KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,780
- 4,942
Mhe.Rais wa JMT,
Mhe.Waziri wa TAMISEMI
Nawapongeza kwa jitihada zenu katika kutengeneza na kutoa fursa za ajira nyingi sana katika kada ya ualimu na Afya. Ni ishara njema katika kupunguza tatizo la ajira nchini.
Mhe. Waziri wa TAMISEMI, maoni na mapendekezo haya ni kwa ajili ya ofisi yako ikiwa kama ofisi inayoratibu mchakato wa ajira za ualimu na Afya zilizotangazwa hivi karibuni. Maoni yangu yatasimamia katika mchakato wa kuomba mpaka kupangiwa vituo.
Ni ukweli usiopingika ,usaili au mtihani ni moja ya njia nzuri ya kupata watu walio bora na usaili ni moja ya mchakato muhimu katika ajira.
Hali imekuwa tofauti kwa ajira za TAMISEMI, labda pengine kutokana na wingi wa wanaoomba au kuwapunguzia gharama waombaji ,usaili au mitihani huwa sioni ikifanyika. Je, mna uhakika gani mliyepatia ajira ni bora kuliko mliyemuacha?
Utaratibu huu wa kuchuja na Kuwapatia ajira bila kuwepo usaili au mitihani lazima utaingiwa na dosari za upendeleo na kupatikana kwa watu wasio na sifa na wenye sifa kuachwa.
Ni vema utaratibu ukabadilishwa ili kutoa fursa sawa kwa waombaji na uangaliwe utaratibu wa kuwafanyia walau "ONLINE APTITUDE TEST" waombaji utazamwe. Kila muombaji ashiriki kwenye test kwa walau hata ya somo moja la atakalofundisha.
Pia katika utaratibu huu wa ONLINE APTITUDE TEST sio lazima waombaji labda walioomba kufundisha' biology' wafanye test ya aina moja, ili kuepusha kupeana majibu au udanganyifu wanaweza kupewa test tofauti au kama ni test ya aina moja mpangilo wa maswali ubadilishwe baina ya waombaji.
Tutumie walau njia hii kuondoa upendeleo wa aina yoyote au lawama kwamba nilikosa huku nikiwa Nina sifa.
Matumaini maoni haya yatakuwa ni msaada katika upatikanaji wa watumishi bora na sahihi.
Ahsante.