Kwanini CCM inaendelea kushinda chaguzi, licha ya kuwa ndio chanzo cha umasikini wa taifa letu, rushwa na ufisadi?!

Simpo tu.... Wekeni tume huru ya uchaguzi na mkuu wa Polisi wa wilaya asiamrishwe na mwenyekiti wa MCC wa wilaya then tuone itakuwaje!!!!!
 
Wanabodi.

Hili ni bandiko mwendelezo wa Licha ya CCM kuwa chanzo cha umasikini, ujinga, rushwa na ufisadi, kwanini CCM bado huwa inashinda chaguzi mbalimbali?
Leo naanzia nilipoishia wiki iliyopita, nikiendeleza Makala zangu elimishi Kwa Maslahi ya Taifa, nikizungumzia mambo mbalimbali ya taifa letu. Leo nikiendelea kueleza kwa nini, licha ya kuwa CCM ndio chanzo cha umasikini wa taifa hili, ndio chanzo cha rushwa na ufisadi, na kuendeleza ujinga kwa Watanzania, lakini CCM bado imeendelea kushinda katika chaguzi mbalimbali hata baada ya Tanzania kuanzisha mfumo wa vyama vingi. Tumefanya chaguzi kuu 5 na zote CCM imekuwa ikiibuka mshindi, jee kushinda kwa CCM, ni kwa sababu CCM inakubalika sana kwa kuwaletea Watanzania maendeleo, CCM inashinda kwa kukosekana kwa upinzani imara na madhubuti, au CCM inashinda kwa sababu ya mazoea tuu na ujinga wa Watanzania, kutokana na elimu duni ya mpiga kura, na umasikini, uliotopea, hivyo wapiga kura wengi wa Tanzania kujikuta hawana uwezo wa kufanya informed decision?.

Tanzania tulipoingia mfumo wa vyama vingi, tuliuparamia tuu, bila kujiandaa kimawazo, kimifumo na kisheria, kuwa nchi ya vyama vingi, hivyo tumeingia kuwa nchi ya vyama vingi, kwa kubadili tuu katiba, bila kubadili mifumo, sheria na mitazamo, matokeo yake, tumeanzisha vyama vingi ndani ya set up ya mfumo wa chama kimoja,huku CCM kikiendelea kuwa chama dola CCM, na vyama vingine vikaanzishwa kushindana na chama dola.

1. Hoja ya kwanza, ni kutoka kwa wana CCM wenyewe kuwa CCM inashinda kwa sababu CCM ndicho chama pekee kilichotapakaa nchi nzima hadi vijijini, na kinapendwa na Watanzania, na kimekubalika kwa kuwaletea Watanzania maendeleo, nitaeleza kidogo kupendwa huku kwa CCM ni kupendwa gani, na hayo maendeleo CCM iliyoyaleta ni maendeleo gani.

2. Lakini sababu halisi ya CCM kuendelea kushinda chaguzi mbali mbali kwa mtizamo wangu, sio kwa sababu CCM inapendwa sana na inakubalika sana kwa kuwaletea Watanzania maendeo, (maendeleo gani?), bali CCM inashinda na kuendelea kushinda kwa sababu, Tanzania bado tuko kwenye setup ya mfumo wa Chama kimoja, na CCM bado ni chama dola, chama bado ndio kimeshika hatamu za uongozi wa nchi hii, hivyo bila kubadili setup ya mfumo kimoja, na kukiondoa chama dola kwenye mindset ya Watanzania, CCM itaendelea kushinda na kutawala nchi hii kwa miaka mingi ijayo.

3. CCM ni chama tajiri, ambapo kimeanzishwa kwa kupora mali za Watanzania. Tulipoanzisha vyama vingi ilibidi CCM kivunjwe kwanza, na zile mali za CCM, zilizotokana na michango ya lazima ya Watanzania wote, yakiwemo majengo ya serikali, viwanja vya umma ambavyo CCM ilivimiliki wakati wa mfumo wa Chama kimoja, vilipaswa virudishwe serikalini, CCM ianze moja kwa mali zake halali tuu, kama vyama vingine, lakini kitendo cha CCM kusajiliwa hivyo hivyo kilivyo na ukwasi loot ya Watanzania, hakuna Chama cha kushindana na CCM na kuingia ikulu!.

4. Mind set ya vyombo vyote vya utendaji na utawala, iko ki CCM CCM tuu, kuanzia Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, vyombo vya dola, na watendaji wa vyombo vingine vyote vya kiutendaji, akiwemo Msajili wa vyama vya Siasa, wote wako ki CCM, CCM!. Mimi sisemi kuwa NEC sio tume huru, kwa sababu uchaguzi unaendeshwa kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni, lakini kwa vile NEC kuanzia Mwenyekiti wake, Mkurugenzi , makamishna, na wakurugenzi wa halmashauri wote wanateuliwa na Mwenyekiti wa chama kimoja wapo, kuna uwezekano akateua makada watupu wa CCM, hivyo zoezi la uchaguzi kuendeshwa kwa ukada ukada zaidi kuliko utendaji ndio maana kuna watu wanapewa barua za utambulisho, wengine wananyimwa!. Kama mtu kama Jaji Mkuu wa Tanzania, anakwenda kugombea CCM, au CDF mstaafu!, hii maana yake hawa ni makada!. Kinachotakiwa kufanyika ni kubadili sheria ya uteuzi, watafutwe watu waadilifu ambao ni neutral kabisa kuongoza NEC, na Ofisi ya Msajili wa vyama, na makamisha kufanyike ushirikishwa wa wadau katika composition yao, ili neutrality sio tuu ionekane bali kuonekana ikitendeka. Pia tubadili sharia zetu za uchaguzi ziwe za haki.

5. CCM imejikita Vijijini, Wapinzani Wamejikita mijini, kutokana na ukongwe wa CCM ambacho kilikuwa chama dola kilichoenea nchi nzima kwa mujibu wa sheria, kuanzia wajumbe wa nyumba kumi, mashina, matawi nchi wamesambaa nchi nzima, kutokana na utajiri wa CCM, CCM ndicho chama pekee chenye uwezo wa kuwa na ofisi nchi mzima, tena sio ofisi moja, bali ni ofisi nne kwenye baadhi ya maeneo, ofisi ya CCM, ofisi ya UVCC, ofisi ya UWT, na ofisi ya Jumuiya ya Wazazi, ambako kote huko kuna maofisa wanaolipwa mishahara, wakati ofisi za vyama vya upinzani ni watu wanajitolea nyumba zao na wanavitumikia vyama hivyo kwa mapenzi yao tuu bila kulipwa chochote!, hivyo chochote ambacho CCM inakipanga kinawafikia wananchi wa chini, na wakati wa kampeni, kama CCM inawadanganya Watanzania, ni wengi zaidi watadanganyika, kwa sababu CCM imewafikia, lakini akitokea mpinzani kusema ukweli, ukweli huu huishia mijini tuu, hivyo kwa mazingira haya, huwezi kushindana na CCM.

6. Ujinga wa Watanzania, tangu tumeanzisha mfumo wa vyama vingi, hakujawahi kutoa elimu yoyote ya uraia, kuwaelimisha Watanzania umuhimu wa uwepo wa vyama vingi, hivyo waliowengi wamedanganywa kuwa vyama vya upinzani vinakuja kuleta fujo na kuhatarisha amani yetu na utulivu, sasa ukiwasikia viongozi wa upinzani wanavyoongea kwa jazba, na vyama vyenyewe ni vya kiharakati, Watanzania wanaogopa kuviamini. Ingetolewa elimu rasmi ya uraia na kuwafikia Watanzania wote, na Tanzania ikawa na vyama serious vya upinzani wa kweli, na Watanzania wakaelimishwa jinsi CCM ndio chanzo cha umasikini huu, ujinga huu, rushwa hii na ufisadi huu, siku nyingi CCM ingeisha pumzishwa kwa amani!, hakuna mtu yoyote anayependa kula mboga siku zote!, Watanzania wangependa sana kubadili mboga, tatizo ni hakuna hata hiyo mboga ya kubadilisha!.

7. Umasikini uliotopea, ambao pia pia unakwenda sambamba na ujinga. Mtu masikini wa kipato, chakula cha shida, mlo mmoja kwa siku, anaishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, akili yake pia inadumaa. Mtu kama huyu shida yake ni mlo, na mavazi, sasa akiletewa ile Tshirt na kofia, na pilau ya siku moja, inatosha kabisa kukichagua chama kilichokulisha na kukuvisha, anakuwa hana uwezo kusikiliza sera na kufanya informed decisions, angalieni maeneo yenye umasikini uliotopea na elimu duni ndio strong holds za CCM. Mikoa yenye ehueni kiuchumi kama Arusha, Kilimanjaro, Bukoba, Iringa, Mbeya. Tanga na maeneo ya mijini, watu walioelimika, kidogo wanaweza kuchagua upinzani, lakini mikoa yenye umasikini wa kutupa kama Dodoma, etc, usitegemee upinzani unaweza kushinda!, shida ya masikini ni njaa tuu, CCM ndicho chama kinachoongoza kwa kugawa rushwa, ushahidi wa kazi nzuri iliyofanywa na fedha za Kagoda upo!. Hivyo CCM kuutumia umasikini wa Watanzania na Ujinga wa Watanzania kama mtaji wake wa Ushindi.

8. CCM inaendelea kushinda kwa sababu, uwanja wetu wa mashindano ya siasa ni uwanja tenge ambao umelalia upande wa CCM, ni kama kugombea kisu cha makali kuwili, halafu mgombea mmoja ameshika kwenye mpini, na mwingine kwenye makali. Vyombo vyote vinaipendelea CCM, kuanzia mfumo uliopo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, vyombo vya dola, huku mgombea mmoja mwenue kila kitu, JWTZ, Polisi, ukwasi mkubwa, ameishika dola na kuitoa igombewe na wengine wasio na kitu kabisa!.

9. CCM inaendelea kushinda kwa sababu Tanzania bado hatuna upinzani Imara, huu upinzani uliopo sasa ni upinzani uchwala, hivyo kamwe hauwezi kushinda kushika dola hivi hivi ulivyo. Mimi nakubaliana kabisa na hoja ya Baba wa Taifa kuwa upinzani wa kweli utatoka CCM!, huu upinzani dhaifu uliopo sasa, na utitiri wa vyama, vyama vya kiharakati, hauwezi kuwapeka wapinzani ikulu. Kujiengua kwa Lowassa kutoka CCM ile 2015, na kujiunga upinzani, ndiko kulikoupatia upinzani mafanikio makubwa kabisa katika upinzani nchini Tanzania, tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, ingekuwa sio hali ya afya ya Lowassa, wafuasi wake na wale wote wenye Imani na Lowassa wangemfuata!, CCM ingepigwa chini!. Kama kwa hali ile tuu alivyo, ameweza kuvuna kura milioni 6, ambazo ni nyingi kuliko zilizomrudisha Kikwete ile 2010, tena kwa taarifa tuu, kwa upande wa Zanzibar, Lowassa ndio aliyepata kura nyingi kuliko Magufuli, kwa mujibu wa matokeo ya NEC, hivyo Zanzibar CCM ilipigwa chini!, hivyo kama Lowassa angekuwa fiti kabisa kiafya na hana mazongezonge ya ufisadi, amini usiamini, CCM ingepigwa chini ile 2015.

10. Wapinzani hawana sera, wala hawajui wanatakiwa kufanya nini, upinzani wa kweli, unapaswa kuonyesha sera mbadala na CCM, mfano sera ya elimu ya CCM ni elimu bure kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne, upinzani wao wakasema sera yao ni elimu bure toka chekechea hadi chuo kikuu. Hapa wangekuwa ni wapinzani makini, sera hii tuu ingetosha kuipiga chini CCM!. Au sera ya Afya bure. Wapinzani hawakupaswa kuishia kusema maneno matupu tuu ya elimu bure hadi chuo kikuu, walipaswa kuja na roadmap ya how?. Wangewaeleza Watanzania watabana wapi matumizi ili kupata kupata fedha za kugharimia elimu bure, kwa kuainisha ufisadi wa serikali ya CCM, mfano kusema utaunda baraza dogo tuu la mawaziri lenye wizara 10, hizi zitaokoa kiasi hiki ambacho kitapelekwa kwenye elimu. Au kujumlisha jumla ya fedha zote zilizofujwa na CCM kwenye ufisadi wa EPA, Deep Green, Meremeta, Escrow, etc na kuonyesha jinsi ambavyo zingetumika kugharimia afya na elimu bure, ili kuwapa Watanzania chaguo mbadala!.

Wasalaam

Nawatakia Furahi Dei Njema.

Paskali
kwa upande mwingine, hadhi ya CCM inarejea kwa gharama kubwa kwa demokrasia changa ya Tanzania. Katika siku za hivi karibuni madiwani na wabunge wa upinzani wamekuwa wakihama vyama vyao kwa madai kuwa Rais Magufuli anafanya kazi nzuri.
Hata hivyo, wapinzani wanadai rushwa imekuwa ikitumika kuwashawishi wahamie CCM.
Kama hiyo haitoshi, Rais Magufuli amekuja na maagizo mapya juu ya namna ya kufanya siasa.
Hakutakuwa tena na mikutano ya siasa ya hadhara mpaka wakati wa uchaguzi isipokuwa kwa wabunge na madiwani katika maeneo yao.
Wakati huohuo, Rais Magufuli mwenyewe anafanya mikutano kama kawaida akichanganya shughuli za chama na serikali.
Kadhalika, viongozi wa upinzani wamejikuta matatani wakikamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi pale wanapotoa matamshi mbalimbali, huku wengine wakihofia usalama wao baada ya kupokea vitisho.
Kwa ujumla tutegemee CCM mpya ya Magufuli kuimarika zaidi, lakini pia tutegemee kudorora kwa upinzani.
Si ajabu kwamba, baada ya miaka mitano ya Rais Magufuli, vyama vyaupinzani vitarejea katika hali yao ya miaka ya 1990 wakati wakipigania haki za msingi za kidemokrasia, badala ya kuzungumzia miradi ya maendeleo, mbadala wa ile ya CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unashindwa kupanga maisha yako unailaumu CCM? vyma vya siasa mbinu za kisiasa wameishiwa wanataka uwazi huku wenyewe sio wawazi wamejaa ubinafsi tuuuu miaka zaidi ya 20 unalia lia tuuu, vijana ndio usiseme ni kulalama tuu kazi hamna kazi hamna wakipata hela kodogo wanawaza kutomba tuuu na kulewa alafu kesho anarudi kijiweni kuilaumu serikali.......hahahaa viongozi wa vyama vya siasa wasipobadilika na kufanya siasa kisomi kwa uwazi na uaminifu kama mahubiri ya dini hakika wataendelea kulia lia sana kama heading ya Pasko hapo.
 
Pasco ni sehemu ya watanzania wajinga wanaoishindisha Ccm.

Pasco ni sehemu ya mafisadi na watetezi wa mafisadi waliotaka kuingia kwenye mfumo wa utawala lakini ikashindikana au niseme ikazuiliwa na watanzania waliobobea kwenye ujinga.

Pasco anaishi kwa vibahasha kama ilivyo wanahabari wengi nchini.
Paskali ni mchumia tumbo wa siku nyingi sana. Nyie mmechelewa sana kumshtukia
 
Nawatakia maandalizi mema ya uchaguzi wa serikali za mitaa, ila mshindi wa jumla ni CCM, tena kwa ushindi wa kishindo maana hata kabla ya uchaguzi tayari CCM imeishashinda kwa kupita bila kupingwa for more than 50%.

Hongera CCM!.
CCM Hoyee...
Malizia...
P
 
Moja kati ya kosa kubwa ambalo litamtafuna baba wa taifa huko alipo ni kutoruhusu chama mbadala kushika dola hata kwa muhula mmoja tu ili ccm ione jambo la kawaida kuwa wanaweza kuishi vizuri hata kama hawapo madarakani!!!Maani C.C.M inahisi kushindwa uchaguzi na chama kingine kushika dola ni ukoma au saratani ya kizazi isiyopona!!!Kama samaki kukosa maji!!!!
 
Vyama viko kibau mbona hamuandiki habari zao? Tabia ya kuandika habari za chama kimoja tu cha upinzani inafanya waandishi waonekane vibaraka wa ccm.

Habari za chama kimoja tu siku zote hadi inakuwa "Routine and Monotonous". Acheni ukanjanja andikeni habari ya vyama vingine pia ili pia tuvifahamu. Sasa nchi utafikiri chama ni kimoja tu. This is very silly and rather bore some. Please we're fed up.
Mkuu Nyanjomigire, pole, hatuandiki kuhusu chama kimoja tuu, na huu sio tuu ni mfano hao, mwandishi wa hoja kama hii, anaweza kuwa kibaraka wa CCM?.

P.
 
Wanabodi.

Naendelea na zile makala zangu za Kwa Maslahi ya Taifa, zinazotoka kila siku ya Jumatatu kwenye gazeti la Raia Mwema, hili likiwa ni bandiko mwendelezo wa Licha ya CCM kuwa chanzo cha umasikini, ujinga, rushwa na ufisadi, kwanini CCM bado huwa inashinda chaguzi mbalimbali?

Leo naanzia nilipoishia wiki iliyopita, nikiendeleza Makala zangu elimishi Kwa Maslahi ya Taifa, nikizungumzia mambo mbalimbali ya taifa letu. Leo nikiendelea kueleza kwa nini, licha ya kuwa CCM ndio chanzo cha umasikini wa taifa hili kwa kudumaza maendeleo, CCM ndio chanzo cha rushwa na ufisadi uliotamalaki kwenye taifa letu, CCM ndio iliyowekeza kwa kuendeleza ujinga kwa Watanzania kwa miaka yote hiyo. Licha ya hayo yote, lakini bado ni CCM imeendelea kushinda ushindi wa jumla katika chaguzi mbalimbali hata baada ya Tanzania kuanzisha mfumo wa vyama vingi zaidi ya miaka 25 iliyopita.

Tumefanya chaguzi kuu 5 za vyama vingi, 1995, 2000, 2005, 2010, 2015 na zote CCM imekuwa ikiibuka mshindi, jee kushinda huku kwa CCM, ni kwa sababu CCM inakubalika sana kwa kuwaletea Watanzania maendeleo?, CCM inashinda kwa kukosekana kwa upinzani imara na madhubuti?, au CCM inashinda kwa sababu ya mazoea tuu na ujinga wa Watanzania, kutokana na elimu duni ya mpiga kura, na umasikini, uliotopea, hivyo wapiga kura wengi wa Tanzania kujikuta hawana uwezo wa kufanya informed decision?.

Tanzania tulipoingia mfumo wa vyama vingi, tuliuparamia tuu, bila kujiandaa kimawazo, kimifumo na kisheria, kuwa nchi ya vyama vingi, hivyo tumeingia kuwa nchi ya vyama vingi, kwa kubadili tuu katiba, bila kubadili mifumo, sheria na mitazamo, matokeo yake, tumeanzisha vyama vingi ndani ya set up ya mfumo wa chama kimoja, huku CCM kikiendelea kuwa chama dola CCM, na vyama vingine vikaanzishwa kushindana na chama dola.

1. Hoja ya kwanza, ni kutoka kwa wana CCM wenyewe kuwa CCM inashinda kwa sababu CCM ndicho chama pekee kilichotapakaa nchi nzima hadi vijijini, na kinapendwa na Watanzania, na kimekubalika kwa kuwaletea Watanzania maendeleo, nitaeleza kidogo kupendwa huku kwa CCM ni kupendwa gani, na hayo maendeleo CCM iliyoyaleta ni maendeleo gani.

2. Lakini sababu halisi ya CCM kuendelea kushinda chaguzi mbali mbali kwa mtizamo wangu, sio kwa sababu CCM inapendwa sana na inakubalika sana kwa kuwaletea Watanzania maendeo, (maendeleo gani?), bali CCM inashinda na kuendelea kushinda kwa sababu, Tanzania bado tuko kwenye setup ya mfumo wa Chama kimoja, na CCM bado ni chama dola, chama bado ndio kimeshika hatamu za uongozi wa nchi hii, hivyo bila kubadili setup ya mfumo wa chama kimoja na kwenda kwenye setup ya mfumo wa vyama vingi, iliwemo kukiondoa chama dola kwenye mindset ya Watanzania, CCM itaendelea kushinda na kutawala nchi hii kwa miaka mingi ijayo, in fact, CCM itatawala milele!.

3. CCM ni chama tajiri, ambapo kimeanzishwa kwa kupora mali za Watanzania. Tulipoanzisha vyama vingi ilibidi CCM kivunjwe kwanza, na zile mali za CCM, zilizotokana na michango ya lazima ya Watanzania wote, yakiwemo majengo ya serikali, viwanja vya umma ambavyo CCM ilivimiliki wakati wa mfumo wa Chama kimoja, vilipaswa virudishwe serikalini na kuwa mali ya umma, CCM ianze moja kwa mali zake halali tuu, kama vyama vingine, lakini kitendo cha CCM kusajiliwa hivyo hivyo kilivyo na ukwasi mkubwa wa loot ya Watanzania, hakuna Chama cha kushindana na CCM na kuingia ikulu!.

4. Mind set ya vyombo vyote vya kiutendaji na kiutawala, iko ki CCM CCM tuu, kuanzia Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, vyombo vya dola, na watendaji wa vyombo vingine vyote vya kiutendaji, akiwemo Msajili wa vyama vya Siasa, wote wako ki CCM, CCM!. Mimi sisemi kuwa NEC sio tume huru, NEC ni Tume Huru ila sio inclusive. Japo uchaguzi unaendeshwa kwa mujibu wa sheria taratibu na kanuni za tume huru, lakini kwa vile NEC kuanzia Mwenyekiti wake, Mkurugenzi, makamishna, na wakurugenzi wote wa halmashauri ambao ndio wasimamizi wa uchaguzi, wanateuliwa na Mwenyekiti wa chama kimoja wapo, kuna uwezekano akateua makada watupu wa CCM, hivyo zoezi la uchaguzi kuendeshwa kwa ukada ukada zaidi kuliko utendaji ndio maana kuna watu wa chama kimoja wanapewa barua za utambulisho, watu wa chama kingine wananyimwa!. Kama mtu kama Jaji Mkuu wa Tanzania, anakwenda kugombea urais CCM, au CDF mstaafu!, hii maana yake hawa ni makada!. Kinachotakiwa kufanyika ni kubadili set up ya NEC iwe inclusive na kubadili sheria ya uchunguzi kipengele cha wasimamizi wa uchaguzi wasiwe makada, watafutwe watu waadilifu ambao ni neutral kabisa kuongoza NEC, na Ofisi ya Msajili wa vyama, na makamisha kufanyike ushirikishwa wa wadau katika composition yao, nafasi za usimamizi wa uchaguzi zitangazwe wenye sifa waombe na sio makada wateuliwa na mmoja wa wagombea ili neutrality sio tuu ionekane bali kuonekana ikitendeka. Pia tubadili sheria zetu za uchaguzi ziwe za haki.

5. CCM imejikita Vijijini, Wapinzani Wamejikita mijini, kutokana na ukongwe wa CCM ambacho kilikuwa chama dola kilichoenea nchi nzima kwa mujibu wa sheria, kuanzia wajumbe wa nyumba kumi, mashina, matawi nchi wamesambaa nchi nzima, kutokana na utajiri wa CCM, CCM ndicho chama pekee chenye uwezo wa kuwa na ofisi nchi mzima, tena sio ofisi moja, bali ni ofisi nne kwenye baadhi ya maeneo, ofisi ya CCM, ofisi ya UVCC, ofisi ya UWT, na ofisi ya Jumuiya ya Wazazi, ambako kote huko kuna maofisa wanaolipwa mishahara, wakati ofisi za vyama vya upinzani ni watu wanajitolea nyumba zao na wanavitumikia vyama hivyo kwa mapenzi yao tuu bila kulipwa chochote!, hivyo chochote ambacho CCM inakipanga kinawafikia wananchi wa chini, na wakati wa kampeni, kama CCM inawadanganya Watanzania, ni wengi zaidi watadanganyika, kwa sababu CCM imewafikia, lakini akitokea mpinzani kusema ukweli, ukweli huu huishia mijini tuu, hivyo kwa mazingira haya, huwezi kushindana na CCM.

6. Ujinga wa Watanzania, tangu tumeanzisha mfumo wa vyama vingi, hakujawahi kutoa elimu yoyote ya uraia, kuwaelimisha Watanzania umuhimu wa uwepo wa vyama vingi, hivyo waliowengi wamedanganywa kuwa vyama vya upinzani vinakuja kuharibu umoja wetu kuleta fujo na kuhatarisha amani yetu na utulivu, sasa ukiwasikia viongozi wa upinzani wanavyoongea kwa jazba, na vyama vyenyewe ni vya kiharakati, vingine na sare za kijeshi jeshi, Watanzania wapenda amani, wanaogopa kuviamini. Ingetolewa elimu rasmi ya uraia na kuwafikia Watanzania wote, na Tanzania ikawa na vyama serious vya upinzani wa kweli, na Watanzania wakaelimishwa jinsi CCM ndio chanzo cha umasikini huu, ujinga huu, rushwa hii na ufisadi huu, siku nyingi CCM ingeisha pumzishwa kwa amani!, hakuna mtu yoyote anayependa kula mboga moja siku zote!, Watanzania wangependa sana kubadili mboga, tatizo ni hakuna hata hiyo mboga ya kubadilisha!.

7. Umasikini uliotopea, ambao pia pia unakwenda sambamba na ujinga. Mtu masikini wa kipato, chakula cha shida, mlo mmoja kwa siku, anaishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku, akili yake pia inadumaa. Mtu kama huyu shida yake ni mlo, na mavazi, sasa akiletewa ile Tshirt na kofia, na pilau ya siku moja, inatosha kabisa kukichagua chama kilichokulisha na kukuvisha, anakuwa hana uwezo kusikiliza sera na kufanya informed decisions, angalieni maeneo yenye umasikini uliotopea na elimu duni ndio strong holds za CCM. Mikoa yenye ehueni kiuchumi kama Arusha, Kilimanjaro, Bukoba, Iringa, Mbeya. Tanga na maeneo ya mijini, watu walioelimika, kidogo wanaweza kuchagua upinzani, lakini mikoa yenye umasikini wa kutupa kama Dodoma, etc, usitegemee upinzani unaweza kushinda!, shida ya masikini ni njaa tuu, CCM ndicho chama kinachoongoza kwa kugawa rushwa, ushahidi wa kazi nzuri iliyofanywa na fedha za Kagoda upo!. Hivyo CCM kuutumia umasikini wa Watanzania na Ujinga wa Watanzania kama mtaji wake wa Ushindi.

8. CCM inaendelea kushinda kwa sababu, uwanja wetu wa mashindano ya siasa ni uwanja tenge ambao umelalia upande wa CCM, ni kama kugombea kisu cha makali kuwili, halafu mgombea mmoja ameshika kwenye mpini, na mwingine kwenye makali. Vyombo vyote vinaipendelea CCM, kuanzia mfumo uliopo, Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, vyombo vya dola, huku mgombea mmoja mwenye ving'ora na kila kitu, JWTZ, Polisi, ukwasi mkubwa, ameishika dola na kuitoa igombewe na wengine wasio na kitu kabisa!.

9. CCM inaendelea kushinda kwa sababu Tanzania bado hatuna upinzani Imara, huu upinzani uliopo sasa ni upinzani uchwala, upinzani lege lege, hivyo kamwe hauwezi kushinda kushika dola hivi hivi ulivyo. Mimi nakubaliana kabisa na hoja ya Baba wa Taifa kuwa upinzani wa kweli utatoka CCM!, huu upinzani dhaifu uliopo sasa, na utitiri wa vyama, vyama vya kiharakati, hauwezi kuwapeka wapinzani ikulu. Kujiengua kwa Lowassa kutoka CCM ile 2015, na kujiunga upinzani, ndiko kulikoupatia upinzani mafanikio makubwa kabisa katika upinzani nchini Tanzania, tangu kuanza kwa mfumo wa vyama vingi, ingekuwa sio hali ya afya ya Lowassa, wafuasi wake na wale wote wenye Imani na Lowassa wangemfuata!, CCM ingepigwa chini!. Kama kwa hali ile tuu alivyo, ameweza kuvuna kura milioni 6, ambazo ni nyingi kuliko zilizomrudisha Kikwete ile 2010, tena kwa taarifa tuu, kwa upande wa Zanzibar, Lowassa ndio aliyepata kura nyingi kuliko Magufuli, kwa mujibu wa matokeo ya NEC, hivyo Zanzibar CCM ilipigwa chini!, hivyo kama Lowassa angekuwa fiti kabisa kiafya na hana mazongezonge ya ufisadi, amini usiamini, CCM ingepigwa chini ile 2015.

10. Wapinzani hawana sera, wala hawajui wanatakiwa kufanya nini, upinzani wa kweli, unapaswa kuonyesha sera mbadala na CCM, mfano sera ya elimu ya CCM ni elimu bure kutoka darasa la kwanza hadi kidato cha nne, upinzani wao wakasema sera yao ni elimu bure toka chekechea hadi chuo kikuu. Hapa wangekuwa ni wapinzani makini, sera hii tuu ingetosha kuipiga chini CCM!. Au sera ya Afya bure. Wapinzani hawakupaswa kuishia kusema maneno matupu tuu ya elimu bure hadi chuo kikuu, walipaswa kuja na roadmap ya how?. Wangewaeleza Watanzania watabana wapi matumizi ili kupata kupata fedha za kugharimia elimu bure, kwa kuainisha ufisadi wa serikali ya CCM, mfano kusema utaunda baraza dogo tuu la mawaziri lenye wizara 10, hizi zitaokoa kiasi hiki ambacho kitapelekwa kwenye elimu. Au kujumlisha jumla ya fedha zote zilizofujwa na CCM kwenye ufisadi wa EPA, Deep Green, Meremeta, Escrow, etc na kuonyesha jinsi ambavyo zingetumika kugharimia afya na elimu bure, ili kuwapa Watanzania chaguo mbadala!.

Wasalaam

Nawatakia Furahi Dei Njema.

Paskali






Mada yako Ni Moto unaounguza,nasikitika watu wa ajabu Kama mtu anejiita Mzee Mwanakijiji na Pascal Mayala wangekua na wao walimsikia Bashiri Ali Katibu Mkuu wa CCM alipokua akiyatamka hayo kwa kinywa chake.Lakini bahati mbaya hawakumsikia.
Huwa ananikumbushia sana Pascal Mayalla , wamefanana sana uandishi nk.
Pascal Mayala hawezi kuja kwa uzi huu na yule mtu Mwanakijiji.

Mzee Mwanakijiji pamoja na Pascal Mayalla , hata mimi kiukweli wamenishangaza sana. The latter yeye ni muumini wa ccm kutawala milele na rais kuongezewa muda! Tena yeye ana wish kwamba baada ya Maghufuli ni zamu ya Makonda!!

The former yeye ameshangaza sana kwasababu pamoja na kwamba ni mwandishi na mtu ambaye amekuwa akijinadi kwamba ni mtu mwenye kupenda mijadala ya hoja badala ya viroja, usemi ambao yeye ndiye aliyeufanya kuwa maarufu humu, ndiye sasa amekuwa champion wa viroja! Ni kweli kabisa humu JF ungekuta yeye ndo mwenye thread ya nguvu kuhusiana na haya yanayoendelea. Anaishi marekani na anafahamu umuhimu wa midahalo na uwezo wa viongozi kujenga hoja ulivyokuwa muhimu mbele ya wapiga kura! Halafu sidhani kama alishawahi hata kulaani ya member mwenzetu humu, ndugu yetu na comrade wetu Ben Saanane. Sijawahi kumsikia akipingana na ukandamizaji wa habari, uvunjwaji wa katiba na mengineyo mengi.

Kweli kuishi kwingi ni kuona mengi. Leo hii Mwanakijiji ni muumini wa ccm!!🤦🏾‍♂️
Hii ni sawa tu na kuyabugia matapishi yako ukijiaminisha ni mlo wa ukweli!
Pascal Mayalla hawezi kuleta pua hapa. Hana hoja ya kuweza kupambana. Atakuja na hoja gani? Na wakati yeye mwenyewe yuko kwenye mission? Ni mwandishi ambaye hata ushirikiano wake na waandishi wenzake una utata. Mfano nchi za wenzetu, wana habari wanashirikiana sana inapokuja kwenye maslahi ya kazi zao, hata kama wana mitazamo ya tofauti.
Wengi wenu ndio mmefunguliwa macho na Dr. Bashiru, angalie akina sisi hili tuliliona lini na tukalizungumza, hivyo hakuna kipya Dr. Bashiru alichozungumza, only to confirm something that was already there and already known.
P
 
Back
Top Bottom