Kwa ufaulu huu kidato 6, 2023. Bila upanuzi vyuo vikuu ni Div one tu wataingia vyuo vikuu

Mm baada ya kuona dogo anayeshinda kwenye madubu amepata div 2 ya pcm nikaamua kutafuta papers za mitihani hiyo.

Nikakuta kwamba mwaka huu mtihani wa physics F6, definition tu ilipewa marks 5. Halafu hesabu za kidato cha 3 na 4 zilikuwemo nyingi.
Basi itoshe kusema kuna upanuzi wa goli. UDSM warudishe marticulation paper ili kuchuja watu.
 
Basi itoshe kusema kuna upanuzi wa goli. UDSM warudishe marticulation paper ili kuchuja watu.
Wakiwapa hiyo matriculation wasahihishe NECTA na walimu wao wa sekondari itapigwa tu. Tatizo ni msahihishaji na maelekezo tola kwammikiki.
 
Wakati nikiwa likizo nyumbani nilitembelewa na kijana mmoja aliyemaliza Form 6 akiwa na DIV2 akiniomba nimsaidie kupata chuo Marekani ninakofanyia kazi zangu. Nikamfanyia usaili wa haraka haraka wa Calculus na Physics nikamkuta ni mweupe kabisa. Inawezekana mitihani ya siku hizi inahusu maswali basic tu au ni maswali yaliyokwisha jirudia sana kiasi kuwa wanafunzi wanakuwa wanajiandaa kwa kutumia past papers tu bila kuwa na deep understanding ya subject matter.
Wanafundishwa kufaulu na sio kitu kingine
 
DR. Msonde enzi zake akiwa Katibu Mtendaji wa NECTA angesema matumizi ya vishikwambi kwa walimu yamechangia matokeo mazuri kwa vijana wetu mwaka huu. Yule alikuwa anajuwa kucheza na furusha akalamba unaibu Katibu Mkuu asubuhi tu mapema.
 
mitihani ilikuwa rahisi sana, ngoja nitafute papers hizo
Mkuu ni siasa chafu.
Watoto wana siri nzito.
Mimi kuna baadhi ya wanafunzi shule tofauti wamefunguka magumu...fanya kautafiti utathibitisha hili
 
Ila imenishangaza kusikia kuwa Hesabu imeongoza kwa ufaulu kidato cha sita au niseme masomo ya saiyansi ndio yameongoza. Nikawa najiuliza, ni ile ile mitihani ya PCB/M tulikuwa tunafanya sisi wahenga au kuna mabadiliko?
Hii nchi haiaminiki
 
Wakati nikiwa likizo nyumbani nilitembelewa na kijana mmoja aliyemaliza Form 6 akiwa na DIV2 akiniomba nimsaidie kupata chuo Marekani ninakofanyia kazi zangu. Nikamfanyia usaili wa haraka haraka wa Calculus na Physics nikamkuta ni mweupe kabisa. Inawezekana mitihani ya siku hizi inahusu maswali basic tu au ni maswali yaliyokwisha jirudia sana kiasi kuwa wanafunzi wanakuwa wanajiandaa kwa kutumia past papers tu bila kuwa na deep understanding ya subject matter.
Ni kweli, wametengenezewa mazingira ya kufaulu kiurahisi pia NECTA wanalegeza
 
Matokeo ya kidato cha sita 2023. Karibu shule zote daraja lenye idadi kubwa ya waliofanya vizuri ni daraja la kwanza ( Division one). Kwa matiki hiyo mambo yafuatayo yanaweza kujitokeza;

1. Kama vyuo vikuu vitachukua wanafunzi kulingana na uwezo wake kama miaka ya nyuma ni dhahili kuwa wanafunzi watakao ingia vyuo vikuu vyote vya umma na binafsi watakuwa waliofaulu kwa daraja la kwanza tu.
2. Kama vyuo vitalazimika kuongeza idadi ya wanafunzi pasipo kwenda sambamba na kuongeza miundo mbinu yake na kuajiri wahadhiri wengine hasa ukizingatia muda haitoshi kulingana na kuanza mwaka wa masomo Oktoba ni dhahili itasababisha kushuka kwa ubora wa elimu itakayotolewa.

3. Tutarajie shule za binafsi kuanza kukosa wanafunzi. Kwani kwa matokeo ya mwaka huu ufaulu umekuwa wa kufanana kwa shule zote, zile za vipaji maalumu, shule za binafsi na hata shule za bweni kawaida na zile za kata Zipo shule za bweni kawaida hazijatoa hata wanafunzi wa daraja la tatu au la pili kabisa. Kwa sababu hiyo wazazi hawataona sababu ya kuwapeleka watoto wao shule za kulipia wakati ufaulu hautofautiani na shule za bure za umma.

Ni wakati wa serikali kujipanga sasa na kukabiliana na ongezeko la ufaulu huu mkubwa kwa kuwa na mipango ya muda mrefu. Kwa mfano kuchelewesha wanafunzi wa kidato cha tano kufungua shule Julai kama ilivyozoeleka na kusongeza mpaka Agosti ni ushahidi wa waziri kuwa serikali haina mipango ya muda mrefu. Huu siyo wakati wa kujenga madarasa kwani walitakiwa kuelewa mapema kuhitajika kwa madarasa.

Wataalamu wao wa Chuo cha Mipango Dodoma wanatakiwa kutumika mapema kuepusha uzembe wa aina hii.
PIA MITIHANI INAVUJA SANA, UNAKUTA HADI GOVERNMENT SCHOOLS soft copy zinawafikia
 
PIA MITIHANI INAVUJA SANA, UNAKUTA HADI GOVERNMENT SCHOOLS soft copy zinawafikia
We hutaki ziwafikie
Acha watoto wafaulu tena wote wangetakiwa wapate div One

Viongozi wenyewe ndiyo hawa tulio nao!!! Acha watoto wafaulu tuu

Maisha ndiyo haya haya mafupiiiiii kama mkia wa mbuzi

Acha tupate raha ya watoto kufaulu tukate na keki huon shilole alivo furahi???

Nasemaje panueni goli zaidi watoto wafaulu

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Wakati nikiwa likizo nyumbani nilitembelewa na kijana mmoja aliyemaliza Form 6 akiwa na DIV2 akiniomba nimsaidie kupata chuo Marekani ninakofanyia kazi zangu. Nikamfanyia usaili wa haraka haraka wa Calculus na Physics nikamkuta ni mweupe kabisa. Inawezekana mitihani ya siku hizi inahusu maswali basic tu au ni maswali yaliyokwisha jirudia sana kiasi kuwa wanafunzi wanakuwa wanajiandaa kwa kutumia past papers tu bila kuwa na deep understanding ya subject matter.
Na hili ndio tatizo kubwa , watu wanajipanga kufaulu tu mitihani sio kuelewa masomo .
 
Siku hizi siasa zimeingia Kwenye elimu.

Walimu wanajazishws mafomu na CCM

Wakuu wa shule wanapigwa biti ole wao wafelishe wanapigwa chini.

Shule za private Wana BAJETI kabisa ya paperz

Cheating inahusika pia.

Mimi Kuna dogo mmoja namjua Wala Hana maajabu ila alipiga wani Kali sana tena six

Hii nchi Ina vituko Kila kona kumejaa vituko

Mara bandari iuzwe , mara hivi yaani ni shida!!!
 
Back
Top Bottom