Kwangu hili ni ajabu la Mwaka; Raisi kutolipa kodi

Waanze kulipa kodi maana hakuna namna nyingine, hii ni ukwepaji kodi kwa kutumia katiba na sheria sio fair

Watu kama nyie mna shida sana, nchi haiwezi kuwa nchi bila katiba na sheria, halafu watu ahao aho wanaolalamikia demokrasia wanataka sheria ivunjwe, kwa nini wasishughulikie au wasusie bunge kutaka sheria irekebishwe wao wanataka tu sheria ivunjwe? Kodi haiwi kodi mpaka sheria iseme, mengine ni michango tu kama ya harusi
 
Sheria mtunge wenyewe hapo mjengoni afu povu liwatoke wenyewe...its simple, kama mnataka alipe kodi basi badilisheni sheria...narrow and shallow-minded wabunge
Sheria inasema wasilipe kodi. Sasa mbona anataka wenzake walipe na yeye asilipe huoni yeye ndiye anavunja sheria aliyoapa kuilinda tena kwa kujinufaisha? Walipe wote
 
Yapo maajabu mengi hapa Tanzania,husasani katika sia lakini kwangu hili ni ajabu la mwaka.Na ajabu hili linaleta picha kwamba kuna watu hawana aibu kabisa aisee.Hivi unawezaje kumsimama kwenye TV kila dakika kadhaa ukihamasisha Watanzania kulipa kodi kwa maendeleo yao na Wewe hulipi kodi kwenye mshahara wako?Inashangaza kwa kweli.Inasemwa katiba ndo imeweka hivyo,hivi katiba ikivunjwa kwenye hili si ni USHUJAA.Mbona haki ya kujieleza kikatiba imefunjwa nk nk......
Hivi akivunja sheria na kutengua katiba na kuanza kujilipa fedha utakubali? Si unataka avunje sheria?
 
Umemtukana Raia Wa Kwanza. Andaa Mil 7!
Kama kusema ukweli napo ni matusi, hii itakuwa sio Tanzaniatena bali ni Korea Kaskazini ambako huruhusiwi kulitaja jina la Kiongozi Mkuu katika karahisho, jinale hutajwa kwenye kusifu tu.
 
Nashauri Pale alipojinyea mgombea urais mwaka Jana wajenge mnara Wa kumbukumbu.
Mjinga wa kiwango cha juu kabisa! Watu wanajadili hoja za maana na zenye tija kwa ustawi wa taifa wewe unaandika upuuzi. Kwa vyovyote utaku ni kilaza product. Ficha ujinga wako na wa familia yako iliyopoteza pesa zao kukusomesha kilaza wewe! Laiti wangalijua hizo pesa ni bora wangetoa sadaka.
 
Sheria inasema wasilipe kodi. Sasa mbona anataka wenzake walipe na yeye asilipe huoni yeye ndiye anavunja sheria aliyoapa kuilinda tena kwa kujinufaisha? Walipe wote
Mkuu, unajua sheria zetu huwa zinatengenezwa kiushabiki bila kuangalia uhalisia. Ukiwauliza waliokuwepo wakati sheria ikitungwa wakueleze sababu za kubagua watanzania kwa kigezo cha kodi hakuna atakayekua jibu stahiki. Yawezekana zilikuwepo sababu lakini ni sababu lakini kwa sasa ni hafifu na zimepitwa na wakati, ni wasaa muafaka wa kuitazama upya hiyo sheria ili kila mtanzania alipe kodi.
 
Yapo maajabu mengi hapa Tanzania,husasani katika sia lakini kwangu hili ni ajabu la mwaka.Na ajabu hili linaleta picha kwamba kuna watu hawana aibu kabisa aisee.Hivi unawezaje kumsimama kwenye TV kila dakika kadhaa ukihamasisha Watanzania kulipa kodi kwa maendeleo yao na Wewe hulipi kodi kwenye mshahara wako?Inashangaza kwa kweli.Inasemwa katiba ndo imeweka hivyo,hivi katiba ikivunjwa kwenye hili si ni USHUJAA.Mbona haki ya kujieleza kikatiba imefunjwa nk nk......
MKUU KISHERIA RAIS HAPASWI KULIPA KODI DUNIANI KOTE IKO HIVYO KWA SABABU KUU MOJA YA KISHERIA, KWA MUJIBU WA SHERIA YA KODI MKUSANYAJI MKUU WA KODI (HEAD OF TAX COLLECTOR) NI RAIS SO KUMWAMBIA ALIPE KODI NI SAWA NA KUINGIZA HELA MFUKO WA KUSHOTO THEN UKATOLEA HELA HIO HIO MFUKO WA KULIA
 
Umemtukana Raia Wa Kwanza. Andaa Mil 7!
Nafikiri OKW Boban Sunzu Ametoa maoni yake kwa moyo wa kizalendo sana. Atakayemshitaki anishitaki na mimi kwa makosa ya kumuunga mkono. Hebu fikiri tena kwa makini: Hata kama huyo unayemuita raia namba 1 alirekodiwa mara moja tu, walipa kodi ambao wengi wao ni walala hoi wanaona picha yake na kusikia sauti yake ikihimiza watu kuwa wazalendo na walipe kodi kwa uaminifu. Hebu tafakari kwa kina watu hao hao walala hoi wajue pia kuwa mhamasishaji wa "kujifunza kulipa kodi" na kulipa kodi yeye mwenyewe halipi eti kwa sababu katiba inasema hivyo. Walioapa kulinda katiba wameivunja katiba hiyo mara ngapi?? Hicho kipengele kinachomfanya mkuu wa kaya awe juu ya sheria ya kodi kivunjwe, na mwenye uwezo huo ni mkuu mwenyewe!
 
Yapo maajabu mengi hapa Tanzania,husasani katika sia lakini kwangu hili ni ajabu la mwaka.Na ajabu hili linaleta picha kwamba kuna watu hawana aibu kabisa aisee.Hivi unawezaje kumsimama kwenye TV kila dakika kadhaa ukihamasisha Watanzania kulipa kodi kwa maendeleo yao na Wewe hulipi kodi kwenye mshahara wako?Inashangaza kwa kweli.Inasemwa katiba ndo imeweka hivyo,hivi katiba ikivunjwa kwenye hili si ni USHUJAA.Mbona haki ya kujieleza kikatiba imefunjwa nk nk......
Kwa sisi masukuma ukiisha anza kucheza ngoma, zile za wagoyangi, wanunguli, wagobogobo, kila kitu kinakua ni utani tu. Hakuna hoja isiyo na utani,au kuchomekea. Itatuchukua muda sana kua serious kujenga hoja bila utani. Hayo ni matokeo ya kucheza ngoma.
 
Back
Top Bottom