Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,284
- 23,253
Akili ya binadamu ni utajiri wenye nguvu zaidi kuliko tunavyoongozwa kuamini katika elimu rasmi ya kitaaluma tunapokuwa shuleni au chuoni.
Nachukia sana watu wanapochanganya akili na elimu. Unaweza kuwa na shahada na bado ukawa mjinga kwa kuamini unajua kila kitu!
Elimu inakuwa na manufaa zaidi kama inakuwezesha kutambua baada ya kumaliza shule kuwa bado unao uhitaji wa kujua zaidi hata kuliko awali.
Kiu ya uhitaji wa kujua zaidi unaitwa udadisi. Udadisi unachangiwa zaidi na akili kuliko elimu rasmi. Tofauti na elimu, akili huendana na hekima na busara!
Kwa Tanzania ya sasa udadisi, hekima na busara zinaogopwa kama ukoma. Taifa limetekwa, nguvu za hoja marufuku na hoja za nguzu ni za hewala bwana!
Udadisi hustawisha akili. Kwa bahati mbaya udadisii huweza kulemazwa na elimu rasmi na kuwa chanzo cha kuzorotesha umakini katika kuliendeleza taifa!
Tukumbuke pia kuwa elimu itakuwa na ufanisi zaidi kama itakuwezesha wewe mhitimu kutambua kwamba kiasi ambacho hujui ni maradufu ya unachojua.
Huu ndio msingi wa msemo wa heri kukaa kimya kuliko kuongea hovyo halafu mwisho wa usiku unakuta umetoa fursa kwa watu kupima uwezo wako kifikra (kiakili).
Akili sio chombo cha kujazwa kama elimu, hapana! Akili haijai bali ni kama tanuru la moto mkali ambao huchochewa na changamoto za maisha kitaifa.
Changamoto hizo zinaweza kuwa za kiutamaduni, kijamii, kiuchumi na kisiasa. Ukidumaa kiakili uwepo wako duniani unakuwa wa kimashaka mashaka.
Akili sio kutokufanya makosa yoyote wakati wowote, bali kuwa na uwezo wa kutambua haraka yalipo na kuyaboresha yawe bora zaidi na yenye manufaa Zaidi.
Tofauti na elimu, binadamu hahitaji cheti kwa kuwa na akili wala hajitangazi kuwa ana akili. Mwenye akili fikra zake ndizo hufundishwa kwa akili ndogo vyuoni.
Katika vyuo vyetu, wahitimu hupewa vyeti kwa kusoma, kukariri na kutenda mawazo ya wenye akili. Huo ndio mwisho wa uwezo wao na kutegemea zaidi ni kujidanganya!
Udadisi umekufa Tanzania, hatuna tena mapambano ya fikra ili kuweza kuchochea udadisi. Watu wale wale, fikra zile zile, CCM ile ile...CCM imehatamia kila kitu!
Hakika CCM imetufikisha pabaya. Tanzania ni ile ileeee!