Kwa Spika Job Ndugai: Busara na hekima inataka mambo mengine mzungumze na wabunge wenzako mkiwa ktk "off the media cameras"

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,951
12,537
Moja ya sifa ya mtu kamili na hususani kwa kiongozi wa umma kama alivyo Spika wa Bunge la JMT ndugu Job Ndugai, ni kutumia busara na hekima katika kufanya maamuzi yake iwe ni kwa kutamka kwa maneno au kwa kutenda kwa vitendo.

Leo asubuhi spika Job Ndugai ametamka pasipo umuhimu wala ulazima wowote kwamba, ni hatari kwa wabunge kutumia usafiri wa Bodaboda kwa sababu wao (hawa wabunge) wanapatikana kwa gharama kubwa.

Kiukweli nilipoisikia kauli hii toka ktk kinywa cha kiongozi huyu mkuu wa umma, nilishtuka sana.

Sekta hii rasmi ya usafirishaji imeajiri watu maelfu kwa maelfu Tanzania nzima na wa rika na elimu zote na kuendesha maisha yao vizuri kabisa.

Kauli hii ya Spika Ndugai imenishangaza sana na inatoa tafsiri moja tu, kuwa, bodaboda ni sekta iliyoajiri watu hatari, majambazi, wavuta unga, vibaka, wabakaji na wauaji wa wananchi na hivyo hatari zaidi kwa wabunge.

Hii si kweli hata kidogo Spika Ndugai. Ni kitu ambacho mimi sikubaliani nacho 100%. Umekosea kutamka hili hadharani kiasi hicho. Uungwana ni kutoa ufafanuzi upya wa jambo hili. Sema ulikuwa na maana gani. Kisha omba radhi pale ulipoeleweka vibaya.

Well, inaweza ikawa alikuwa na nia njema kwa wabunge wake na hakuwa na nia ya kuonesha dharau yoyote na kushusha hadhi ya bodaboda wote nchini. Lakini ukweli mchungu ni huu, hili litapokelewa kwa hisia mbaya na tofauti kabisa na jamii kwa ujumla na gharama ya kurekebisha "damage" itakayokuwa imesababishwa na kauli yake tu ni kubwa sana.

Ni ushauri tu kwako Bwana Spika Ndugai Job, kuwa, siyo kila kitu lazima ukisemee ndani ya bunge ukimulikwa na makamera ya vyombo vya habari. Mengine, kutana na wabunge wako faragha na mzungumze off the media cameras.

Hili ulilosema siyo jema hata kama nia yako ilikuwa njema kwa wenzako.
 
Mimi naona kasema ukweli kwa upande mmoja na kafisha taarifa sahihi kwetu wananchi kuwa wabunge wengi wameingia bungeni kwa gharama kubwa sana maana kupeleka V8 Nanjilinji, Mbagala kwa Mwarabu, Mpandaswala, Mlele, n.k kupindua matokeo kunahitaji gharama kubwa sana.
 
Hivi hatuwezi kumpigia kura ya kutokuwa na imani huyu mpuuzi?
Labda atimuliwe uanachama wa chama chake.......apoteze ubunge jambo ambalo ni gumu kwasasa.....wabunge hawa sidhani kama kuna mtu anaweza kudhubutu jambo hilo
 
Mimi nilivyomuelewa ni kuwa kamaanisha Wabunge ni Watu muhimu sana hivyo wasijichanganye na huduma zinazowalenga kundi la kina Kajambanani.
 
Moja ya sifa ya mtu kamili na hususani kwa kiongozi wa umma kama alivyo Spika wa Bunge la JMT ndugu Job Ndugai, ni kutumia busara na hekima katika kufanya maamuzi yake iwe ni kwa kutamka kwa maneno au kwa kutenda kwa vitendo.

Leo asubuhi spika Job Ndugai ametamka pasipo umuhimu wala ulazima wowote kwamba, ni hatari kwa wabunge kutumia usafiri wa Bodaboda kwa sababu wao (hawa wabunge) wanapatikana kwa gharama kubwa.

Kiukweli nilipoisikia kauli hii toka ktk kinywa cha kiongozi huyu mkuu wa umma, nilishtuka sana.

Sekta hii rasmi ya usafirishaji imeajiri watu maelfu kwa maelfu Tanzania nzima na wa rika na elimu zote na kuendesha maisha yao vizuri kabisa.

Kauli hii ya Spika Ndugai imenishangaza sana na inatoa tafsiri moja tu, kuwa, bodaboda ni sekta iliyoajiri watu hatari, majambazi, wavuta unga, vibaka, wabakaji na wauaji wa wananchi na hivyo hatari zaidi kwa wabunge.

Hii si kweli hata kidogo Spika Ndugai. Ni kitu ambacho mimi sikubaliani nacho 100%. Umekosea kutamka hili hadharani kiasi hicho. Uungwana ni kutoa ufafanuzi upya wa jambo hili. Sema ulikuwa na maana gani. Kisha omba radhi pale ulipoeleweka vibaya.

Well, inaweza ikawa alikuwa na nia njema kwa wabunge wake na hakuwa na nia ya kuonesha dharau yoyote na kushusha hadhi ya bodaboda wote nchini. Lakini ukweli mchungu ni huu, hili litapokelewa kwa hisia mbaya na tofauti kabisa na jamii kwa ujumla na gharama ya kurekebisha "damage" itakayokuwa imesababishwa na kauli yake tu ni kubwa sana.

Ni ushauri tu kwako Bwana Spika Ndugai Job, kuwa, siyo kila kitu lazima ukisemee ndani ya bunge ukimulikwa na makamera ya vyombo vya habari. Mengine, kutana na wabunge wako faragha na mzungumze off the media cameras.

Hili ulilosema siyo jema hata kama nia yako ilikuwa njema kwa wenzako.
Ndugai hafai kuwa spika ajiuzulu!
 
Amemaanisha wabunge ni binadamu daraja LA kwanza! Yaani miili yao imeumbwa kwa udongo tofauti na huu wa sisi wengine!!

Wanasiasa wanadharau sana!
 
Back
Top Bottom