Kwako Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla kuhusu sisi wafanyakazi wa Hospitali ya Ks

ecolizer baba

Member
Sep 29, 2010
88
310
Amani iwe kwenu wadau.

Ninaomba kupitia jukwaa hili nifikishe kilio chetu sisi Wafanyakazi wa hospitali ya Ks kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makala.

Naomba kuwasilisha hoja zifuatazo:

1. KUCHELEWESHEWA MISHAHARA: Uongozi wa hospitali ya Ks unatucheleweshea sana mishahara sisi watumishi wake. Yaani kwa mfano hadi muda huu bado hatujalipwa mishahara yetu ya mwezi wa pili na hakuna dalili za kulipwa!! Hadi tumeanza kutembea kwa mguu kwenda kazini na kurudi nyumbani. Na hii sio mara ya kwanza kufanyiwa hivi. Wenye hospitali wanachojali ni sisi kuhudumia wagonjwa wapate hela lakini kutujali sisi tunao fanya hizo hela zije hawafanyi hivyo. Tunaonekana si lolote na si chochote

2. MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII:
Hiki nacho kinatuumiza sana. Kwa utaratibu inatakiwa kila mwezi mwajiri awasilishe makato na malipo ya mafao ya waajiriwa wake kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii mfano PPD, LAPF, PSPF, NSSF n.k. Lakini kwetu sisi hakuna kitu kama hicho. Unakuta mtu amefanya kazi kwenye hospitali hii zaidi za miaka mitano na anakuja kuondoka hakuna hela yoyote iliyopelekwa kwenye mifuko hiyo. Kipindi fulani mwaka jana tulipolalamika waliwaleta watu wa NSSF wakatupiga picha na kututengenezea vitambulisho. Hii nilikuja baada ya kulalamika kwenye jukwaa hili. Kumbe ilikuwa geresha ili upepo upite. Hakuna hela yoyote iliyopelekwa huko. Kama imepelekwa labda ni ya mwezi mmoja au miwili.

3. KUFUKUZA WAFANYAKAZI BILA KUFUATA UTARATIBU.

Kuna baadhi ya Wafanyakazi wenzetu wamefukuzwa bila kufuata utaratibu. Yaani wakiona wewe unajifanya kufuatilia haki zako unafukuzwa. Maelekezo yanatolewa na Mkurugenzi(Mama mwenye hospitali) kwenda kwa Katibu halafu huyo Katibu anakutimua. Kibaya zaidi unatimuliwa bila kujua hatma ya Mafao yako kwa muda huo uliofanya kazi. Unaondoka hauna kitu!! Inauma sana.

4. HOSPITALI KUENDESHA BILA KUFUATA TARATIBU.

Hiki ni kichekesho kwa kweli. Yaani mwenye kauli kwenye kila kitu ni Mama mwenye hospitali ambaye ndiye Mkurugenzi. Mhasibu na Katibu hawana sauti hata kidogo. Wamewekwa pale kama rubber stamp. Yaani hata issue ya Hela Mhazini huwa anatengwa kabisa na hana mamlaka ya kufanya miamala yoyote. Yupo tu kama jina. Hata ikitokea dharura ipi na Mama mwenyewe hayuko hakuna malipo yatakayofanyika hadi mama arudi hata kama yuko nje ya nchi!!

Kwa hiyo tunamuomba sana mkuu wa Mkoa wetu Mh. Amos Makala aifuatilie hoja hizi kwa ukaribu vinginevyo sisi Wafanyakazi wa Ks hospitali tutaendelea kuumia.

Walioko karibu na Makala mfikishie kilio hiki. Asanteni.

--------------
Pia soma...
Hospitali binafsi ya Ks iliyoko mkoani Mbeya inawadhulumu watumishi wake. Tunaomba imulikwe

Wizara ya afya imulikeni hopitali ya KS iliyoko Mbeya
 
Amani iwe kwenu wadau.

Ninaomba kupitia jukwaa hili nifikishe kilio chetu sisi Wafanyakazi wa hospitali ya Ks kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Amos Makala.

Naomba kuwasilisha hoja zifuatazo:

1. KUCHELEWESHEWA MISHAHARA: Uongozi wa hospitali ya Ks unatucheleweshea sana mishahara sisi watumishi wake. Yaani kwa mfano hadi muda huu bado hatujalipwa mishahara yetu ya mwezi wa pili na hakuna dalili za kulipwa!! Hadi tumeanza kutembea kwa mguu kwenda kazini na kurudi nyumbani. Na hii sio mara ya kwanza kufanyiwa hivi. Wenye hospitali wanachojali ni sisi kuhudumia wagonjwa wapate hela lakini kutujali sisi tunao fanya hizo hela zije hawafanyi hivyo. Tunaonekana si lolote na si chochote

2. MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII:
Hiki nacho kinatuumiza sana. Kwa utaratibu inatakiwa kila mwezi mwajiri awasilishe makato na malipo ya mafao ya waajiriwa wake kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii mfano PPD, LAPF, PSPF, NSSF n.k. Lakini kwetu sisi hakuna kitu kama hicho. Unakuta mtu amefanya kazi kwenye hospitali hii zaidi za miaka mitano na anakuja kuondoka hakuna hela yoyote iliyopelekwa kwenye mifuko hiyo. Kipindi fulani mwaka jana tulipolalamika waliwaleta watu wa NSSF wakatupiga picha na kututengenezea vitambulisho. Hii nilikuja baada ya kulalamika kwenye jukwaa hili. Kumbe ilikuwa geresha ili upepo upite. Hakuna hela yoyote iliyopelekwa huko. Kama imepelekwa labda ni ya mwezi mmoja au miwili.

3. KUFUKUZA WAFANYAKAZI BILA KUFUATA UTARATIBU.

Kuna baadhi ya Wafanyakazi wenzetu wamefukuzwa bila kufuata utaratibu. Yaani wakiona wewe unajifanya kufuatilia haki zako unafukuzwa. Maelekezo yanatolewa na Mkurugenzi(Mama mwenye hospitali) kwenda kwa Katibu halafu huyo Katibu anakutimua. Kibaya zaidi unatimuliwa bila kujua hatma ya Mafao yako kwa muda huo uliofanya kazi. Unaondoka hauna kitu!! Inauma sana.

4. HOSPITALI KUENDESHA BILA KUFUATA TARATIBU.

Hiki ni kichekesho kwa kweli. Yaani mwenye kauli kwenye kila kitu ni Mama mwenye hospitali ambaye ndiye Mkurugenzi. Mhasibu na Katibu hawana sauti hata kidogo. Wamewekwa pale kama rubber stamp. Yaani hata issue ya Hela Mhazini huwa anatengwa kabisa na hana mamlaka ya kufanya miamala yoyote. Yupo tu kama jina. Hata ikitokea dharura ipi na Mama mwenyewe hayuko hakuna malipo yatakayofanyika hadi mama arudi hata kama yuko nje ya nchi!!

Kwa hiyo tunamuomba sana mkuu wa Mkoa wetu Mh. Amos Makala azifuatilie hoja hizi kwa ukaribu vinginevyo sisi Wafanyakazi wa Ks hospitali tutaendelea kuumia.

Walioko karibu na Mh. Makala mfikishieni kilio hiki. Asanteni.
 
Back
Top Bottom