Kwani serikali ya Tanzania inalazimisha lugha ya kufundishia elimu ya awali na msingi iwe Kiswahili

live on

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
851
1,353
Hili swali Huwa najiuliza sana alafu sipati majibu
Hivi ni kweli hawa viongozi wa serikali hawajui magumu wanayopitia watoto pale wanapoingia kidato Cha kwanza na kukuta lugha imebadirika ghafla?

Hivi ni kweli hawa viongozi wa serikali hawajui umuhimu wa lugha ya kingereza ndani ya nchi yetu na nje ya nchi yetu ?

Hivi ni kweli hawaoni tofauti kati ya mtoto aliyetumia lugha ya kiswahili darasa la kwanza Hadi darasa la saba na mtoto aliyesoma English medium pale watoto hawa wanapokutana kidato Cha kwanza?

Kwani mawaziri. Makatibu wakuu, wakuu wa mikoa na wakurugenzi mbali mbali wanawasomesha watoto wao EM badala ya Kayamba wakati wao ndio waliotunga na kuisimamia sera ya kuwa kiswahili ndio iwe lugha ya kufundishia elimu ya awali na msingi ?

Hapa Kuna Siri iliyokificha nyuma ya pazia watanzania amkeni

Kwa sababu nakumbuka kipindi hakuna EM za private serikali walikuwa na za kwao Kwa hapa Dar ni Olympiyo na Bunge na kipindi hicho asilimia 90 ya waliosoma hizi shule walikuwa ni watoto wa mawaziri na viongizi wengine

Kwahiyo sio kama hawajui umuhimu wa lugha ya kufundishia elimu ya awali na msingi iwe kingereza ila tu wanawapumbaza watanzania walio wenge kuwa eti watoto wao kutumia kiswahili shule za awali na msingi ndio kudumisha uzalendo
 
Watoto wa siku hizi uzembe unachangia sana. Kizazi chetu kurudi nyuma na hakukuwa na internet,TV wala nini mbona tuligonga shule kwa English na mambo yalienda na watu walitoboa?

Me nadhani madogo wa sasa uzembe ni mwingi,wanatazama sana contents za kutafsiriwa,hawasomi vitabu na kujifunza lugha. Hao wachina tu kwa mfano,wanapata shida sana kutoboa kibiashara kimataifa sababu ya lugha mbovu ya English na sasa wanapambana kujifunza English ili waweze kutoboa kiuchumi zaidi ya sasa.
 
Jiulize wachina wanatima kichina warisi kirusi wajerumani warussia usiwe mtumwa wa lugha ya kikoloni
 
Jiulize wachina wanatima kichina warisi kirusi wajerumani warussia usiwe mtumwa wa lugha ya kikoloni
Una umri gani mkuu? Au ndio matokeo ya kusoma Kiswahili yamekupofusha? Mnajikuta wazalendo halafu uzalendo mnaoupigania ni uchwara.

Lugha haipo kwa ajili ya umbeya na kuchambana tu. Lugha inatakiwa iwe imepevuka kitamaduni,kisayansi na teknolojia.

Nenda kwenye sayansi na teknolojia halafu uone Kiswahili ni dhaifu kiasi gani! Unavyosema kirusi na kichina hizo pia tayari ni lugha zilizojitosheleza kwenye hiyo angle.
 
Fatilia misamiati yote ipo…ni utayar tu ndo haupo.
Mkuu hoja ni kukubalika sio kuwepo! Kiswahili kinamisamiati mingi ambayo jamii imeshindwa kuitumia either kwa ugumu wake or lugha nyingine kuwa na misamiati rahisi. Mfano mtanzania wa ndanindani huko ukimuuliza keyboard ni nini anaweza kukujibu tofauti na ukimuuliza baobonye ni kitu gani! Kwanza atakushanga
 
Jiulize wachina wanatima kichina warisi kirusi wajerumani warussia usiwe mtumwa wa lugha ya kikoloni
Tayari Tanzania ni watumwa wa lugha ya kingereza na ndio maana ofisi zote za serikali documents zake zipo Kwa lugha ya kingereza

Alafu wewe unaonekana ni kilaza ndio hayo tunayoyasema hizo nchi ulizozitaja hapo mfumo wao wa Elimu ni Kwa lugha yao kuanzia elimu ya awali Hadi chuo kikuu

Kwanini na sisi tusichague Moja kama ni kiswahili basi iwe ndio lugha ya kufundishia kuanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu na kima tukichagua kingereza pia iwe hivyo kuanzia elimu ya awali hadi chuo kikuu

Kama wao kiswahili wanaona ni lugha muhimu kwanini hawataki kitumike secondary na Chuo kikuu?

Na kama wanaona kingereza ni lugha muhimu kwanini hawataki itumike kufundishia kuanzia elimu ya awali na msingi ?
 
Hata mim hili huwa linanishangaza sana,afu ukisema kuna wajinga humu wanakuja na porojo zao za kuwa sjui taifa gani na gani liliendelea kwa kutumia lugha yao,

Kiswahili pia ni moja ya kitu kinacholeta umaskin tz

Ukiachana na lugha kuna baadhi ya mambo ukiyaona ni kama ni madogo lakin serikali unakuta inashindwa kuyafanyia mabadiliko,mfano kuna sheria ya ndoa inaruhusu watoto kuolewa lakin mpaka leo hawairekebish
 
Jiulize wachina wanatima kichina warisi kirusi wajerumani warussia usiwe mtumwa wa lugha ya kikoloni
Kiswahili kinajitosheleza? Hao unaowasema lugha zao zinajitosheleza kuanzia vitabu, walimu, maabara, nk.

Leo unamfundisha mtoto kwa kiswahili kuanzia I hadi VII then sekondari kiingereza, una akili kweli wewe?
 
Lazima akushangae Kwa sababu hilo neno BAOBONYE sio msamiati wa lugha ya kiswahili ila Kuna mtu alikaa Kwa kutumia akili zake akabuni hilo jina
Misamiati ya lugha haibuniwi na watu ila Huwa ipo automatically tokea zamani
 
Lazima akushangae Kwa sababu hilo neno BAOBONYE sio msamiati wa lugha ya kiswahili ila Kuna mtu alikaa Kwa kutumia akili zake akabuni hilo jina
Misamiati ya lugha haibuniwi na watu ila Huwa ipo automatically tokea zamani
Ndio maana kwenye defn unakutana na neno "kukubalika", sasa maneno mengi ya kisayansi na teknolojia kwenye kiswahili ni yakihuni huni tu. Ccm wanajua mtaji wao ni watu wasio na exposure. Wanachofanya ni makusudi wala sio kwa bahati mbaya ndio maana unakuta mtoto wa Mwigulu yupo pale Feza
 
Kwakweli inasikitisha sana tena hivi Sasa ndio Kuna hizi shule zao secondary za kata wanawajaza watoto huko waliyotoka shule za kayumba wanakutana na kingereza wakati akiwa anapambana na kingereza mtihani wa kidato Cha nne huo anachukua division four yake au zero anarudi nyumbani anakuwa hana tofauti yoyote na aliyeishia darasa la saba

Mwisho wa siku aliyesoma kayumba anabaki kuwa kayumba tu

Watanzania wananyanyaswa sana na serikali yao

Wakija kwenu wanakuambieni hakuna umuhimu wa watoto wenu wasome Kwa lugha ya kingereza elimu ya awali na msingi

Wakirudi majumbani kwao wanachukua watoto wao wanawapeleka wakasome elimu ya awali na msingi Kwa lugha ya kingereza

Kwahiyo watanzania mlio wengi mnadumaa nyinyi na vizazi vyenu alafu wao na vizazi vyao wanakuwa active
 
Ninakumbuka nilipokwenda form one nilipata shida sana. anyway hapa mwalimu alikosea sana. Hii pia imesababisha kuwa na diaspora wachache sana ukilinganisha na nchi kama Kenya, Zimbabwe na ziginezo. Inakuwa ngumu sana tunapokuwa nje kuzungumza kiingereza fasha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…