MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
- Thread starter
- #21
Mkuu huko sikutaka kupagusa sana maana kusema hivyo ni kutibua maumivu yaliyokwisha potea, Bora umeenda in deep uwakumbushe watanzania ambao minds zao zinachezewa.Kujua kwa nini CCM wanapiga debe la nguvu la kushinimiza CUF wampokee tena Profesa Lipumba kwenye nafasi ya uenyekiti, tujikumbushe kidogo kile kikao cha October mwaka jana kilichofanyika pale hotelini Peacock ambapo alitangaza kujivua Uenyekiti kwa madai ya kutoafikiana na ujio wa Lowassa kwenye Ukawa, wakati siku chache alionekana kwenye vyombo vya habari akishangilia ujio wa Lowassa!
Tujikumbushe pia kuwa mara tu alipomaliza kikao hicho pale Peacock alikimbizwa moja kwa moja uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere ambapo alikwea 'pipa' kuelekea Kigali huku akiimbatana na 'bodyguards' kutoka KITENGO.
Vile Vile ilifahamika kuwa gharama zote za hotel alikofikia Profesa Lipumba kule Kigali ziligharimiwa na TI...SS.
Kwa hiyo hapo ndipo unapata jawabu ni kwa nini Chama Cha Majipu kinashangilia sana jaribio la Lipumba la kutaka kurejea CUF kwa nafasi yake ya Uenyekiti.