar kwani yeye kwao amezoea kupikiwa hovyo hovyo na anaona chipsi ni kitu cha kawaida tu. Naamini kama angeonja chipsi za Dar, hakika siku ya kurudi angezipakia kwenye shangazi kaja yake akawaonjeshe akina malafyale.
Hata nilipoenda Arusha, nilikuta mishikaki na supu ya kule haina mvuto kama ya Dar. Ukweli ni kwamba Dar ni jiji Kuu na watu wake ni wabunifu kwenye kila nyanja
 
Wewe umeshangaa wingi wa vibanda, mimi nilishangaa mazingira ya uchafu wa vibanda hivyo, vumbi, inzi na uchafu wa waandaji chips wenyewe.
 
Badala yakusema dar nimeona fursa kadhaa za biashara!we umeona mabanda ya chips tu?? Ukiishi huu mji ndio utaelewa,watu wapo fasta kuliko mda wenyewe!hakuna mda wakusonga ugali na kupika makande uku!na afya tunazo za kutosha na Mungu anatubariki sana tu
Kwanza angejiuliza kwanini dada zake wakija hawataki kurudi kwao
 
Kwanza angejiuliza kwanini dada zake wakija hawataki kurudi kwao
Hahaha apo ungejiuliza kwanza wewe kwa nini wake zenu,dada wikiend wanatoroka mkoani kuja dar kusalimia kidogo na kurudi?? Nakumbuka kuna dada mmoja ivi kwy dala2 juzi alipigiwa simu tukiwa mitaa ya kinondoni akamdanganya mumewe eti nipo apa mwanjelwa sokoni,kumbe yupo kino anapelekwa machinjioni!
 
Nimeishi Mbeya na Dar. Licha ya kwamba viazi mviringo vinalimwa kwa wingi Kanda ya Nyanda za Juu Kusini (ikiwemo Mbeya), watu wa huko Mbeya hawajui kuifanya chipsi (french fries) iwe na ladha ya kuvutia, na sishangai huyu jamaa anavyoshangaa vibanda vingi vya chips Dar kwani yeye kwao amezoea kupikiwa hovyo hovyo na anaona chipsi ni kitu cha kawaida tu. Naamini kama angeonja chipsi za Dar, hakika siku ya kurudi angezipakia kwenye shangazi kaja yake akawaonjeshe akina malafyale.
Hata nilipoenda Arusha, nilikuta mishikaki na supu ya kule haina mvuto kama ya Dar. Ukweli ni kwamba Dar ni jiji Kuu na watu wake ni wabunifu kwenye kila nyanja
 
wanaume wa dar tunapenda sana chips sababu ndo chakula ambacho kinapatikana kirahisi
Kwa jinsia yoyote; WAKATI WA KAZI NA NI CHAKULA AMBACHO KINA USALAMA ZAIDI, na haraka hata kubebeka. Chakula hiki kimekuwa maarufu sana pale pirika za kiuchumi zilipoongezeka. Na hii ni sifa ya majiji yote duniani yaani uwepo wa fast food kila kona
 
Hahaha apo ungejiuliza kwanza wewe kwa nini wake zenu,dada wikiend wanatoroka mkoani kuja dar kusalimia kidogo na kurudi?? Nakumbuka kuna dada mmoja ivi kwy dala2 juzi alipigiwa simu tukiwa mitaa ya kinondoni akamdanganya mumewe eti nipo apa mwanjelwa sokoni,kumbe yupo kino anapelekwa machinjioni!
Umenielewa kweli au ndo walewale?
 
Back
Top Bottom