Kwanini CCM wanafurahiria Prof Lipumba kutaka kurudia uongozi CUF?

Mkuu huko sikutaka kupagusa sana maana kusema hivyo ni kutibua maumivu yaliyokwisha potea, Bora umeenda in deep uwakumbushe watanzania ambao minds zao zinachezewa.
 
Ishu si CCM wanapenda UKAWA ivunjike, Mpenda haki yeyote lazima awaonee huruma CUF walivyo vipofu na wanavyomezwa na kupotezwa ndani ya Ukawa.
Ukawa haina usawa, ukawa imeundwa kumjenga CHADEMA zaidi na si kuinua upinzani kwa ujumla wao.
Nani anakikumbuka NCCR now, Mabunge Mazezeta ya CUF yamekosa mtu wa kuwaongoza na kuwatetea ndani ya UKAWA, Maalim seif yeye anawaza Zanzibar yake tu na haifikiliii kwa vyovyote CUF bara, wamenyimwa nafasi zote muhimu ndani ya ukawa Uwazir kivuli, Umeya Dar na hata usemaji.
Wazee wenye maono ndo maana wameenda kumpigia magoti PROF LIPUMBA arudi
 
Duhh ccm wameuharibu mpango wa lipumba maana viongozi wa cuf wameisha mshitukia maana mara baada ya katibu mkuu kwenda UN huku lipumba anataka kurudi huu ni mchezo mchafu wa ccm
 
Toa mfano boss
Huyo Pro Lipumba wako, Unajiuzulu huku ukidai nafsi yako inakusuta kisha unatengua maamuzi yako!Matumizi ya PhD yako yako maeneo gani hapo?Kwahiyo nafsi yake haimsuti kwa kutengua maamuzi yeke?
 
Ukishaajiita Pro Magufuli ni CCM tu! So kazi yako ni kumfanyia promo Lipumba.Hamna madhara kwenu endeleeni kumpigia debe kama mtafanikiwa.
 
Ukishaajiita Pro Magufuli ni CCM tu! So kazi yako ni kumfanyia promo Lipumba.Hamna madhara kwenu endeleeni kumpigia debe kama mtafanikiwa.
Ndio Mimi ni Pro Magufuli kweli, ni ccm kweli.
Kuwa mkweli huoni hatar ya kupotezwa waliyonayo CUF ndani ya UKAWA?
Huoni kuwa CUF na vyama shirika ndani ya ukawa vinanyonywa tofauti na mahubir yenu yanayohamasisha usawa na haki?
Cuf anachukuliwa poa na mashabiki wa ukawa haswa chadema na kuwaona kama nyongeza wakati in reality mko sawa.
 
Gazeti la Jamvi La Habari la leo leandika kuwa, 'Sasa ni dhahiri kwamba hali ndani ya Chama cha wananchi CUF si shwari kama ilivyokuwa hapo awali Gazeti hili linaweza kuthibitisha.

Kitendo cha aliyekuwa mwenyekiti wa Chama hicho Prof . Ibrahim Lipumba kutangaza kutaka kurejea nafasi yake ya uenyekiti kwa mujibu wa katiba hiyo kimeibua hisia tofauti tofauti miongoni mwa wanachama na viongozi waandamizi wa Chama hicho huku wakionyesha kugawanyika kwa kiasi kikubwa.

Nini Mtazamo wako? ?.


 
Prof. Lipumba mwanasiasa kupitia chama pinzani, alianza kugombea nafasi ya URAIS tangu mwka 1995 hadi 2010 bila mafanikio.

Wewe binafsi unajifunza nini, kutokana na hili,,, na una neno gani kuhusu hili.

Mimi nimemaliza.
 
Ndio mwanasiasa aliyezani atapata umaarufu baada yakujiondoa upinzan wkt wa kampen, ila ndio ikawa anakufa kifo cha mende kwenye siasa
 
Prof. Lipumba mwanasiasa kupitia chama pinzani, alianza kugombea nafasi ya URAIS tangu mwka 1995 hadi 2010 bila mafanikio.

Wewe binafsi unajifunza nini, kutokana na hili,,, na una neno gani kuhusu hili.

Mimi nimemaliza.
Hakua na faida yeyote, alikuepo kwa kazi maalum.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…