Kwa wizi huu wa TANESCO, lazima tufike 1.9tr

Huo ni upotoshaji mkubwa, unless mleta mada aweke risiti ya malipo ili watu wajihakikishie. Kodi ya 50+% sijawahi kuiona.
Yawezekana jamaa alikuwa na madeni siku za nyuma hivyo hajachunguza vyema alichokatwa ni nini, vinginevyo atakuwa muongo na mzushi!
 
Ndugu Mzalendo Halisi
1. Gharama za huduma zipo kikatiba na kwa mujibu wa Sheria ya Bunge na nchi na si maamuzi ya TANESCO kupanga viwango vya Kodi na garama bali ni mdhibiti ambaye ni EWURA pamoja na mamlaka zingine husika kama TRA na si kweli kwamba ukinunua umeme wa elfu 40 unakatwa kodi ya shilingi 23,000 sawa na asilimia 57.5 kodi inayokatwa ni asilimia 18 Na zingine 3 kwaajili ya garama za umeme vijijini zinazoendelea za REA na EWURA asilimia 1 na SIYO asilimia 57.5 kama ulivyoainisha wewe hapo juu. Huo ni upotoshaji na kama hiyo token unayo tatizo lilikutokea ifikishe ofisi za Tanesco zilizo karibu yako utapatiwa msaada wa kushughulikia tatizo lako mara moja ama kupewa maelezo yaliyo sahihi.

2. KUHUSU SERVICE CHARGE/GARAMA YA HUDUMA ZA TANESCO; Gharama za Huduma ni gharama ambazo mteja analipa ili inapotokea TANESCO wanakuja mtaani kwenu kubadilisha nguzo iliyooza, kubadilisha waya uliokatika kwenye line ya mteja, kubadilisha mita yako ambayo ni mbovu, kukata matawi ya miti mtaani kwenu, kubadilisha transfoma iliyoibiwa mafuta au kuungua nk gharama hizo zifidiwe na michango hiyo ya "service charges" Ijulikane kwamba mfano waya, mita na nguzo ambazo mteja Ulilipia wakati unaingiziwa umeme kama zikiharibika, TANESCO wanakuja kukubadilishia bure. Je tufute "service charge" alafu nguzo ikianguka au mita kuharibika au ukitupigia emergency kuja nyumbani au mtaani kwako kutoa huduma tukucharge upya?
VIWANGO VYA "SERVICE CHARGE "
Wateja wote ambao hawazidishi unit 75 (D1) kwa mwezi hawalipi service charge. Na umeme wanauziwa TZS 100 kwa unit moja (Bila kodi). Ila ukizidisha unit. Kila unit utauziwa TZS 350.
Wateja wanaozidi unit 75 lakini hawavuki unit 7500 kwa mwezi (T1) wanalipa service charge ya TZS 5,520 na unit moja wanauziwa TZS 298 (Bila kodi). T2 na T3, ni kwa ajili ya wafanyabiashara, mahoteli, viwanda, migodi na wengine wanautumia umeme mwingi.
Kama una swali lolote tupigie 0800 780 800. Kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 11.00 jioni.
hayo unayosema yapo Kenya au wapi?:
 
Naona hili swali wahusika waliokuwa wamejitolea kuijibia TANESCO wameshindwa kulijibu.
Wafanyakazi wa Tanesco wanalipa sawa kama mteja yeyote anavyolopia umeme.hakuna upendeleo katika hili .Na kama huamini katika hili nenda Ewura kathibitishe.
Na kuhusu Service charge Tanesco wameiomba Ewura indolewe. Kwa maelezo zaidi tembelea Website ya Ewura
 
Ofisa wa TANESCO nikuambia huna unachokijua hukutaka kukubali. Umejitahidi kutulazimisha kuwa service charge ni mpingo usioweza kubadilika rangi sembuse kuukata. Leo Mkurugenzi wako ametangaza kuwa wameamua kuifuta service charge baada ya wananchi kupiga kelele. Na amini usiamini hata baada ya hapo, tutapiga kelele mpaka hata hiyo VAT ipunguzwe.
 
Unacholipia kuomba kuunganishiwa umeme ni gharama ya service line.

Mita haununui inabaki kuwa mali ya TANESCO sio mali ya mteja Adili.

Inakuwaje nitozwe service charge in perpetuity wakati nililipia nilipofungiwa?
 
Hapa kazi tu , mwananchi wa chini ni mtumwa wa leo - kazi kuwalisha wafanyakazi wa serikali na ufisadi na pia wafanya biashara
 
Back
Top Bottom