Kwa wajuzi na wajuvi wa Kiswahili, nini Kiswahili cha haya maneno?

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
94,012
121,292
1. President-elect; kwa Kiswahili tafsiri yake ni Rais mteule.

Rais aliyechaguliwa anakuwaje rais mteule? Mteule si yule anayeteuliwa?

President - rais.

Elect-chagua/ chaguliwa.

Kwa nini huyo anayeitwa rais mteule asiitwe ‘Rais-mchaguliwa’, badala yake?

2. Nini Kiswahili cha haya maneno?
  • shule
  • chai
  • pesa.
  • redio
  • shati
 
nadhani ni kwasababu inatamkika kirahisi zaidi
 
Kiswahili cha maneno uliyoyataja ndicho hichohicho, si tumetohoa mazee!

Neno Raisi Mteule limekaa vibaya kama neno la kiingereza Criminal Lawyer. Mtu anaweza kuchanganya tafasiri kwamba either a lawyer is a criminal or a lawyer specializes in criminal law.​
 
Kiswahili kimeazima maneno mengi sana toka lugha zingine!

Hata ‘pilau’ ni neno ambalo limeazimwa.
 
1. President-elect; kwa Kiswahili tafsiri yake ni Rais mteule.

Rais aliyechaguliwa anakuwaje rais mteule? Mteule si yule anayeteuliwa?

President - rais.

Elect-chagua/ chaguliwa.

Kwa nini huyo anayeitwa rais mteule asiitwe ‘Rais-mchaguliwa’, badala yake?

2. Nini Kiswahili cha haya maneno?
  • shule
  • chai
  • pesa.
  • redio
  • shati
Nafkiri neno mteule limetumika kama upekee wa kuongeza maana ya umuhimu kwa kuzingatia vigezo vya kijamii zaidi. Maana ktk dini na Imani pamoja utapambana kuishika dini yako lakini maamuzi ya kuingia ktk pepo bado hayapo kwako. Yapo kwa Mola wako. Ndiyo maana ktk Imani na dini wanasema waitwao ni wengi wateule ni Wachache. Naamini kwa maana hiyo hiyo neno rais mteule limetumika kuonesha si iituhada za mgombea Bali ninkama bahati yeye kuwa pale.
Mawazo yangu.
Pia, kiswahili tulitafuta maneno yetu kujitofautisha tu na wengine. Ndiyo maana tuna msumbiji na afrika kusini. Ila hakuna nchi zinazotumia majina haya.
 
Mfano,

Mwanasheria mteule wa familia (ili asimamie mirathi ya Marehemu)

Hapo maana yake huyo Mwanasheria amechaguliwa na wana familia husika/Ameaminiwa ili awawakilishe kwenye mirathi.
Kuteuliwa ni kuwa appointed.

‘The family will appoint a lawyer to be the executor of the decedent’s will’.

‘Familia itamteua mwanasheria kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu’.
 
Kuteuliwa ni kuwa appointed.

‘The family will appoint a lawyer to be the executor of the decedent’s will’.

‘Familia itamteua mwanasheria kuwa msimamizi wa mirathi ya marehemu’.
Unateuliwa baada ya majadiliano ya wanafamilia na kukubaliana kisha ndio wanakuchagua/kukuteua wewe,

Huwezi ukateuliwa na watu wengi bali unachaguliwa,mtu mmoja ndio anaweza kuteua coz inakua ni amri yake yeye pekee na hakuna wa kumpinga.
 
Lugha zote zinaazima maneno.

Lugha ya kiingereza maneno yake ya asili ni 24% tu, mengine imeazima kutoka kwenye kifaransa, kilatini, kigiriki, kidenishi na kijerumani.​
Ni kweli!

Na ukweli huo ndo huivunja hoja ya wale wasmao kwamba eti Kiswahili hakijitoshelezi na ndo maana lugha ya Kiingereza bado inatumika kwenye sehemu kama mahakama.

Swali langu kwao, ni lugha gani/ ipi hapa duniani inayojitosheleza?
 
Back
Top Bottom